Hizi ndizo sababu za kutopokea simu za baba yangu mzazi

Mzee ana kijiji kule...
Kile kijiji kinasoma aiseeee sasa shule zikifunguliwa kasheshe mkuu utatamani kuhama nchi
Si jukumu la mtoto kutunza mzazi.

Mzazi ndio mwenye jukumu la kutunza mtoto.

Huyo mzee wako, mwambie bado unajitafuta. Asiweke matarajio ya kukugeuza kitega uchumi wake.

Yeye kama alishaharibu ujanani huko, atulie, avune alichopanda.

Kila mtu awajibike na matendo yake. Asiwatwike nyie ujinga wake.
 
Bado haujamsaidia, hao mentor wako wapi?
 
Mkuu mi sipo mbeya ila dingi yupo pale uyole...
Nuliondoka kule tangu 2021 ndio mpaka leo mana nilienda chuo nikaunga mazima
Yupo uyole ? Unahisi mzee ni muelewa kiasi kuwa nikimface hawezi kuhisi labda nimetumwa kumuweka mbali na kijana wake ?

Nauliza haya ili niende nikiwa full nondo na tayari kwa lolote mdogo wangu
 
Namsikilizia anijibu yupo mbeya wapi baba yake ili nikakae na huyo mwaisa aache kumpa mawazo kijana wake japo pia mimi namtaka kijana nikutane naye nimkataze mishangazi yaani mimi nastruggle kuwapata wanawake alafu dogo anajilia tu
Hahaha mishangazi imelundikana humu jf umeshindwa kujiokotea unahangaika na madanga ya kijana, unaniangusha ujueπŸ˜‚
 
Hahaha mishangazi imelundikana humu jf umeshindwa kujiokotea unahangaika na madanga ya kijana, unaniangusha ujueπŸ˜‚
Hiyo mishangazi unaiona hapa jamvini ila tuulize sisi tunaozama PM kila uchwao kubembeleza penzi ,kati ya kumi ni wawili ndiyo wamama na hao hawataki mapenzi ya kugandana ila eti huduma ya siku au wiki ,sasa dada wewe kuweza ?
 
Hiyo mishangazi unaiona hapa jamvini ila tuulize sisi tunaozama PM kila uchwao kubembeleza penzi ,kati ya kumi ni wawili ndiyo wamama na hao hawataki mapenzi ya kugandana ila eti huduma ya siku au wiki ,sasa dada wewe kuweza ?
Lambisha asali mkuu, kwani zamani kipindi wenzio wanaoana humu we ulienda wapi? Pole sana mkuuπŸ˜…
 
Toa msaada basi babu wenye shida tuko wengi humu..
Acha basiii πŸ˜„

Hata wewe It's hard to believe

Ngumu kutoa msaada cause issues nyingi za kiroho zipo related na Culture ya mtu anapotokea tatizo linakuja kwamba watu wengi wapo kwenye mtego wa kiimani

Ila the way alivyoongea tu hapo aliposimulia Baba yake Huwa ana mtokea na kumwambia aseme shida zote atamsaidia Binafsi nimemuelewa Tena sana πŸ˜„πŸ˜„πŸ€£πŸ€£

Kazi anayo I felt sorry for him
 
Unamvimbia alie sababisha uwepo ?
Haikua lazima yeye ndio asababishe uwepo wake.

Unaweza na ungeweza kuzaliwa na mtu yeyote yule, mahali popote pale.

Kwanza wazazi walikuwa kwenye starehe zao za kunyanduana tu.

Hakuna aliyejua au anayejua atazaliwa wapi na atazaliwa na mzazi yupi.

Sisi wote ni matokeo ya watu wawili walioamua kusex kwa starehe zao tu!
 
Yupo mbeya mkuu
Sasa na wewe si upo Mbeya hapo hapo? Umenikumbusha kuna kipindi issue km hio ilinipa mother mzazi alipandisha pressure aliposikia nimeondoka sehemu ghafla akapiga simu sikupokea mother pressure juu mpaka akaenda kulazwa nakuja kucheck nimefika missed call zake kibao kucheck naambiwa pressure imepandisha pressure kwa sababu yangu kalazwa. Sababu nini niliondoka ghafla na hawakua wanajua naenda wapiu ingawa nilitoa taarifa akaajua sitorudi ndio akaanza kunipigia sikupokea simu ilikua silent, ila baadae alivyoruhusiwa hospital tukaongea tu vizuri, sasa sikia wewe upo Mbeya au upo wapi?
 
