Hofu ya Mwenyezi Mungu iliyo ndani ya Rais Samia imemfanya kuwa mkweli na muwazi katika Uendeshaji wa Serikali

Huwezi kuamini Mungu kweli kweli halafu ukaongoza nchi.

Kuongoza nchi ni statement kwamba humuamini Mungu kwamba ataiongoza nchi vizuri, hivyo unataka kuongoza wewe.
 
Utakuja kuchoka mwenyewe

Na uchawa wako

Ova
 
Nape, Makamba na wote wanaofanana na hao utawaita wastaarabu?

Ni wahuni watupu
Uhuni wao upo wapi? Acha kutaja taja majina ya watu kwa chuki zako binafsi au mkumbo tu wakuwachukia watu pasipo kuwa na sababu za msingi,Usirithishwe adui Wala mbaya wa kumchukia
 
Utakuja kuchoka mwenyewe

Na uchawa wako

Ova
Kwani Nimekwambia naandika hapa kutumia nguvu Kama kubeba kokoto Hadi useme nitakuja kuchoka? Napenda kukwambia kuwa IPO siku utasimama hadharani kuipongeza serikali ya mama Samia baada ya kutambua kuwa watanzania wote wapo upande wa mh Rais wetu mpendwa mama Samia
 
Huwezi kuamini Mungu kweli kweli halafu ukaongoza nchi.

Kuongoza nchi ni statement kwamba humuamini Mungu kwamba ataiongoza nchi vizuri, hivyo unataka kuongoza wewe.
Kasome upya vitabu vya Dini,Kama huamini uwepo wa Mwenyezi MUNGU Basi Ni ngumu Sana kubishana na wewe maana unavinasaba vya uwakala wa shetani,Mimi moyo wangu na Imani yangu Ni juu ya uwepo wa Mwenyezi MUNGU na siku zote humtumainia na kumtegemea Mwenyezi MUNGU. Hata mh Rais wetu Ameonyesha kwa matendo na maneno kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu,ndio sababu unaona akihubiri Haki katika Taifa letu iliyopelekea kutamalaki kwa utulivu na Amani nchini
 
Lucas mwashambwa Mimi siamini uwapo wa shetani kwa sababu zilezile zinazonifanya nisiamini uwepo wa Mungu.

Yani wewe unayeamini uwepo wa Mungu upo karibu zaidi na ushetani kuliko mimi.Kwa sababu kwanza unaamini shetani yupo. Mimi hata siamini shetani yupo.

Kwa hivyo siwezi kuwa wakala wa shetani, siamini kwamba shetani yupo, na shetani hayupo, sasa nitakuwaje wakala wa shetani ambaye hayupo?

Huyo Mungu unayemuamini unaruhusiwa kumuamini, lakini hayupo, na huwezi kuthibitisha yupo.

Rais anayesema kwamba yeye atashinda uchaguzi akipigiwa kura na watu au asipopigiwa kura na watu, kwa sababu ana uwezo wa kuiba kura, hawezi kuwa anaamini Mungu kihivyo

Rais anayewanyima watu haki yao ya kikatiba ya kufanya mikutano ya kisiasa, hawezi kuwa anamuamini Mungu kihivyo.

rajiih unaona yale mambo niliyokuwa nakwambia muda mchache tu uliopita huyu jamaa anayathibitisha hapa?
 
mama ni dereva mwema
 
Kwa kweli hapa alikuwa mkweli na muwazi sanaπŸ’πŸ’πŸ’
Your browser is not able to display this video.
 
Pole Sana ndugu yangu kwa Imani hiyo,Ila naomba uamini kuanzia leo kuwa Mwenyezi MUNGU muumba wa mbingu na Dunia yupo hai,pia lazima ufahamu kuwa hata uzima na uwepo hai kwako mpaka leo hii Ni kwa Neema ya Mwenyezi MUNGU,jiulize wangapi ulio kuwa unaowafahamu au ndugu zako wa karibu au jirani wametangulia mbele za haki? Jiulize kwanini wewe upo hai Hadi leo? Tambua Ni kwa Neema tu ya Mwenyezi Mungu na makusudi take,Mrudie muumba wako kwa kumtumainia na kumtegemea kwa kila jambo
 
Akijibu kiutaalamu bila kuwa hopeless nipo nimekaa palee nabugia mihogo yangu mnistue.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kwa kweli hapa alikuwa mkweli na muwazi sanaπŸ’πŸ’πŸ’
View attachment 2455939
Hapo mh Rais wetu mpendwa alimaanisha kuwa viongozi wote watosheke na vipato vyao wavipatovya na vilivyopo kisheria,wasitamani na kufuja pesa za umma kwa Tamaa Binafsi, ,waridhike na mishahara yao,wasiwake Tamaa ya kujiongezea vipato kinyume na sheria
 
Nakwambia hivi, huyo Mungu unamuamini tu, na ni haki yako kumuamini. Siwezi kukupinga kwenye imani.

Lakini, kiuhalisia, kwa facts, hayupo.

Ndiyo maana huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Unaishia kusema habari za imani tu.

Imani unaweza kuamini chochote.Unaweza kuamini mavi yako ni Mungu.

Je, ukiamini mavi yako ni Mungu, hilo litafanya mavi yako yawe Mungu kweli?
 
Watanzania wengi sana bado wana ushamba wa kuchanganya dini na siasa, na viongozi wao washawajulia kwenye hilo wanawashikia akili.

Kiongozi hata kama si mtu wa dini, akiona anaingia kwenye siasa anajifanya mtu wa dini.

Samia mwenyewe alishasema alikuwa anavaa jeans na hakuvaa ushungi, baada ya kuingia kwenye siasa anajifunika ushungi aonekane ana maadili ya kidini.

Anawashikia akili mazuzu.
 
Nini kinakufanya usiamini uwepo wa Mwenyezi Mungu?
 
Nini kinakufanya usiamini uwepo wa Mwenyezi Mungu?
Habari zinazoelezea uwepo wa Mungu hazina logical consistency na zina contradiction.

Unaelewa maana ya kitu kukosa logical consistency na kuwa na contradiction ni nini?

Wewe nini kinakufanya uamini uwepo wa Mwenyezi Mungu?
 
Mwenye hofu ya Mungu angeweza kuona na kuacha raia wakiteseka huku tozo kule maji huku umeme hapa machinga! Pumbavu kabisa Kiongozi wa hovyo asiye na hofu ya Mungu ndiye anayeweza kutesa wananchi wake kiasi hicho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…