Hizi ndizo sababu za kutopokea simu za baba yangu mzazi

Hizi ndizo sababu za kutopokea simu za baba yangu mzazi

Kweli unamatatizo Kichwani.

Hakuna Jambo linalokusumbua hapo. Ni wewe kuwa weak kupenda validation na kuwa Impress watu akiwemo Mzee wako,

Pokea simu. Kama huna mwambie huna.

Akitoa lawama mkatie simu.
Usipende kumpigia simu. Siku akikuuliza kwa nini mwambie kwa sababu Kila ukimpigia amekuwa mtu wa lawama.

Usimjibishe vibaya, ila mwambie ukweli kwa busara.

Akimaindi akakutukana kata Simu.
Akikuuliza kwa nini unakataga simu mwambie hupendi kumwona anakukosea heshima wakati wewe unamheshimu kama Baba. Akianza kulalamika mwambie mtazungumza baadaye upo kazini.

Linalokusumbua ni Jambo dogo Sana.
Usitake kuwa perfect kwa watu wasiowakamilifu. Usitake kutimiza wajibu wote kwa watu walioshindwa kutimiza wajibu wao wote. Huo ni utumwa.

Maisha ni yako.
Unaanza wewe ndipo wanafuata wengine.

Furaha, Amani na heshima yako ni muhimu kuliko Baba au mama, au mtoto au mke au mtu yeyote. Na huo sio ubinafsi. Bali ndivyo maisha yanataka
Umemaliza kila kitu, huyu kinachomsumbua ni validation,
 
Mimi huwa nashangaa sana, waafrika wametengeneza utamaduni wa kutaka kusaidiwa, utafikiri msaada ni haki yao.

Mtu ashafeli huko, amechezea ujana wake anaanza kufosi kusaidiwa utafikiri ni haki yake.

Msaada ni hiari.

Msaada si lazima wala si haki.

Wazazi wapumbavu wanaozaa bila malengo ndio huwageuza watoto vitega uchumi.

Wao walishaharibu huko ujanani, wanaanza kusumbua watoto uzeeni.

Wazazi wa namna hii ni kuwaacha, wakafie mbelee!!

Hii Dunia kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe.

Wakusaidiwa na kupewa matunzo ni mtoto kwanzia amezaliwa mpaka umri wa miaka 18 to 20 years.

Baada ya hapo kila mtu ajipambanie mpaka kufa.

Kusaidiana kupo kwenye hali za dharura na za msingi tu, Sio kila wakati li mtu linataka kutumiwa hela tu!
min -me unavyofurahia sasa🙌🏾
 
Maviongozi mafisadi kazi yao ni kujaza minofu ya kuku kwenye matumbo yao , hayaweki mazingira mazuri ya maisha bora kwa kila mtanzania , vijana wana ishi kwa kutegemea kubeti tena wasomi , jumapili nao wachungaji wanakazia shida zao ni matatizo ya kiroho wasali sana, wewe unaona hapo kuna mabadiliko?
Jamani😂 leo nimedownload app ya kubet nianze kubet pia sio poa aisee🤣
 
Ndo hapo sasa, wewe umeleta kiumbe duniani unawajibu wa ku invest effectively ili kikue na kustawi ili kuendeleza kizazi bora na imara, ila ww uliishia kusomesha tu, unataka mtt na ka mshahara kake aje azibe failure zako zote za ujanani , hii ndo imesababisha chain ya umasikini isiishe, wazazi wabadilike wawape nafasi watt wao, ya kukua na kustawi
 
Huo ndio ukweli, nchi za wenzetu wapo straight sana kwenye mambo yao , mzazi asipojipanga lazima awe homeless na watoto wanajipambania kivyao , hakuna cha matatizo ya kiroho serikali wameweka mifumo ya ajira na biashara ya kueleweka ushindwe tu mwenyewe
Mi ndio nilishashindwa kuendekeza mzazi au mtoto, kama haiwezekani silazimishi, zamani nilikuwa nakasirika mama hanipi mtaji na pesa anayo! Kuna siku nilimind hanipeleki kwenye biashara zake namimi nijifunze mara kuna siku kaninyima funguo nikajifunze drvng, nikawa namuona mbinafsi tu, nilivyojifunza kukomaa mwenyewe naona sikuhizi ananuna yeye sijisogezi kumtafua😂
 
Mkuu nipo vizur nafnya flat design vzr sana...
Aiseh, ONGEZA juhudi kama HUNA KITU kingine chakufanya zama Instagram tengeneza content kama za akina deo, Fatboy n.k.

Au UNAWEZA kujifunza commercial product design Kisha una sponsa Zina wateja unapiga PESA chache mwanzoni LAKINI ukifocus UNAWEZA fungua baadae HATA ofisi ya photoshoot picha na mademu wanapenda sana tafuta location wakati unasubiri ajira . UNAWEZA anzia geto lako likawa ofisi humo humo unapika ugali.

Otherwise labda saidia fundi SABABU najua hiyo field Kupata ajira ni ngumu MPAKA uwe mbunifu kama kina hance.

Ukubalike studio za tv MANAKE WATU wamekuona au UNAWEZA nunua dynamic au condenser mic na kufanya matangazo ya video na sauti kama una sauti nzuri kimsingi tangazo MOJA ni 50k. Mambo ya jingle zinanunuliwa na radio


Ni idea TU.
 