Kula dislike kwanza.

Stori yako imeanzia kati ,hujatuambia tofauti yako na mzee wako ni nini mpaka hutaki kupokea simu zake.

Je una uhakika anataka kukuomba hela?

Nini kimepelekea mpaka hutaki kabisa mawasiliano na ndugu zako?
 
Bwana! Hivi vitisho sasa unajua? Jaribu kuongea naye umsaidie inawezekana tu kila jambo linawezekanika!
 
Ipo hivi mkuu..
Naongea haya najua kuna ant angu ni mfatailiaji sana wa hii mitandao ata akiona poa tuu..

Hapo mwanzo nimewahi ambiwa na naNdgu kuwa ukoo wetu watoto wote wa kiume tuna shida.

Na hii shida inasababishwa na maagano ya matambiko sijui.

Then nikaambiwa mimi baba angu ni mtu wa kitabu sana hivo aamini mambo ya mila hivo kaachana na mila

Ukija kwangu mimi binafsi ni mtu wa imani sijui kama nipo stable au laaa lakini kwa sasa hata nikiwa naenda kufanya ibada najua hii ya leo sijafanya kitu nimecheza tu..

Mkuu nimesoma dini kiasi chake maana kwa mzee kule auala la dini ni bora utoroke shule uende madrasaa hivo imani ninayo ila kadri siku zilipokua zinaenda sula la imani kwangu likawa dogo sana.

Mi siamini kwa mambo ya ushirikina na sijawahi fanya chichote kinachohusiana na ushirikina lakini pia kwa upande wa sir God sipo deep kama zamani yaan nipo partially

Hi ni kutokana na utandawazi na kujua mambo mapya kutoka kwa kina Kiranga na Infropreneur hii ikafanya niamini kuwa mafanikio ni about hardwarking .....

Kama ni ishu ya kiroho basi naweza sema hii equation yangu haijawa balanced
 
Kwanza pole kwa changamoto mkuu
Labda nikwambie kitu kimoja mfumo wa maisha ya ki africa tumejengwa katika hofu ili tudumae na tutawaliwe vyema, kwenye maisha hakuna mtu anayekudai au unayemdai isipokuwa tu kama una mtoto, mtu yeyote asikupe lawama kuwa humsaidii ukiikubali na kuijali hii lawama utadumaa na hutakua ,
Jitengeneze ,jipe mda na pambana,
Kama hawatakuwa na subira iwe wazazi au ndugu achana nao, wew ndo mwamuzi wa maisha yako, hii falfasa ya kiafrica kuwa unazaa mtt ili aje akusaidie ndo inazalisha hizi lawama
 
Kweli unamatatizo Kichwani.

Hakuna Jambo linalokusumbua hapo. Ni wewe kuwa weak kupenda validation na kuwa Impress watu akiwemo Mzee wako,

Pokea simu. Kama huna mwambie huna.

Akitoa lawama mkatie simu.
Usipende kumpigia simu. Siku akikuuliza kwa nini mwambie kwa sababu Kila ukimpigia amekuwa mtu wa lawama.

Usimjibishe vibaya, ila mwambie ukweli kwa busara.

Akimaindi akakutukana kata Simu.
Akikuuliza kwa nini unakataga simu mwambie hupendi kumwona anakukosea heshima wakati wewe unamheshimu kama Baba. Akianza kulalamika mwambie mtazungumza baadaye upo kazini.

Linalokusumbua ni Jambo dogo Sana.
Usitake kuwa perfect kwa watu wasiowakamilifu. Usitake kutimiza wajibu wote kwa watu walioshindwa kutimiza wajibu wao wote. Huo ni utumwa.

Maisha ni yako.
Unaanza wewe ndipo wanafuata wengine.

Furaha, Amani na heshima yako ni muhimu kuliko Baba au mama, au mtoto au mke au mtu yeyote. Na huo sio ubinafsi. Bali ndivyo maisha yanataka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…