Hofu yenu kwa Umoja Party ni jibu tosha

Punguza hofu, najua unaumia sababu unajaribu kumchafua hayati JPM lakini hawezi kuchafuka maana yupo ndani ya mioyo ya mama lishe, wakulima, na wamachinga.

Habari kuwa nani atakuwa ni mwenyekiti sio ishu.

Ishu ni namna watavyotembea na falsafa ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kupinga ufisadi.

Unamtaja Marehemu Filinkunjombe sabau alikuwa rafiki yako?

Mbona husemi wazi namna hayati JPM alivobana mafisadi na kufanya mambo makubwa kwa muda mfupi?
 
Wewe haupo serious kupigania maslahi ya wananchi. Ni kweli ulianza vizuri hasa ulipokuja na mkwara wa Azimio la Tabora ukiwahadaa wananchi upo kijamaa zaidi kumbe mbwembwe tu.
 
Mkuu, hivi mnakumbuka chadema mliwahi kutuuzia mbuzi kwa gunia!?
Mnalituhadaa Lowasa fisadi mkamvuta tena kupitia mlango wa nyuma, kitendo hiko ndicho kiliniondoa chadema, na ukipima tu, nguvu ya chadema ilianza kupoa tokea hapo
Sasa ni kwanini mwaka ule Chadema ndio kilipata kura nyingi na wabunge na madewani wengi zaidi ya chaguzi zilizopita?
 
 
Hiki chama kiweke kwenye katiba kuwa JPM aliuawa na wana CCM ambao hawakukubaliana na sera zake. The guy was silenced kwa maslahi ya kundi mojawapo ndani ya CCM
 
ukiwatazama vizuri ni kama wamechanganyikiwa sijui na huu ni mwezi ya mvua akifika kiangazi watakuwa wanaongea peke yao njiani
 
Al
Alikua na nguvu akakimbilia Ubalozi wa Ujerumani! Wenye nguvu ni kina Amolo walioilazimisha serikali ya Kenya ikafanya hand shake nao.

Kuna mtu ambaye hajui CDM na Lissu 2020 walisaidiwa na CCM anti Magufuli?!!
 
Upepo tu huo kijana. CCJ na CCK viliundwa na watu waliotoswa na JK. Akina Sitta, Nape na wengineo..

Hicho chama chenu kipya kinaundwa na waliotoswa na Samia, upepo utapita tu na wala usijiaminishe kwamba kitaweza kukichallenge hata TLP au NCCR. Njia pekee ya kukijenga hicho chama angalau kiwe hadhi ya NCCR au Chas hapo 2025 ni wale team Magufuli wote ambao wamewatuma hao vijana wawili kusajili Chama wataachia nafasi zao za Ubunge, Uwaziri, Ubalozi na zingine kwenye vyombo vya Dola na kujiunga mapema kukijenga hicho chama kuelekea 2025. Hapo mnaweza kubahatisha Mbunge Mmoja kutoka Usukumani na madiwani wanne​
 
Huwajui wananchi wa hii nchi wewe.. Huwajui Watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…