and 100 others
JF-Expert Member
- Feb 3, 2023
- 3,707
- 12,367
Hizi ndege wangeshazileta lakini kupanda tu ndege ya kivita kama F16 lazima ufanyiwe testing kwenye simulators, wanaziita centrifuge machines, kumbuka kasi ya ndege ya kivita inasababisha acceleration forces, ile acceleration hupelekea kama kuvutwa hivi wanaita G force.
Ndege vita inaweza fikisha hadi 9G , maana yake ile gravity ya dunia inakuwa mara 9.
Hivyo marubani wanaweza ku withstand huo uvutano usababishwao na acceleration kutokana na mafunzo maalumu, vifaa maalumu na techniques mbali mbali za upumuaji n.k
Hizo forces hupelekea kuathiri hadi heart rate, mzunguko wa damu n.k na hupelekea pilots hadi kuzirai wakiwa kwenye testing ya hizo machines.
Kwa mtu average huwezi withsatnd hizo G forces, utazirai au ukafa kabisa.
Huo uvutano unaweza kusukuma damu kwa wingi kuelekea kichwani, au kuelekea miguuni ndipo hapo mtu huzirai..
Kwa hii hypersonic yenye speed karibu mara 7 ya ndege vita, hata rubani wa F16 hawezi himili hio G force.
Ingekua wameshatengeneza hadi ndege za abiria unasafiri masaa ma 3 upo USA au China.