#COVID19 Hizi chanjo za Corona zinaenda kuondoa herd immunity tuliyoipata nchini

Nakuonya Corona Haipendi kabisa Dharau
Unaelewa Jinsi ilivyomalizana na Mzee Meko, Yule Mzee Mwendakuzimu
Hahaha, ila Corona ilikuwa ni mpango wa Mungu wanaomsema hawa jamaa, ikatuondolea kero ndani ya nchi! Ukitaka kujua jamaa alikuwa jinga ni vile kafa na gazeti lake la kutukana watu limekufa (Tanzanite), alikokuwa anaelekea huku mwishoni angeipeleka nchi kwenye vita, hakuwa mpenda amani hata kidogo
 
Mungu hajaribiwi, fungeni hospitali zote mwende kwenye maombi ili muone matokeo yake. Ikiwa Moses Kulola bingwa wa maombi alifia hospitalini yatosha kusema ACHENI UZWAZWA.
 
Idadi ya waliokufa mpaka sasa ni 714. Kuna idadi ya wagonjwa wanaopata naafu pia. Kwa ujumla suala zima la corona lipo kitakwimu zaidi kuliko haya masuala ya ramli.
 
Kwani unatumia biblia ipi ? KjV, AV , NKJV,....au biblia nyengine kati ya mamia ya biblia ?

Mungu wa Biblia hajajifungia kwenye box. Ndio maana ametupa sisi watoto wake Roho Mtakatifu msaidizi anaye ishi ndani yetu ili awe wa kutuelewesha Neno la Mungu. Huyu ni tofauti sana na yule anaye abudiwa mpaka na majini. Huyu wa kwetu ameweka bayana kwamba majini na bwana wao shetani sehemu yao muafaka ni lile ziwa liwakalo moto milele yote kule kuzimu aka jehanamu aka hell.
 
Chai za Biblia hizo zilizoandikwa na watu miaka zaidi ya 2500 iliyopita, hazina proof
 
Kapige mbizi
 
Mungu hajaribiwi, fungeni hospitali zote mwende kwenye maombi ili muone matokeo yake. Ikiwa Moses Kulola bingwa wa maombi alifia hospitalini yatosha kusema ACHENI UZWAZWA.
Hayo ya kufunga hospitali unayasema wewe! Sisi tunasema tulimwomba Mungu mbele ya dunia yote na dunia yote imdshunudia Mungu akituponya!! Ukiangalia yaliyotokea na yanayoendelea kutokea duniani kote huwezi kukwepa kuuona mkono wa Mungu jliotuokoa!! Hata wanaokufuru bado nao Mungu aliwaokoa!! Ndiyo maana wako hai japo wanautumia uhai huo kumkufuru na kumkejeli Mungu. Lakini siku moja watakutana nays siku ya hukumu!!
 
Mungu amempa binadamu maarifa ya kupambana na changamoto katika maisha!
Kupata chanjo sio kumkana Mungu bali ni kuutukuza ukuu wake!Mungu anajionesha kwa namna nyingi!Huenda Chanjo ndiyo jawabu alilolitoa Mungu kupitia mwanadamu kuwakomboa viumbe wake na Uviko!
 
Utukufu wa Mungu Tanzania hakuna anayeweza kuutwaa kwa kutuokoa na Corona.
Walitaka kutuaminisha kuwa kuvaa barakoa na kuchanjwa kumetuokoa na wimbi la 6.

Mungu kaamua kuwafedhehesha watu hawavai barakoa na kuchanjwa wamegoma na hakuna mlipuko.
Wamebakia tu viongozi wakivalia mibarakoa huku nafsi zikiwasuta.

Mungu humurehemu atakaye kumurehemu na hakuna kibwengo wa kuzuia.
 
Huenda Chanjo ndiyo jawabu alilolitoa Mungu kupitia mwanadamu kuwakomboa viumbe wake na Uviko!
Sio kwa chanjo hizi za kihuni.

Hamtaki kutumia tiba asili mnabugia matakataka ya mabeberu eti mnaita chanjo!

Hahahaa chanjoo!!!!
 
Ni kweli kabisa mtoa mada, Mungu huwa hashindwi jambo.
Inashangaza sana pale Kiongozi mkubwa kabisa anapokuwa amepata cheo kabla ya kuanza kutumikia cheo hicho anaapa kwa kushika Kitabu kitakatifu, na anamalizia kiapo chake kwa kusema"MUNGU NISAIDIE" sasa unapofika wakati wa kumtumainia Mungu katika jambo fulani, unakuta kiongozi huyo huyo badala ya kumhusisha Mungu, unakuta anampa kisogo Mungu na kuambatana na kile kinachoitwa Sayansi. Ni aibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…