Hongera Masoud Kipanya ila tunaomba ufafanuzi kidogo kuhusu hii gari yako

Hongera Masoud Kipanya ila tunaomba ufafanuzi kidogo kuhusu hii gari yako

Hongera kwake, katika Gari kubwa ubunifu body ,matumizi nk,kwa kuzingatia STDs vifaa vingine ni assembly unanunua kwa wadau wengine.
 
Na kwa muundo huu hawez kupata wateja hii haiwezi kushindana na kirikuu
Unadhani kwa sasa anataka kushindana na kampuni kubwa kama Suzuki? Kwa sasa naamimi atatengeneza kwa oda. Mtu akiweka Oda anatengenezewa.

Ni suala la muda tu utagundua fikra zake ni tofauti sana na zako Labda bei iwe juu sana ashindwe kuuza kwa uhalisia.

Ila mpaka hapa alipofika anastahili pongezi.
 
Ngoja tuone...

Pengine bei yake ni nafuu sana kuzidi Kirikuu...
Yani ashindane na kirikuu ambayo Bei yake ni chini karibia 12m afu hiyo yake kasema imemgarimu zaidi ya 40 atashindanaje Sasa hapo.
 
Kibaha kipo kiwanda cha kuunda magari
Kwani ni Cha KP?. Nimepongeza juhudi za kijasiriamali za KP.

Apongezwe, atakapoishia mwingine amuunge mkono aendeleze safari za ndoto yake isife.

Kina Musk walikuwa na fikra kama hizi na hawajazikuza wenyewe, wapo watu walioendeleza pale walipokwama mpaka leo anakuwa mtu wa aina yake.
 
Yani ashindane na kirikuu ambayo Bei yake ni chini karibia 12m afu hiyo yake kasema imemgarimu zaidi ya 40 atashindanaje Sasa hapo..????

Nimetumia neno pengine, sababu sina details za kutosha...

Nimepata kumsikia kwenye kipindi cha PB cha Clouds siku chache kabla ya uzinduzi, hakuwa kaweka bayana vitu vingi...

Alichosisitiza tu kuwa hiyo ni prototype, mengine yatafuata...

Pia katika moja ya kauli zake, alisema hajafanya ubunifu huu ili kushindana na waliomtangulia sana, isipokuwa anaona kuna ambao anaweza kushindana nao kwenye soko (kama hizo toyo n.k)
 
Back
Top Bottom