Hizi Harrier 3rd gen zilivyojazana hapa mjini utasema haziuzwi Mil 70+

Hii changamoto ya kurudisha mileage unaweza kui-outsmart vipi mkuu?, maana mwakani hapo na mimi nataka nijichukulie angalao kitoyota allex
 
Maisha ya DUNIANI banaaaa!!!! Wengine wanatamani gari yako na wewe unatamani magari ya wengine..
Hapa DAR unaweza kufa Kwa presha hasa ukiwa barabarani maana kuna watu wanasukuma ndinga za hatari sana
Mkuu kwa barabarani mimi amani ya moyo huwa napata nikiwa mkoani. mkoani inabidi uwe na gari yoyote tu ila kwa dar unajihisi mnyonge kwa gari zetu za 15M hizi maana kuna watu wanaendesha michuma ni laana.
 
Mkuu kwa barabarani mimi amani ya moyo huwa napata nikiwa mkoani. mkoani inabidi uwe na gari yoyote tu ila kwa dar unajihisi mnyonge kwa gari zetu za 15M hizi maana kuna watu wanaendesha michuma ni laana.
Daaa aisee uko sahihi kabisa. Mi mwanangu tumesoma wote sekondari na chuo sasa yeye ni mbunge yaani mashine anayoendesha ni balaaa. Kuna watu huku duniani wanatamani wale maisha milele.
 
Duuuh 5 milion per month..
Huu uchumi mzuri sana
 
Kma unanunulia Bongo - Ndio unaweza kupigwa. Kama unaagiza moja kwa moja Japan, Hakuna huo ujnga.
Mimi nimenunua magari Hong Kong,Japan na SA kwa kwenda mwenyewe nachozungumza sio kwamba nasimuliwa pana ujanja mwingi upo kwenye magari mazee ila sio makampuni mengi yanafanya huo ujinga na pia wanaangalia soko lao linataka nini kama ni Mileage wanashusha tu.
 
Hizi chuma hata huku Mkoani kwetu nimeanza kuziona ona! Nadhani sasa tako la nyani litaanza kushuka kwa kasi..
 
Hapo kwa lugha nyepesi wewe ni anti-japanese
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…