Hofu ya Mwenyezi Mungu iliyo ndani ya Rais Samia imemfanya kuwa mkweli na muwazi katika Uendeshaji wa Serikali

Hofu ya Mwenyezi Mungu iliyo ndani ya Rais Samia imemfanya kuwa mkweli na muwazi katika Uendeshaji wa Serikali

Huwezi kuamini Mungu kweli kweli halafu ukaongoza nchi.

Kuongoza nchi ni statement kwamba humuamini Mungu kwamba ataiongoza nchi vizuri, hivyo unataka kuongoza wewe.
 
Utakuja kuchoka mwenyewe

Na uchawa wako

Ova
 
Nape, Makamba na wote wanaofanana na hao utawaita wastaarabu?

Ni wahuni watupu
Uhuni wao upo wapi? Acha kutaja taja majina ya watu kwa chuki zako binafsi au mkumbo tu wakuwachukia watu pasipo kuwa na sababu za msingi,Usirithishwe adui Wala mbaya wa kumchukia
 
Utakuja kuchoka mwenyewe

Na uchawa wako

Ova
Kwani Nimekwambia naandika hapa kutumia nguvu Kama kubeba kokoto Hadi useme nitakuja kuchoka? Napenda kukwambia kuwa IPO siku utasimama hadharani kuipongeza serikali ya mama Samia baada ya kutambua kuwa watanzania wote wapo upande wa mh Rais wetu mpendwa mama Samia
 
Huwezi kuamini Mungu kweli kweli halafu ukaongoza nchi.

Kuongoza nchi ni statement kwamba humuamini Mungu kwamba ataiongoza nchi vizuri, hivyo unataka kuongoza wewe.
Kasome upya vitabu vya Dini,Kama huamini uwepo wa Mwenyezi MUNGU Basi Ni ngumu Sana kubishana na wewe maana unavinasaba vya uwakala wa shetani,Mimi moyo wangu na Imani yangu Ni juu ya uwepo wa Mwenyezi MUNGU na siku zote humtumainia na kumtegemea Mwenyezi MUNGU. Hata mh Rais wetu Ameonyesha kwa matendo na maneno kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu,ndio sababu unaona akihubiri Haki katika Taifa letu iliyopelekea kutamalaki kwa utulivu na Amani nchini
 
Lucas mwashambwa Mimi siamini uwapo wa shetani kwa sababu zilezile zinazonifanya nisiamini uwepo wa Mungu.

Yani wewe unayeamini uwepo wa Mungu upo karibu zaidi na ushetani kuliko mimi.Kwa sababu kwanza unaamini shetani yupo. Mimi hata siamini shetani yupo.

Kwa hivyo siwezi kuwa wakala wa shetani, siamini kwamba shetani yupo, na shetani hayupo, sasa nitakuwaje wakala wa shetani ambaye hayupo?

Huyo Mungu unayemuamini unaruhusiwa kumuamini, lakini hayupo, na huwezi kuthibitisha yupo.

Rais anayesema kwamba yeye atashinda uchaguzi akipigiwa kura na watu au asipopigiwa kura na watu, kwa sababu ana uwezo wa kuiba kura, hawezi kuwa anaamini Mungu kihivyo

Rais anayewanyima watu haki yao ya kikatiba ya kufanya mikutano ya kisiasa, hawezi kuwa anamuamini Mungu kihivyo.

rajiih unaona yale mambo niliyokuwa nakwambia muda mchache tu uliopita huyu jamaa anayathibitisha hapa?
 
Ndugu zangu,

Rais Samia Ni kiongozi wa kipekee Sana, Ni kiongozi mkweli na muwazi Sana. Ni kiongozi mcha Mungu na mwenye hofu ya Mwenyezi MUNGU. Ni kiongozi ambaye Dhamira yake na kifua chake kimetawaliwa na hofu ya Mwenyezi Mungu. Ni kiongozi ambaye ukimsikiliza unaona Hataki kuzungumza maneno ili kumfurahisha mtu au watu. Hapendi kudanganya Wala kuwadanganya watanzania. Anasema ukweli na Ni msema kweli muda wote.

Anaeleza kila kinachokuwa kinaendelea serikalini kwake. Anahitaji kuona watanzania Tunajuwa na kufahamu kila kitu kinachotokea na Kuendelea katika serikali yetu. Anasema na kuzungumza kilicho katika kifua chake na kilicho Cha kweli. Roho yake na maneno yake huambatana kwa pamoja na kwa kuwa Ni mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu na mcha Mungu unaona maneno yake na kauli zake zikiwa zenye uhalisia. Hii ndio sababu ya kuona akiungwa mkono na mamillion ya watanzania kwa kuwa serikali yake Inaendeshwa kwenye mwanga na siyo gizani. Ndio sababu anatetewa na wengi kwa kuwa wengi wanakuwa wanaufahamu ukweli wa mambo unaotokana na kuambiwa na kuelezwa ukweli.

