Ndoa kama ndoa haina tatizo lolote. Tatizo lipo kwa wanandoa.
Iko hivi;
Niifananishe ndoa na gari. Gari inahitaji dereva mmoja tu kwa wakati mmoja. Hawezi kuta gari inaendeshwa na madereva 2 kwa wakati mmoja.
Haiwezekani dereva mmoja akanyage brake halafu mwingine akanyage accelerator na hiyo gari itembee. Lazima kutayokea mkwamo wa safari.
Ndoa inapaswa kuwa na dereva mmoja na msaidizi mmoja na abiria. Dereva akishika usukani aachwe aendeshe gari bila kusumbuliwa na msaidizi.
Msaidizi akae kwenye nafasi yake ya usaidizi na dereva akae kwenye nafasi yake ya udereva, kila mmoja atimize majukumu na aheshimu mipaka yake.
Dereva ni Mume, msaidizi ni Mke na abiria ni watoto (kama wapo). Yeyote atakayeifuata hii kanuni atafurahia maisha yake ya ndoa.