Hongera Masoud Kipanya ila tunaomba ufafanuzi kidogo kuhusu hii gari yako

Hongera Masoud Kipanya ila tunaomba ufafanuzi kidogo kuhusu hii gari yako

nimeona mwananchi wameweka kuwa Gari la kwanza la umeme ndio limezinduliwa mbona huu uongo jamani? kwa nini msifamye tafiti kwanza jaman?

Kule Arusha watu wametengeneza Gari tena za Kwenda Mbugani ni full umeme tu!

acheni kukuza watu kwa kuwa tu wana majina makubwa! acheni kumtafutia mtu promo kiboya

angalieni hapa
 
Kama nilimsikia vizuri Kp alisema material za gari yake zinatoka kwenye kiwanda chake na kama gari ikiharibika spare zinapatikana.
Je, huyo wa Arusha material katengeneza yeye au alichofanya ni kubadili mfumo wa gari kutoka kwenye mafuta mpaka kwenye umeme?
Mleta mada umemuelewa vizuri?
 
Pongezi kwa kipanya na kampuni yake kwa uthubutu.

Kamwe asivunjike moyo kwa wivu wa kitz maana huwa hawapendi kuona mbongo anafanya mambo makubwa kama haya....either wataamkatisha tamaa kwa maneno ya ovyo....au kumpiga ushirikina.....hivyo tunamuombea sana Mungu amlinde lkn pia naye anapaswa sana kujiombea mara zote ili watanzania wapate manufaa kwa ubunifu wake huu
 
Usije kuta ametumia vifaa vya ujenzi,

vipuri msijali mtatumia vya piki piki, ist, stalet na bajaj
 
Nikupongeze kwa hatua hii ya kuzindua gari uliyoitengeneza wewe mwenyewe kama ulivyotuaminisha ila naomba basi utusaidie yafuatayo ili utuvutie zaidi kuweza kununua gari yako

1. Je, ukichaji gari ikajaa unaweza kutembea kwa umbali wa kilomita ngapi?
2. Je, vipuri vya gari vikiharibika vinapatikana?
3. TBS imethibitisha ubora wake?
4. Je kuna aina nyingine tofauti na iliyozinduliwa?
5. Speed ya gari ni ngapi maximum?
Swali namba 6 : ametumia gharama gani kulitengeneza?
 
nimeona mwananchi wameweka kuwa Gari la kwanza la umeme ndio limezinduliwa mbona huu uongo jamani? kwa nini msifamye tafiti kwanza jaman?

Kule Arusha watu wametengeneza Gari tena za Kwenda Mbugani ni full umeme tu!

acheni kukuza watu kwa kuwa tu wana majina makubwa! acheni kumtafutia mtu promo kiboya

angalieni hapa

Punguza jazba , watu wote tutawapa promo wajitangaze tu sisi tutawasapoti
 
Back
Top Bottom