Kila hatua au mchakato au maamuzi au juhudi zozote zinazokuwa zinafanywa na serikali yake lazima awaeleze watanzania, iwe Ni miradi, mikopo,Tozo, Kodi, Hali ya uchumi au vyovyote vile unaona akitoka hadharani na kuwaeleza watanzania. Ni viongozi wachache Sana Barani Afrika na hata Duniani kwote wenye uwezo wa kuendesha serikali kwa uwazi na ukweli Kama afanyavyo Rais Samia na serikali Yake.

Anafanya hivyo kwa kuwa kila afanyacho ni kwa dhamira njema kwa nchi yetu. Ni kwa kuwa Rais Samia ni mzalendo wa kweli. Ni kwa kuwa ana mapenzi ya dhati na upendo wa kweli na Taifa hili, anafanya hivyo kwa kuwa Amedhamilia kuwatumikia watanzania kwa kuiweka serikali mikononi mwa watanzania ambao ndio walio ichagua. Ndio maana anawambia ukweli pasipo kuwadanganya au kuwarubuni. Anausema ukweli hata Kama Ni mchungu.

Rais Samia Ni Mfano Wa kuigwa Barani Afrika. Ni Nyota Ya Matumaini kwa waliokata Tamaa. Ni nuru iwakayo gizani. Ni Taa imulikayo mioyo iliyokata Tamaa na kuona Giza mbele. Ni mfariji wa Taifa Kama mkuu wa nchi na kiongozi wa serikali yetu. Ni Tumaini na Faraja ya wanyonge wasio na sauti. Ni nguvu kwa wanyonge Na Askari mpambanaji asiye choka Wala kukata Tamaaa katika vita ya kulipigania na kuliletea Maendeleo Taifa letu. Rais Samia Anastahili pongezi, kutiwa moyo, Faraja, kuungwa mkono, kusaidiwa vyema na wasaidizi wake, kuombewa na watanzania afya njema na nguvu za kututumikia watanzania pamoja na macho ya Rohoni ya kuona na kung'amua yasiyo weza kuonekana kwa macho ya nyama.

Mwenyezi Mungu ambariki Rais Samia na kumlimda wakati wote. Amtetee na kumpigania katika Hatua zote apigazo na kusonga mbele katika kuzielekea ndoto za kuona Taifa hili linainuka kiuchumi na kumgusa kila mtanzania afanyaye kazi na juhudi za kujikwamua kiuchumi. Ampe maarifa Zaid na zaidi ya kuongoza Taifa letu, amzidishie hekima na busara katika kufanya maamuzi juu ya Taifa letu. Ampe watu wema na waungwana na wenye Dhamira ya Dhati na kweli na ya kizalendo katika kulitumikia Taifa letu pindi wamshauripo na kutoa mawazo yao, Amuondolee watu wabaya karibu yake ili wakae mbali Naye. Ampe ujasiri wa kufanya maamuzi magumu pale inapohitajika kwa maslahi ya Taifa letu. Ampe na kumzidishia moyo wa ujasiri katika kufanya maamuzi kwa manufaa ya Taifa letu, Mwenyezi MUNGU asiondoe mkono wake mahali alipo Rais wetu, popote awapo Rais wetu Basi uwepo wa Mwenyezi MUNGU Ukawepo mahali Hapo na kusimama Naye.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627
mama ni dereva mwema
 
Kwa kweli hapa alikuwa mkweli na muwazi sana🐒🐒🐒
 
Lucas mwashambwa Mimi siamini uwapo wa shetani kwa sababu zilezile zinazonifanya nisiamini uwepo wa Mungu.

Yani wewe unayeamini uwepo wa Mungu upo karibu zaidi na ushetani kuliko mimi.Kwa sababu kwanza unaamini shetani yupo. Mimi hata siamini shetani yupo.

Kwa hivyo siwezi kuwa wakala wa shetani, siamini kwamba shetani yupo, na shetani hayupo, sasa nitakuwaje wakala wa shetani ambaye hayupo?

Huyo Mungu unayemuamini unaruhusiwa kumuamini, lakini hayupo, na huwezi kuthibitisha yupo.

Rais anayesema kwamba yeye atashinda uchaguzi akipigiwa kura na watu au asipopigiwa kura na watu, kwa sababu ana uwezo wa kuiba kura, hawezi kuwa anaamini Mungu kihivyo

Rais anayewanyima watu haki yao ya kikatiba ya kufanya mikutano ya kisiasa, hawezi kuwa anamuamini Mungu kihivyo.

rajiih unaona yale mambo niliyokuwa nakwambia muda mchache tu uliopita huyu jamaa anayathibitisha hapa?
Pole Sana ndugu yangu kwa Imani hiyo,Ila naomba uamini kuanzia leo kuwa Mwenyezi MUNGU muumba wa mbingu na Dunia yupo hai,pia lazima ufahamu kuwa hata uzima na uwepo hai kwako mpaka leo hii Ni kwa Neema ya Mwenyezi MUNGU,jiulize wangapi ulio kuwa unaowafahamu au ndugu zako wa karibu au jirani wametangulia mbele za haki? Jiulize kwanini wewe upo hai Hadi leo? Tambua Ni kwa Neema tu ya Mwenyezi Mungu na makusudi take,Mrudie muumba wako kwa kumtumainia na kumtegemea kwa kila jambo
 
KAMA ni mkweli na mcha MUNGU kwanini Anawalipa Mishahara wabunge 19 wasio na sifa ya Ubunge kutokana na kutokuwa na Chama?

Kwanini anazuia Mikutano ya Vyama vingine ili hali chama chake kinafanya mikutano?
Kwanini Hataki KATIBA MPYA katiba ambayo Wenye Nchi ambao ni Wananchi Wanaitaka?
Kwanini Hataki TUME HURU ya Uchaguzi ili HAKI itendeke kama MUNGU atakavyo HAKI?
Akijibu kiutaalamu bila kuwa hopeless nipo nimekaa palee nabugia mihogo yangu mnistue.😂😂😂😂
 
Kwa kweli hapa alikuwa mkweli na muwazi sana🐒🐒🐒
View attachment 2455939
Hapo mh Rais wetu mpendwa alimaanisha kuwa viongozi wote watosheke na vipato vyao wavipatovya na vilivyopo kisheria,wasitamani na kufuja pesa za umma kwa Tamaa Binafsi, ,waridhike na mishahara yao,wasiwake Tamaa ya kujiongezea vipato kinyume na sheria
 
Pole Sana ndugu yangu kwa Imani hiyo,Ila naomba uamini kuanzia leo kuwa Mwenyezi MUNGU muumba wa mbingu na Dunia yupo hai,pia lazima ufahamu kuwa hata uzima na uwepo hai kwako mpaka leo hii Ni kwa Neema ya Mwenyezi MUNGU,jiulize wangapi ulio kuwa unaowafahamu au ndugu zako wa karibu au jirani wametangulia mbele za haki? Jiulize kwanini wewe upo hai Hadi leo? Tambua Ni kwa Neema tu ya Mwenyezi Mungu na makusudi take,Mrudie muumba wako kwa kumtumainia na kumtegemea kwa kila jambo
Nakwambia hivi, huyo Mungu unamuamini tu, na ni haki yako kumuamini. Siwezi kukupinga kwenye imani.

Lakini, kiuhalisia, kwa facts, hayupo.

Ndiyo maana huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Unaishia kusema habari za imani tu.

Imani unaweza kuamini chochote.Unaweza kuamini mavi yako ni Mungu.

Je, ukiamini mavi yako ni Mungu, hilo litafanya mavi yako yawe Mungu kweli?
 
Watanzania wengi sana bado wana ushamba wa kuchanganya dini na siasa, na viongozi wao washawajulia kwenye hilo wanawashikia akili.

Kiongozi hata kama si mtu wa dini, akiona anaingia kwenye siasa anajifanya mtu wa dini.

Samia mwenyewe alishasema alikuwa anavaa jeans na hakuvaa ushungi, baada ya kuingia kwenye siasa anajifunika ushungi aonekane ana maadili ya kidini.

Anawashikia akili mazuzu.
 
Nakwambia hivi, huyo Mungu unamuamini tu, na ni haki yako kumuamini. Siwezi kukupinga kwenye imani.

Lakini, kiuhalisia, kwa facts, hayupo.

Ndiyo maana huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Unaishia kusema habari za imani tu.

Imani unaweza kuamini chochote.Unaweza kuamini mavi yako ni Mungu.

Je, ukiamini mavi yako ni Mungu, hilo litafanya mavi yako yawe Mungu kweli?
Nini kinakufanya usiamini uwepo wa Mwenyezi Mungu?
 
Nini kinakufanya usiamini uwepo wa Mwenyezi Mungu?
Habari zinazoelezea uwepo wa Mungu hazina logical consistency na zina contradiction.

Unaelewa maana ya kitu kukosa logical consistency na kuwa na contradiction ni nini?

Wewe nini kinakufanya uamini uwepo wa Mwenyezi Mungu?
 
Mwenye hofu ya Mungu angeweza kuona na kuacha raia wakiteseka huku tozo kule maji huku umeme hapa machinga! Pumbavu kabisa Kiongozi wa hovyo asiye na hofu ya Mungu ndiye anayeweza kutesa wananchi wake kiasi hicho
 
Back
Top Bottom