Mi ndio nilishashindwa kuendekeza mzazi au mtoto, kama haiwezekani silazimishi, zamani nilikuwa nakasirika mama hanipi mtaji na pesa anayo! Kuna siku nilimind hanipeleki kwenye biashara zake namimi nijifunze mara kuna siku kaninyima funguo nikajifunze drvng, nikawa namuona mbinafsi tu, nilivyojifunza kukomaa mwenyewe naona sikuhizi ananuna yeye sijisogezi kumtafua😂
Ila alipaswa akufundishe , siku akistaafu yeye biashara zake zitakufa
 
Baada ya kusoma uzi huu nikahitimisha kwamba watanzania tuna changamoto ya kuwa wazi, kumwambia mtu ukweli na kuishi uhalisia. Sio wewe tu mleta mada, ni wengi tupo hivyo.

Tunataka kuaminisha watu wetu kuwa kila kitu kipo sawa, ila kiuhalisia we're bleeding inside.

Mkuu, kiwa wazi na utakuwa huru.
 
Wakuu Salama humu ndani...

Kama umesoma uzi wa mimi kutaka sana kukaa kijinini basi mambo yalianzia huku

Wakuu mimi nipo salama kabisa physical lakini kichwani hapana nina pitia mengi sana kiasi ambacho nahitaji msaada wa karibu wa mawazo pamoja na cancelling...

Sio kwamba jamii nayokaa nayo haina watu wazima, au ndgu jamaa na marafiki.

Wapo lakini ni wale ambao wa kusikiliza tu hakuna kitu wata change au watabadilisha.

Napandisha huku kutokana na hii ni kama familia kwangu maana nipo huku toka nikiwa shule ya msingi.

Pia huku ni sehemu ambayo nakua huru kutoa ya moyoni tofauti na unapo mfuata mtu kuongea nae ni mara kumi uongee na mtu baki kuliko kuongea na ndgu maana unaweza kuta unatengeneza tatizo juu ya tatizo.

Ishu iliyopo hapa ni kwamba nina mwezi sijapokea simu za mzee..

Nina mwezi mzima sijapokea simu za baba mzazi na chanzo cha kutokupokea ni kuogopa lawama na kuogopa majukumu.

Tangu nikiwa chuo nimesoma kwa namna ya kukwepa SIM za mzee kiasi ambacho nikikaa mwenyewe huwa nawaza kwann nina haki ya kuishi ikiwa mambo yangu ndo hivo najitafuta lakini bado mzee nae anasema anahitaji pesa.

Nilovotoka chuo nilijitenga mbali kabisa na ndgu yaani hakuna mtu ananijua wala hakuna mtu wa nyumbani anajua nakaa wapi zaidi ni marafiki zangu wawili ambao nimesoma nao advance.

Ila sasa baada ya ndgu kujua nipo huku daah hali imekua si hali tena maana zitapigwa simu nende kusalimia huku na kule kitu ambacho ni ngumu huku harakati zetu tunajua wenyewe .

Mara moja moja muhindi akitu bless ndo tunavimba au ndo hivo JITU BANDIA akituma odds za uhakika tunaluka nazo

Mimi ni Mtoto wa kwanza..

Mtoto wa kwanza wanasema anaandamwa na mambo mengi basi kwangu mimi nahisi imekua hivo hivo.. maana nimetoka chuo tatu mambo yamekua tofauti kama nilivyozania...

Natamani sana kumsaidia mzee lakini how naanzaje ikiwa mimi mwenyewe sina permanent au temporary work ambayo naweza pata hata laki tatu per monthly

Sina source ya income ambayo naweza saidia familia yangu even mimi mwenyewe life yangu mimi tia maji tia maji.

Hii ni kwa baba upande wa mama kidogo mama angu anapambana alhamdullilah yeye yupo huko mbali kabisa mara nyingi yeye ndio namuombaga pesa maana yeye alishatengana na baba kitambo sana ...

Shida inayokuja hapa ni kuwa nimekua mpaka naota kuhusu baba ananitokea na kuniambia vitu mbali mbali

Ndoto ya kwanza niliwahi ota baba anafanya kazi nzito ambayo mimi nikawa nashangaaa mbona kazi nzito hivi alafu malipo sisimizi

Ndoto ya PILI ni hii ya leo nimeota nimekutana na baba msikitini..

Mda ambao mi natoka msikitini tena nimetoka bila kuswali nilikua nazuga tu humo ndani. Nakuta mzee yupo nje nikakutana nae tukawa tunatembea akawa anasema "" mwanangu sema matatizo yako yote unayopita "" sijajua kwann alisema hivi. Mshana Jr naomba msaada wa hizi ndoto mana yake nini

Ukizingatia mzee tingi ni kama mganga wa kitabu yule wa kutengeneza makombe

Ndio maana naposema nataka niwe mbali na hii system Namaanisha kabisa hili suala linaumiza sana.

Unaweza pokea ukaambiwa maneno ambayo ukabaki unaumia moyoni na unajua kabisa huna cha kufanya,

Mi naamini katika stage hii ya utafutaji unakua unstable kaisi ambacho unakuta sometimes unaweza ahawishika uingie kufanya mambo ya ajabu ili tu unyamazishe wazazi....

Father hawaelewi kabisa hili nalopitia mimi anaona namnyima pesa wakati pesa nayopata ni hv hv mpaka umuokote mdada tena sio mdada ni mmama awe ana pesa zake ndo anakusaidia.

Hii imepelekea niwe mbali na kitu kinaitwa kuhonga.. nimelemazwa na hawa wamama.

Naomba msaada kama kuna mtu mzima yupo.mbeya anaweza nicheki nikaongea nae kila kitu kuhusu hii ishu ili anisaidie kuongea na Baba yangu...a

Mimi nashindwa na naogopa..
Nikipokea atauliza kwann upokei simu zangu.. kuna kitu nimekukosea mwanangu.

Just imagine maneno kama hayo ni very painful wakuu

Asanteni wakuu...🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
Naona kama utoto unakusumbua
 
Back
Top Bottom