Hofu yenu kwa Umoja Party ni jibu tosha

Hofu yenu kwa Umoja Party ni jibu tosha

Tatizo lenu ni CHADEMA sio CCM mnarudia kosa la ACT 2015, mwisho wakambulia Kura za urais 90,000 nchi nzima na nafasi moja ya ubunge. Siku mtakapoanza kupimwa na dola ndio mtajua kwanini chadema ni chama Kikuu Cha Upinzani nchini.
Ukoja party CCM- D
 
Lakini wewe ni mwanaccm pia mbona unawatukana wenzako? wamekufanya nini?
Ccm wamenikoroga vibaya mno kumsema vibaya MTU ambaye kwa mapenzi ya chama chao walituletea wao wenyewe, halafu wanamtukana na wakati pia alijizolea umarufu na kupendwa na wengi mno na ccm wanalijua hili.
Wanajidai kusahaulishwa na majambazi machache ndani ya chama yaliyokuwa yamebanwa mbavu na kiongozi asiyependa ujingaujinga
 
Unashangilia hewa! Huijui vyema ccm Yako uliyokuwa unaiabudu kuliko Muumba wako! Mtapigwa na kitu kizito ku kichwa hamtaamini!
Usiishi kwa kukariri, hakuna anayeweza kuizidi nguvu ya umma.
 
Mkuu, hivi mnakumbuka chadema mliwahi kutuuzia mbuzi kwa gunia!?
Mnalituhadaa Lowasa fisadi mkamvuta tena kupitia mlango wa nyuma, kitendo hiko ndicho kiliniondoa chadema, na ukipima tu, nguvu ya chadema ilianza kupoa tokea hapo

Chadema ingepoa nguvu uchaguzi wa 2020 usingevurugwa na kuwekewa vikwazo vingi. Halafu huyo Lowasa unayemsema yupo wapi Sasa?. Mbona mtoto wake alipewa ubunge Tena Chini ya Magufuli. Yani anamkubali Lowassa wa CCM na kumkataa lowasaa wa CHADEMA kweli Kuna shida.
 
Nilikuwa nimekosa chama baada ya JPM R.I.P kukataliwa na kusemwa vibaya na chama chake na chadema!

Sasa Mimi rasimi Umoja Party

Wapuuzi tu wanaoubeza upepo wa Hayati JPM

Tayari ccm wanajinyea, chadema ndo kabisaa
Bora umehamia rasmi umoja party (Sgang party)🤸
 
Kwamba kumbe hayati JPM alikuwa anakubalika na wengi. The majority ya wananchi wanyonge ambao hata mumchafue vipi kwao yeye hachafuki maana wanajua kazi aliyoifanya kwa taifa lake.

Umoja party tayari imeshazichanga karata na inakwenda kuzoa lundo la wafuasi wapinga ufisadi na ubadhirifu na wananchi wa kawaida wenye uchungu na taifa lao.

Kwa nini mnaanza kutapatapa mapema namna hii?
Tunamgokea atakayekisajjili tumwone...ilikuja CCK ya Nape makaratasi yakachakalia kwemye Bahasa.

Sisi wenye akili hatutaki vyama tena; hitaji la leo ni KATIBA moya tu.
 
Kwamba kumbe hayati JPM alikuwa anakubalika na wengi. The majority ya wananchi wanyonge ambao hata mumchafue vipi kwao yeye hachafuki maana wanajua kazi aliyoifanya kwa taifa lake.

Umoja party tayari imeshazichanga karata na inakwenda kuzoa lundo la wafuasi wapinga ufisadi na ubadhirifu na wananchi wa kawaida wenye uchungu na taifa lao.

Kwa nini mnaanza kutapatapa mapema namna hii?
Acheni kukuza mambo, hivi hiyo nguvu si ingedhihirika bungeni au ndani ya CCM? Mbona Kinana alishinda kwa 100% kama kweli wanaopenda JPM wapo wengi CCM!!

Then ukifuata upepo wa JPM what's next? Kwamba 2025 ndio JPM anakua mgombea Urais ama inakuaje? CCM imejaa wanafiki hakuna atakayehama eti akaanzishe chama kuipinga CCM ya Samia!!! Watalalamika ila ikifia 2025 sio kabudi sio Mpina watakua front seat kumpigia kampeni Samia.

2015-20 ni Nyalandu tu ndio alikua na ujasiri wa kuhama wengine wote walibaki ndani hata kama hawakumkubali JPM. so punguzeni mihemko hakuna mzalendo CCM huko mwenye huo ujasiri wote ni wezi tu na wanajua siku wakihama madudu yote yanaanikwa
 
Kweli wameshindwa kuja na strategy mpya...eti wanataka kupitia nyota ya Magufuli??? Mwacheni baba wa watu apumzike kwa amani, kusema Magufuli na Wanyonge ni kapu moja..what a mistake??, huyo aliewaza kujenga kwao CHATO na kutopandisha mishahara/madaraja kwa 'wanyonge' leo ndio mnataka kutupa presha...tunawaangalia tuuu....tunasema hihiiiiiiiiiiiiiii (In Magufuli's voice).
 
Kama kinakuja na upepo wa nguvu ya mtu na sio nguvu ya itikadi, basi kimeshindwa kabla ya kuanza......tena kimeshindwa kijinga kweli kweli!!
 
Wapuuzi tu wanaoubeza upepo wa Hayati JPM
Hata DRC kuna chama kilisimama na Lumumba in fact mgombea Urais alikua kijana wa Lumumba but walianguka mbali sana.

Mtu akishakufa ameenda zake huwezi ukatembelea kivuli chake kwamba na wwe utaweza fanya alichofanya!! Eti atokee mtu aseme anaendeleza Unyerere wakati huna charisma au character zake utaweza wapi??

Hao wameona fursa tu ya kupata funding na kuingia bungeni kwa mgongo wa kufufua sera za JPM but on the real sense Hilo haliwezekani Kila mtu ana leadership character zake binafsi ambazo ni unique kwa mwingine.
 
Ccm wamenikoroga vibaya mno kumsema vibaya MTU ambaye kwa mapenzi ya chama chao walituletea wao wenyewe, halafu wanamtukana na wakati pia alijizolea umarufu na kupendwa na wengi mno na ccm wanalijua hili.
Wanajidai kusahaulishwa na majambazi machache ndani ya chama yaliyokuwa yamebanwa mbavu na kiongozi asiyependa ujingaujinga
Kuna uzi nilianzisha mwezi haujapita nikiwatahadharisha ccm ku handle issue ya Magufuli with care kwa ustawi wao ndo kwanzaaa mama anaupiga mwingi kwa kumbagaza.
 
Kama ungeliijua ccm na chadema usingelikuwa na hiyo mawazo
 
Ushauri [emoji205][emoji116]

Huyu kabwela mbona hazikwi Pemba na Maalim seif Sharrif? Acheni unyumbu.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom