Hofu ya Mwenyezi Mungu iliyo ndani ya Rais Samia imemfanya kuwa mkweli na muwazi katika Uendeshaji wa Serikali

Huwezi ukamuongoza Mwenyezi MUNGU katika Jambo lolote lile la kiuanadamu kimafanikio,Ukiongoza bila hofu ya Mwenyezi Mungu utakuwa ni Kama kipofu gizani
 
Nonsense. Tafuta kazi ya kufanya, huu uchawa haukusaidii.
 
Wapi nimesema kuwa Rais hakumaanisha kuwa viongozi wasitosheke na vipato vyao?!

Unajishtukia kupinga mambo ambayo sijasema kwa kuwa unahaha na unahaha kwa sababu unajua ya kwamba unatetea uovu.
 
Huwezi ukamuongoza Mwenyezi MUNGU katika Jambo lolote lile la kiuanadamu kimafanikio,Ukiongoza bila hofu ya Mwenyezi Mungu utakuwa ni Kama kipofu gizani
Nakubaliana nawe siwezi kumuongoza Mungu.

Kwa sababu hayupo.

Nitamuongozaje Mungu kama hayupo?

Kama unabisha na kusema Mungu yupo, thibitisha Mungu yupo.
 
Unapaswa uitwe LUCAS MWASHAMBWA CHAWA MKUU huoni Kila mtu anakupinga?
 
Mwenye hofu ya Mungu angeweza kuona na kuacha raia wakiteseka huku tozo kule maji huku umeme hapa machinga! Pumbavu kabisa Kiongozi wa hovyo asiye na hofu ya Mungu ndiye anayeweza kutesa wananchi wake kiasi hicho
Nchi gani iliyoendelea pasipo wananchi wake kushiriki katika ujenzi wa Taifa lao kupitia mikono yao Kama vile kulipa Kodi na Tozo? Ni wapi na Taifa lipi limepiga hatua pasipo wananchi wake kuchangia kutoka katika vipato vyao? Unataka Nani atujengee Taifa letu? Masuala ya maji na umeme kwa Sasa siyo changamoto kwa kuwa Hali Ni njema sana Sasa,Hali aliyokuwa imejitokeza ilikuwa Ni mpito uliotokana na Hali ya ukame uliokuwa umeikumba nchi yetu
 
Unapaswa uitwe LUCAS MWASHAMBWA CHAWA MKUU huoni Kila mtu anakupinga?
Kasome habari za Galileo uone namna alivyo pingwa na watu wengi pale alipokuwa anasimamia ukweli ,lakini mwisho wa siku waliokuwa wanampinga walikuja kugundua kuwa alikuwa sahihi,Hivyo naamini IPO siku mtakuja mkubali na kuniunga mkono katika haya niandikayo. Ukweli unabaki kuwa ukweli tu bila kuangalia wangapi wanaupinga au kuunga mkono
 
Mwenyezi MUNGU ndiye hutoa maarifa na njia kwa mwanadamu,Usipotambua uwepo wake na kuzingatia maandiko yake utajikuta unaongoza Kama kipofu au Gari lisilo Na Taa usiku,Lazima utakwenda korongoni Tu
Lkn viongoz wetu tofaut kbs hofu ya MUNGU hakunaga!! Na huo ndio ukweriii
 
Lkn viongoz wetu tofaut kbs hofu ya MUNGU hakunaga!! Na huo ndio ukweriii
Kwa mama Samia sote tunamuona na kumsikia kimaneno na kimatendo namna alivyo Tawaliwa na hofu ya Mwenyezi Mungu Moyoni mwake,unaona namna anavyohubiri na kuitenda haki katika majukumu take,Unaona namna anavyopinga uonezi kwa wananchi wake,unaona namna anavyohubiri utendekaji wa Haki kwa wasaidizi wake wafanyapo maamuzi
 
Watu wazuri hawafi, ndiyo maana Kikwete na Kinana hawajafa. Kumbuka Rais Samia ndiye kiongozi wa hili genge lililomuua Dkt Magufuli, Mkapa na Nyerere (hawa watu wabaya). Hiyo hofu inatoka wapi?? Au ndiyo kuogopa karma???
 
Watu wazuri hawafi, ndiyo maana Kikwete na Kinana hawajafa. Kumbuka Rais Samia ndiye kiongozi wa hili genge lililomuua Dkt Magufuli, Mkapa na Nyerere (hawa watu wabaya). Hiyo hofu inatoka wapi?? Au ndiyo kuogopa karma???
Acha kuongea mambo pasipo kuwa na ushahidi ,acha kuongea na kuandika maneno kwa kuwapaka matope watu,acha Kuandika mambo kwa hisia pasipo kuwa na uthibitisho wa aina yoyote Ile
 
Mwanasiasa ni mwanasiasa mzee usidanganyike na maneno wala vitendo! Mwanasiasa kamwe hawez kua mcha MUNGU!!
 

Attachments

  • 1671513296448.jpg
    34.9 KB · Views: 1
Kusudi la mapanbio haya ni Nini..... , Kiongozi kutekeleza majukumu yake kama inavyotakiwa kisheria Kuna shida Gani mpaka kuwe kumtukuza Ivyo,
Kijana pambana na hali yako. Dunia
haiwezi kutambua thamani Yako kama wewe...haujaitambua wewe mwenyewe....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu,

Rais Samia Ni kiongozi wa kipekee Sana, Ni kiongozi mkweli na muwazi Sana. Ni kiongozi mcha Mungu na mwenye hofu ya Mwenyezi MUNGU.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627
Naunga mkono hoja, Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania 2025. Hivyo kwanza tumemshauri Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! kisha Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
P
 
Kwani watu wangapi wanapewa kila aina ya stahiki na malipo lakini wanashindwa kutimiza wajibu wao? Kama watu na viongozi wote wangekuwa wanatekeleza majukumu na wajibu wao unafikiri kungekuwa na mabango katika ziara za viongozi wetu wakuu? Unafikiri mbio za mwenge zingeibua ufisadi? Unafikiri kungekuwa na kero ndogo ndogo? Huoni hayo yanatokea kwa kuwa Kuna viongozi wanaolipwa mishahara lakini hawatimiza wajibu wao? Sasa kwanini Tusimpongeze mh Rais wetu kwa kutimiza vyema wajibu wake? Kwanini tusimtie moyo na kumpa faraja? Kwani Tusimuunge mkono kwa kutimiza wajibu wake vyema?
 
Una hoja za kitoto sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…