Kambi sawa zitarekebishwa
Hezbollah command centre hairekebishiki. Maofisa wa Iran hawarudi, maofisa wa Hezbollah hawarudi, Hamas haivamii tena.
Bado yajayo kwa Iran hanafurahisha.
F-35 zitaletwa mpya kutoka USA hilo linafahamika na makao makuu yatajengwa upya.
Makao makuu gani yalipigwa? Kila kilichopigwa na Israel picha zipo, nipe evidence makao makuu yamepigwa. Makombora yalikuwa yanajidondokea bila shabaha halisi.
F-35 Israel inanunua, au onyesha ni fighter jets gani "zililetwa Israel" bila Israel kutoa hela. Na zinaletwa za nini wakati hamna zilizoharibika.
Kwanza F-35 za Israel ni za kipekee kuliko F-35 nyinginezo, ni 'Adir'. Haubebi ndege from nowhere ukaleta Israel zikatumika. Na nani atazitoa, na Lockheed Martin hawazifyatui bila order kama gari.
Utaona kama Israel itanunua ndege yeyote kabla haijaijibu Iran.
Ila wewe jamaa huwa hukosi sababu,si wewe juzi ulisema Iran na makombora yake yasiyo na madhara haina cha kufanya!?
Makombora hayana mashara ndio. Cha kufanya ilikuwa nacho, ni kufyatua makombora yasiyo na madhara. Siku ile shambulizi la magaidi wawili kwa bunduki lilileta madhara makubwa kuliko shambulizi la makombora 200.
Mkuu huwa napendaga kujadiliana na wewe kwasababu una accuracy kubwa ya kujadili hoja,Iran sio Hizbollah na wala sio Hamas.
Iran ni nchi kamili na ina jeshi kamili na ina kila aina ya silaha ambayo Israel anayo.
Iran haina fighter jets, haina refuering tanks, haina airlifters, haina air defence systems covering the vast country, haina nukes, haina subs.
Iran haifanani kwa lolote na Israel kijeshi. Iran ina jeshi limekazania kujihami, kujilinda. Israel ina jeshi linalosisitiza kushambulia. Kwa sera za Israel ni bora iwe na attack jets kuliko kuwa na interceptor jets.
Iran ina idadi ya wanajeshi wengi ambayo haina maana kwa mantiki hii sababu haipakani na Israel, sasa watapita wapi?
Pia ina makombora mengi na drones.
Kumbuka Israel haijawahi tumia ballistic missile wala ICBM labda cruise tu. Wote hawa watatumia anga kushambuliana na Iran haina air dominance.
Hata katika rank ya majeshi Iran yupo juu ya Israel,je uongo!?
Pia nilichogundua Iran inapiga kulingana na makosa,Ile mwezi May alitumia drone za taratibu na makombora mepesi,ila awamu hii katuma full ballistic na hypersonic missiles zilizotembea dakika 15 kwa kilometa 2000.
Sasa tunataka ajibu huyo Israel halafu tuone Iran itachomfanya.
Hivi una habari mkuu kama jana tu Israel imepoteza askari 14 walipojaribu kuingia ndani ya Lebanon kwa kupigwa na hizbollah!??
Askari 14 kwenye vita serious ni idadi ndogo sana labda uzungumzie vita njaa kama Vita ya Kagera. Hujaona casualties za Hezbollah na wala sio kila siku Israel itapoteza 14. Na kawaida ya invading forces inatarajiwa kupata casualties 3:1 kwa defending forces kama zina nguvu sawa. Ila sababu Israel ina nguvu, Hezbollah ndio watachakaa zaidi.