Hofu hii inasababishwa na nini na kwanini haikuwapo wakati wa kupigania uhuru?

Asante mkuu kwa ufafanuzi muruwa, swali bado limesimama palepale inabidi jamii ipate elimu kuhusu majina, je ni majina ya kidini au ya jamii za eneo fulani?
 
Wewe una ushahidi upi kwamba Mkwawa alikuwa na dini kabla hajawa muislamu?

..kwangu mimi mambo ya kiasili ya wahehe, ikiwemo matambiko, ni imani / dini. Ndio maana nasema Mkwawa alikuwa na dini yake ya asili kabla hajasilimu.
 
Inaonekana purpose ya maisha yako ni kutaka kuaminisha uma kwamba TANU ni chama cha waislamu. Na wapigania uhuru wote walikuwa ni waislamu. Lakini yanakufaidisha nini haya?

Tukiwatambua tu kama Watanzania bila kuangalia dini zao kuna shida?
Soma asili ya Tanu iliasisiwa na waislamu kwanza kama movement kilipokuwa ndo wakaanza ingiza wasomi wengine mfano Mwalimu Nyerere, waislamu wa pwani ndio walioleta UHURU wa nchi hii wao waliamua kumpa Mwalimu Nyerere ikiwa na maana ni msomi Ili aweze kuwaongoza wakiwa na lengo la kumdhibiti Mwalimu ambapo ikawa kinyume chake maana Mwalimu akaamua kuviunganisha vyama vyote maana vilikuwa na lengo moja la kudai UHURU ndipo ikazaliwa Tanu.
 
Vito...
Wapo Mkwawa ambao si Waislam hili linafahamika lakini uchifu umebakia kwa ukoo wa Mtwa Abdallah Mkwawa.

Ingia Google utaisoma historia hiyo tena kutoka vyanzo vya kuaminika.

Fika Kalenga Mkwawa Museum utajifunza mengi.
Hivi mzee Adam Sapi Mkwawa alikuwa ni Muislamu au Mkristo.
Kama alikuwa Muislamu nini ajabu kwa baba yake kuwa Muislamu.
 
Mini...
Kuwa Mtwa Mkwawa alikuwa Muislam utaelezwa hapo Mkwawa Museum na utafahamishwa pia ilikuwaje na utapewa jina la aliyemsilimisha.

Aliyemsilimisha ni Abushiri bin Salim Al Harith.
 
Invisible...
Umeghadhibika.

Lugha yako imekuwa kama pana ugomvi baina yetu ilhali ni mjadala.

Huwa mtu akifika hali hii mimi humwepuka.
 
Hivi mzee Adam Sapi Mkwawa alikuwa ni Muislamu au Mkristo.
Kama alikuwa Muislamu nini ajabu kwa baba yake kuwa Muislamu.
Kalunya,
Mkwawa Museum kuna picha ya kaburi la Mkwawa sehemu iitwayo Mlambalasi alikozikiwa.

Picha ya kaburi lake ukiangalia ni kaburi la Kiislam.

Makaburi mwanae Mkwawa Sapi na kaburi la mkewe Sapi Bi. Johari yapo Kalenga ndani ya Mkwawa Museum yote ni makaburi ya Kiislam.

Angalia picha hapo chini:

Kulia ni kaburi la Mkwawa na chini ni picha ya kaburi la mkewe Sapi Mkwawa Bi. Johari.

 
Mawazo mazuri, ubishi usokuwa na jibu kiutafiti unasumbua sana.
 
Jenga hoja zako kitaalamu siyo blaa blaa tu.

Lete ushahidi kama alivyoleta yeye kuwa Mkwawa alikuwa hana dini au ni wa dini nyingine yo yote ile.
 
Umeshawahi kuona au kusikia kuhusu msikiti aliokuwa anaswali mkwawa?
Ni upi au ulikua wapi?
 
