Hizi taasisi bila mjomba na mganga anayeeleweka hupati kazi

Hizi taasisi bila mjomba na mganga anayeeleweka hupati kazi

Utakuwa na nyota kali sana

Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.

Mhubiri 9:11
 
watoto wa masikini wakikaza sana wataishia halmashauri za buhigwe ,namtumbo na simiyu ama na mashirika uchwara .

ila ukitaka utoboe kwenye hii list lazima uwe na Godfather huko, ama una ndumba kali.

mashirika na taasis zenyewe ni hizi hapa chini

1.TRA
2.BOT
3.DCEA
4.TISS
5.IMMIGRATION
6.NBS
7.TFRA
8.HAZINA
9.WORLD VISION
10.TCRA
11.DANISH REFUGEE COUNCIL
Bora niwe mchuuzi........
 
Nakuambia sasa hao jamaa pesa ipo sana...Tumekaa na jamaa alifanya kazi mikoa kama 6 ndani ya miaka 10 tu...Ana pesa kinoma ila ni kada.

Sijakukatalia, naomba urudie tena kusoma nilichokiandika, suala la pesa katika idara yoyote Ile , inategemea na kitengo na majukumu.

Hali kadhalika Kwa TISS, inategemea yupo kitengo gani. Sio wote wenye pesa, unataka kuniambia PSU atalingana marupurupu na aliyeko kitengo kingine? Wanatofautiana sana, na wapo wenye pesa ya kawaida kuliko wengi wanavyofikiria.

Huyo umetolea mfano ni miongoni mwa hao wenye vitengo vyenye pesa kutokana na nature ya majukumu yake.

Walio wengi ni ile heshima ya kufanya kazi huko ndio wanachofaidi zaidi. Ndio maana wengine hufikia hatua ya kulazimisha hiyo heshima Kwa jamii.
 
Sijui nikupangie hata taasisi bora ? Utashangaa sana hasa hapo ni 4 tu za maana ...

TISS ni ndoto na watu wanapata wanachomolewq tu kweny ofisi yeyote kutokana na nidhamu zao...Wanapelekwa mafunzo.

Uzuri wa TISS ni mmoja pesa za kutosha kazi chache ...Mda wa free ni mwingi ukipata tasks nzito ujue kuna posho za ziada.
Kumbe... 🤔
 
Maisha,nyakati,uhitaji,elimu na mabadiliko kadhaa kidunia yanachangia.Nakumbuka nilipomaliza kidato cha nne tu,wiki iloyofuata nikapata kazi ya ukarani kwenye kampuni ya tumbaku/Dimon.Na hata nilipohitimu kidato cha sita baada ya mwezi nikaajiriwa wilaya fulani Nyanda za juu kusini.Na bado nikawa siitaki wilaya hiyo kwa visingizio vya kitoto.Je,leo kuna mtu atafanya hivyo?
usawa huu nani afanye hivoo, watu tuna boksa mbili miezi nenda rudi kwa sababu ya msoto
 
Back
Top Bottom