Hizi ni ajali tatu zilizoniachia kumbukumbu mbaya zenye simanzi kwenye akili yangu

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Hizi ni ajali ambazo hadi leo zimeniachia simanzi na kumbukumbu mbaya kichwani mwangu. Sikupoteza ndugu wala mtu yeyote wa karibu ila ziliniumiza mno.

1. Ajali ya moto kwenye bweni la wasichana Shauritanga sec, Rombo

Hii ajali ilitokea usiku wa tarehe 18 June 1994. Bweni lilishika moto na kuteketeza mabinti wadogo waliokuwa bwenini. Ninakumbuka tukiwa ibadani kanisa katoliki la Lambo, Machame tarehe 19 June 1994, tulitangaziwa kutokea kwa hiyo ajali huko Rombo. Hadi leo ninahuzunika sana.

2. Ajali ya MV Bukoba mwaka 1996

Siku ninasikia taarifa za hii ajali nilikuwa nimetoka shule ndo nikakuta nyumbani watu wanaongelea. Ninadhani hii ajali ni mojawapo iliyowahi kuhuzunisha nchi nzima. Pia ni ajali iliyoweka wazi kuwa nchi yetu ilikuwa maskini mno wakati ule.

3. Ajali ya ndege pwani ya Gabon iliyoua timu nzima ya mpira ya Zambia.

Hii ajali maarufu kama "Gabon disaster 1993" ilikuwa ni ajali ya ndege iliyoanguka kwenye bahari ya Atlantic huko Gabon muda mfupi baada ya kupaa toka Libreville kuelekea Dakar, Senegal kwa ajili ya mechi ya kufuzu kucheza kombe la dunia. Watu wote 25 wakiwemo wachezaji, makocha na viongozi walifariki.

Kilichonihuzunisha zaidi ni kuwa ndege iliyowabeba ilikuwa tayari haifai kwa matumizi. Na hata siku ya safari ilionekana kuna tatizo kwenye engine. Kulikuwa na uzembe mkubwa.
 
Kalusha Bwalya na Charles Musonda walipona kwenye hiyo ajali kwa kuwa walikuwa wanacheza ligi za Europe hivyo wao walitokea huko Ulaya moja kwa moja.
 
Hizi ni ajali ambazo hadi leo zimeniachia simanzi na kumbukumbu mbaya kichwani mwangu. Sikupoteza ndugu wala mtu yeyote wa karibu ila ziliniumiza mno.

1. Ajali ya moto kwenye bweni la wasichana Shauritanga sec, Rombo

Hii ajali ilitokea usiku wa tarehe 18 June 1994. Bweni lilishika moto na kuteketeza mabinti wadogo waliokuwa bwenini. Ninakumbuka tukiwa ibadani kanisa katoliki la Lambo, Machame tarehe 19 June 1994, tulitangaziwa kutokea kwa hiyo ajali huko Rombo. Hadi leo ninahuzunika sana.

2. Ajali ya MV Bukoba mwaka 1996

Siku ninasikia taarifa za hii ajali nilikuwa nimetoka shule ndo nikakuta nyumbani watu wanaongelea. Ninadhani hii ajali ni mojawapo iliyowahi kuhuzunisha nchi nzima. Pia ni ajali iliyoweka wazi kuwa nchi yetu ilikuwa maskini mno wakati ule.

3. Ajali ya ndege pwani ya Gabon iliyoua timu nzima ya mpira ya Zambia.

Hii ajali maarufu kama "Gabon disaster 1993" ilikuwa ni ajali ya ndege iliyoanguka kwenye bahari ya Atlantic huko Gabon muda mfupi baada ya kupaa toka Libreville kuelekea Dakar, Senegal kwa ajili ya mechi ya kufuzu kucheza kombe la dunia. Watu wote 25 wakiwemo wachezaji, makocha na viongozi walifariki.

Kilichonihuzunisha zaidi ni kuwa ndege iliyowabeba ilikuwa tayari haifai kwa matumizi. Na hata siku ya safari ilionekana kuna tatizo kwenye engine. Kulikuwa na uzembe mkubwa.
-Ajali mbaya zaidi ya zote hizo ulizozitaja ni ajali ya Samia kuua maelfu ya vijana wa Kitanganyika October 29th 2025.
 
Nikisikia au kuona neno ajali nakumbuka Treni Dodoma 2002. Damu zilichuruzika kutoka kwenye mabehewa na kutiririka kama maji mtaroni.
 
Hizi ni ajali ambazo hadi leo zimeniachia simanzi na kumbukumbu mbaya kichwani mwangu. Sikupoteza ndugu wala mtu yeyote wa karibu ila ziliniumiza mno.

1. Ajali ya moto kwenye bweni la wasichana Shauritanga sec, Rombo

Hii ajali ilitokea usiku wa tarehe 18 June 1994. Bweni lilishika moto na kuteketeza mabinti wadogo waliokuwa bwenini. Ninakumbuka tukiwa ibadani kanisa katoliki la Lambo, Machame tarehe 19 June 1994, tulitangaziwa kutokea kwa hiyo ajali huko Rombo. Hadi leo ninahuzunika sana.

2. Ajali ya MV Bukoba mwaka 1996

Siku ninasikia taarifa za hii ajali nilikuwa nimetoka shule ndo nikakuta nyumbani watu wanaongelea. Ninadhani hii ajali ni mojawapo iliyowahi kuhuzunisha nchi nzima. Pia ni ajali iliyoweka wazi kuwa nchi yetu ilikuwa maskini mno wakati ule.

3. Ajali ya ndege pwani ya Gabon iliyoua timu nzima ya mpira ya Zambia.

Hii ajali maarufu kama "Gabon disaster 1993" ilikuwa ni ajali ya ndege iliyoanguka kwenye bahari ya Atlantic huko Gabon muda mfupi baada ya kupaa toka Libreville kuelekea Dakar, Senegal kwa ajili ya mechi ya kufuzu kucheza kombe la dunia. Watu wote 25 wakiwemo wachezaji, makocha na viongozi walifariki.

Kilichonihuzunisha zaidi ni kuwa ndege iliyowabeba ilikuwa tayari haifai kwa matumizi. Na hata siku ya safari ilionekana kuna tatizo kwenye engine. Kulikuwa na uzembe mkubwa.
Vipi ya mo29 haiku kuachia kumbukumbu?
 
Back
Top Bottom