Case closed
 
Hivi kwani Kuna tija gani ku "islamize" harakati za uhuru?
Kama mwanamuziki tajiri bongo ni Nasibu Abdul, Diamond, siku ikiandikwa historia, kwanini isitoshe kuandika tu jina lake, kwanini, iongezwe, alikuwa muislam? kwani huo uislam utakuwa umechangia nini kwenye muziki wake?
Huo uislam wa Mkwawa, uoisaidia vipi harakati za kudai uhuru?
Mandela alikuwa mkristo,lakini kwenye historia hatuandiki mpigania haki na baba wa Taifa, SA Mandela aliyekuwa mkristo pia!! huo ukristo, had nothing to do with fight against apartheid.
Hebu weka mchango wa uislam kama dini, au taasisi kwenye kudai uhuru.
Siku ikiandikwa historia ya huduma za jamii bongo,afya na Elimu, ukristo umechangia sana, sio kwa kuwa na waalimu wenye majina ya kikristo! la hasha kwa kujenga miundo mbinu, shule, hospitari, nk,
Je uislam ndio ulitengeneza mikuki, bunduki wakati wa vita ya majimaji?
 
Kwahili Mzee wangu hapa umepotoka, mimi kijijini kwetu kwa wazee wangu kuna makaburi kama haya na hawaujui uislamu hata chembe.

Makaburi mengi ni ya hivi makaburi yenye misalaba ni ya miaka baada ya uhuru watu walipoanza kupokea dini ya wamisionari.

Kama haya makaburi ndio ushahidi wa Mkwawa alikuwa dini gani basi nenda Musoma utasema wote ni waislamu utayakuta makaburi kama haya na ukifanya utafiti utagunduwa hata baba yake Nyerere au babu yake kaburi lake ni kama hilo la Mkwawa.
 
..kwangu mimi mambo ya kiasili ya wahehe, ikiwemo matambiko, ni imani / dini. Ndio maana nasema Mkwawa alikuwa na dini yake ya asili kabla hajasilimu.
Hawa watu wa dini za Abraham Waislamu na Wakristo hawaamini kama kuna dini nje ya hizo, nje ya Abraham religion wanakuita mpagani, sasa hakuna kusilimu kwa mpagani.
 
Umeshawahi kuona au kusikia kuhusu msikiti aliokuwa anaswali mkwawa?
Ni upi au ulikua wapi?
Daudi...
Nimefika Kalenga njiani nikaonyeshwa kichuguu ambacho Mtwa Mkwawa alikuwa akisimama kuhutubia watu wake.

Miaka ile kilikuwa kirefu hivi sasa kimeliwa na mvua nk. ni kifupi.

Hapo Museum nikaelezwa kuwa ndipo ilipokuwa nyumba yake lakini haikuweza kuhifadhiwa kwa kuwa ujenzi wa nyumba ile ulikuwa nyasi udongo na miti.

Nje uwanjani nyumbani palipokuwa kwa Mkwawa nilionyeshwa mabaki ya ngome iliyokuwa inapita ukuta wa urefu mita 12 na upana mita tatu.

Ngome hii ndiyo inayotenganisha Kalenga na Tosamaganga.

Wajerumani walishambulia ngome hii kutokea hapo.

Leo hiyo sehemu limejengwa kanisa kubwa.

Huu ukuta ulipigwa mabomu na kubomolewa kabisa na Wajerumani katika mapambano ya mwisho na Mkwawa.

Katika hali kama hii nyumba zote zilitekeketea.

Kama kulikuwapo na msikiti usingeweza kubakia.

Lakini hapo Kalenga nimesikia adhana kujulisha kuwa kuna msikiti.

Picha ya kwanza hapo chini ni kichuguu ambacho Mtwa Mkwawa akitoa hutuba zake.

Picha ya pili ni mabaki ya ukuta wa mita 12 urefu na mita tatu upana.

 
Mzee wangu hapa umetowa tu maelezo ya safari yako ya Kalenga lakini haujajibu swali.

Sasa hivi ukienda Butiama ambako ni ardhi ya Zanaki kuna msikiti mkubwa tu na adhana utaisikia.

Ziko taasisi za kutoka nje za kiislamu zimejitolea ujenzi wa misikiti sehemu yoyote ili mradi uwaoneshe kiwanja tu.
 
Matola,
Umeniuliza kama nimeona msikiti aliokuwa anasali Mkwawa na jibu langu ndilo hilo kuwa hapo Kalenga hakuna chochote kilichobaki si nyumba ya Mkwawa wala ngome yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…