Hizi bei za nyama kupandishwa kiholela nani wa kuwasaidia Wananchi? Sasa hivi kilo TZS 12,000/ Bodi ya nyama kazi yake nini?

Kuna mwanangu mmoja alikua anatafuta kazi akapewa dili ya kukamata mbwa wanaozurura mtaani awe anawachinja na kuwachuna ngozi alaf kichwa na miguu aizike mbali isionekane.
Mwana alikataa hiyo kazi ila naamini kuna mtu alipewa akakubali na sahivi kuna sehemu watu wanakula mishkaki ya mbwa
 
Nimepitia majukumu ya Bodi ya Nyama, nimeona ina majukumu manne (4) Kwa mujibu wa Sheria iliyoiunda Bodi yenyewe

Ila nimevutiwa na Jukumu lao namba 4, linasema "Kufanya ushawishi na utetezi wa wadau wa tasnia ya nyama"

Sasa hapo sijajua huo utetezi unafanywa Kwa Mlaji ama MuuzajiπŸ™Œ

Wanasema mwenye kisu kikali ndiye atakula nyama, hopefully wenye visu vikali watakuwa Wauzaji ndiyo ambao watakuwa wanatetewa badala ya kutetewa Walaji
 
Unalalama nyama kuongezwa elfu mbili, ila umeme magu alituachia tuvute kwa 27,000! Ila ukapandishwa mpaka 321,000! Hilo ulichekelea acha ccm itambe kila mtu atakula urefu wa kamba na alipopeleka mboga!
 
Soko La Utalii Arusha pamoja na Uwapo wa Viwanda Vikubwa vya Bidhaa za Nyama kama Eliya Food, Happy Sausage, Arusha Meat na Meat King Distributors LTD vinachangia Upandaji wa Bei Ya Nyama kiholela.

Kukua kwa Soko la Nyama Ya Tanzania Huko Uarabuni pia ni sababu kubwa ya kupanda bei ya nyama kwa sababu inakuwa adimu.

Waarabu wnanunua Wanyama wakiwa hai kwa wingi hivyo kusababisha upungufu mkubwa kwa soko la ndani.

Tabia ya Wamasai Kujilimbikizia Mifugo pia ni sababu moja wapo lakini pia uwepo wa Madalali katika minada ya mifugo ni sababu by ngine kubwa ya Ongezeko kubwa la Bei ya Nyama.
 
Nyama zinapanda ndege na meli zinaenda kiliwa ng'ambo,
Msisahau mlishangilia mauzo yanyama kwenye masoko yakimataifa.
 
hawajuwi kuwa Mama kafunguwq masoko ya Dubai na Saudi Arabia.
 
Kuleni panya, si nyama pia? Mliona Mtwara wanalalamikia bei ya nyama huko?

Wanapeleka panya na ndezi kama hawana akili vizuri.

Mipaka yote iliyojazana mitaani, kama huna pesa ya ng'ombe kula paka.
Ivi
Ndezi ni mnyama gani? Ikipatikana picha itapendeza, Nipo curious kumfahamu. Mimi nili dhania ndezi ni neno la kiswahili liki maanisha mtu mzubaifu/mshamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…