Hofu ya Mwenyezi Mungu iliyo ndani ya Rais Samia imemfanya kuwa mkweli na muwazi katika Uendeshaji wa Serikali

Tunachohitaji Ni maendeleo tuu sifa zitakuja baadaye,sisi wenyewe Ni watu wazima tunaelewa
 
Ndivyo alivyokwambia au unajifanye msemaji wake? Nadhani anatimiza wajibu wake kama kiongozi na mwananchi. Kwa waongo kusema uongo ndiko kunahitaji hayo unayosema. Acheni mama afanye kazi badala ya kutafuta kumtukuza hata asipopaswa.
 
Hiki ulichoandika hakina mashiko sana ,kwa kuwa haongozi taasisi ya dini
Anaongoza serikali kwa haki katika kuwaletea maendeleo watanzania huku matendo na maneno yake yakiwa yenye upendo unyenyekevu uzalendo na uvumilivu kutokana na kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu ndani yake
 
Kwani wewe akili yako haiwezi kutambua Hilo mpaka uambiwe?
Sina akili ya wala muda wa kujikombakomba. Mara kiongozi wa pekee. Hujui kuwa kila mtu ni wa kipekee? Nyie ndiiyo mnaowafisidi viongozi wetu. Mnawaabudia hadi wanawaona kama wanyama na kuwa mafisadi na wakatili halafu mnaanza kulalama.
 
Tunachohitaji Ni maendeleo tuu sifa zitakuja baadaye,sisi wenyewe Ni watu wazima tunaelewa
Kazi ya kuleta na kuchochea maendeleo ameipiga na kuifanya katika kila secta,kuanzia Elimu , Afya ,kilimo, N.k unakuta Ni mafanikio tu na uwekezaji mkubwa wa fedha ili zimguse na kumnufaisha mtanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…