Hizi ndizo sababu za kutopokea simu za baba yangu mzazi

Hizi ndizo sababu za kutopokea simu za baba yangu mzazi

Lambisha asali mkuu, kwani zamani kipindi wenzio wanaoana humu we ulienda wapi? Pole sana mkuu😅
Sasa hivi nimeanza kutafuta mialiko mbalimbali ya warsha na matamasha ya wamama najua huko sitakosa .

Juzi nilikuwa Rungwe kwenye tamasha fulani ,nikakuta mimama ni mibonge mibonge tu alafu inatembea kwa shida ,nikajiwqzia mimi na hili tumbo langu ,nimpate tena mwanamke mwenye kitambi na anatembea kwa shida mbona itakuwa vichekesho basi namba sikuchukua ila bado nasaka
 
Si jukumu la mtoto kutunza mzazi.

Mzazi ndio mwenye jukumu la kutunza mtoto.

Huyo mzee wako, mwambie bado unajitafuta. Asiweke matarajio ya kukugeuza kitega uchumi wake.

Yeye kama alishaharibu ujanani huko, atulie, avune alichopanda.

Kila mtu awajibike na matendo yake. Asiwatwike nyie ujinga wake.
Mkuu tatizo kujibu hvo unaona ni sawa kabisa
 
Nje ya mada: Siku baba huyo akivuta shuka "akifa", at some point kwenye life yako, utatamani upate mtu wa kumpigia simu, umuite baba hutampata.

Ushauri: Mtendee vizuri baba yako bwamdogo, hutakuwa nae muda wote wa maisha hako baba yako. Na yeye, alikuwa anakutana na hali ngumu kama mwanaume. Hali unayopitia wewe hakuna mwanaume hapitii, lakini usikubali uanaume ukutoke. Kamata simu ya mshua, mweleze situation yako, yeye pia anayajua maisha ya kiume.

Kuna watu wanatamani wapate baba hata wa kufikia, hawana.
Punguza utoto, grow up, be a man.
 
Ipo hivi mkuu..
Naongea haya najua kuna ant angu ni mfatailiaji sana wa hii mitandao ata akiona poa tuu..

Hapo mwanzo nimewahi ambiwa na naNdgu kuwa ukoo wetu watoto wote wa kiume tuna shida.

Na hii shida inasababishwa na maagano ya matambiko sijui.

Then nikaambiwa mimi baba angu ni mtu wa kitabu sana hivo aamini mambo ya mila hivo kaachana na mila

Ukija kwangu mimi binafsi ni mtu wa imani sijui kama nipo stable au laaa lakini kwa sasa hata nikiwa naenda kufanya ibada najua hii ya leo sijafanya kitu nimecheza tu..

Mkuu nimesoma dini kiasi chake maana kwa mzee kule auala la dini ni bora utoroke shule uende madrasaa hivo imani ninayo ila kadri siku zilipokua zinaenda sula la imani kwangu likawa dogo sana.

Mi siamini kwa mambo ya ushirikina na sijawahi fanya chichote kinachohusiana na ushirikina lakini pia kwa upande wa sir God sipo deep kama zamani yaan nipo partially

Hi ni kutokana na utandawazi na kujua mambo mapya kutoka kwa kina Kiranga na Infropreneur hii ikafanya niamini kuwa mafanikio ni about hardwarking .....

Kama ni ishu ya kiroho basi naweza sema hii equation yangu haijawa balanced
🎤 Iceberg9 Njoo
 
Kwanza pole kwa changamoto mkuu
Labda nikwambie kitu kimoja mfumo wa maisha ya ki africa tumejengwa katika hofu ili tudumae na tutawaliwe vyema, kwenye maisha hakuna mtu anayekudai au unayemdai isipokuwa tu kama una mtoto, mtu yeyote asikupe lawama kuwa humsaidii ukiikubali na kuijali hii lawama utadumaa na hutakua ,
Jitengeneze ,jipe mda na pambana,
Kama hawatakuwa na subira iwe wazazi au ndugu achana nao, wew ndo mwamuzi wa maisha yako, hii falfasa ya kiafrica kuwa unazaa mtt ili aje akusaidie ndo inazalisha hizi lawama
Mimi huwa nashangaa sana, waafrika wametengeneza utamaduni wa kutaka kusaidiwa, utafikiri msaada ni haki yao.

Mtu ashafeli huko, amechezea ujana wake anaanza kufosi kusaidiwa utafikiri ni haki yake.

Msaada ni hiari.

Msaada si lazima wala si haki.

Wazazi wapumbavu wanaozaa bila malengo ndio huwageuza watoto vitega uchumi.

Wao walishaharibu huko ujanani, wanaanza kusumbua watoto uzeeni.

Wazazi wa namna hii ni kuwaacha, wakafie mbelee!!

Hii Dunia kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe.

Wakusaidiwa na kupewa matunzo ni mtoto kwanzia amezaliwa mpaka umri wa miaka 18 to 20 years.

Baada ya hapo kila mtu ajipambanie mpaka kufa.

Kusaidiana kupo kwenye hali za dharura na za msingi tu, Sio kila wakati li mtu linataka kutumiwa hela tu!
 
Sasa hivi nimeanza kutafuta mialiko mbalimbali ya warsha na matamasha ya wamama najua huko sitakosa .

Juzi nilikuwa Rungwe kwenye tamasha fulani ,nikakuta mimama ni mibonge mibonge tu alafu inatembea kwa shida ,nikajiwqzia mimi na hili tumbo langu ,nimpate tena mwanamke mwenye kitambi na anatembea kwa shida mbona itakuwa vichekesho basi namba sikuchukua ila bado nasaka
Nimecheka jmn😂 kila siku mnatushauri tusichague sana, ona wewe ambavyo hutaki walioshiwa uroto🤣

Sikukuu ya wanawake imepita walikuwa wamekusanyana sana ungecheza mitaa hiyo faster sana unajiokotea kitu🤗
 
Mkuu hiyo hali hata nimi nilipitia wakati ndio nimepata kibarua, ndugu walinisakama sana kutaka misaada. Ilikuwa mbinde kwa sababu wakati nahitaji kujipanga ndugu wanataka kunipa majukumu ya familia zao.

Sio hali nzuri hata kidogo kuikubali. Ukweli utakuweka huru. Tafuta muda wa kumchana ukweli mzee, atachagua mwenyewe kama aelewe au asielewe, lakini wewe umempa ukweli
 
Mkuu tatizo kujibu hvo unaona ni sawa kabisa
Unapotaka kumuelezea mtu kweli unamchana live, hata kama ni mzazi.

Mwambie wewe bado unajitafuta, bado huna uwezo wa kumsaidia yeye.

Afikirie namna nyingine ya kuendesha maisha yake. Asiweke matarajio makubwa kwako.

Kama haelewi sasa, una mblock kila mahali. Akafie mbele!
 
Dahh watupe ajira tu tuone kama kweli tuna matatizo ya namna hii au ni stress za maisha kiujumla..
Maviongozi mafisadi kazi yao ni kujaza minofu ya kuku kwenye matumbo yao , hayaweki mazingira mazuri ya maisha bora kwa kila mtanzania , vijana wana ishi kwa kutegemea kubeti tena wasomi , jumapili nao wachungaji wanakazia shida zao ni matatizo ya kiroho wasali sana, wewe unaona hapo kuna mabadiliko?
 
Back
Top Bottom