Hongera Masoud Kipanya ila tunaomba ufafanuzi kidogo kuhusu hii gari yako

Hongera Masoud Kipanya ila tunaomba ufafanuzi kidogo kuhusu hii gari yako

Unadhani kwa sasa anataka kushindana na kampuni kubwa kama Suzuki? Kwa sasa naamimi atatengeneza kwa oda. Mtu akiweka Oda anatengenezewa. Ni suala la muda tu utagundua fikra zake ni tofauti sana na zako Labda bei iwe juu sana ashindwe kuuza kwa uhalisia. Ila mpaka hapa alipofika anastahili pongezi.
Bei iko chini ya 10M
 
Nitakujibu kwa kifupi:
1. Ukichaji kwa saa 6, utatumia units 600
2. Chaji hiyo unaweza kuitumia kwa km 100 au saa 1 na nusu
3. Kinaweza kupakia kg 200 au mifuko 4 ya smenti pamoja na dereva
4. Spear zake kwa sasa hakuna
5. Kinaweza kudumu kwa miaka 5
Unit 600 utahitaji umeme wa laki 2 na nusu...Ili uende km100.....ujinga mtupu
 
Magari ya mafuta yataendelea kuwa bora siku zote, embu fikiria una safari ya ghafla usubiri masaa 6 chaji, au linakuzimikia batabarani upeleke chaji usubirie, mafuta hata kwa dumu unafuata na maisha yanasonga
Tesla wana gari la zaidi ya 1000KM per charge, na huwezi safiri KM zote hizo bila kupumzika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ina make sense maana 1000km ni kama umbali wa Dar hadi Mwanza.
Ukifika Mwanza unachaji tena kwa ajili ya safari ya kurudi dar haina usumbufu ni zaidi ya mafuta full tank.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Nchi za wenzetu hautengenezi gari na kuingiza sokoni kienyeji.

Hizo test zote lazima.

Ndo maana karibu gari zote za wenzetu zinakuwa na safety ratings.

Hizo noah voxy ukitafuta safety ratings zake utazipata.
Nchi za wenzeti ni zipi..?
Nani kaingiza gari sokoni kienyeji?
 
1. Ukichaji kwa masaa sita linakuwa kimekula units ngapi za umeme?
2. Kinauwezo wa kusukuma Tani ngapi if not kilos?
3. Kikiharibika kinaenda garage au kwa fundi simu/ radio?
4. Kina shelf life ya miaka mingapi kwa engine take na max load capacity
..... basi nadhani kulikuwa na maswali mengi sana alipaswa kuyajibu kwenye speech yake siku ya uzinduzi! Maana wengi wanajiuliza maswali mengi sana juu ya ndinga hili! Hata hivyo, hongera nyingi zimfikie kwa ubunifu huu na uthubutu wake!
 
Yani ashindane na kirikuu ambayo Bei yake ni chini karibia 12m afu hiyo yake kasema imemgarimu zaidi ya 40 atashindanaje Sasa hapo..????
Tuwe tunasikiliza na kuelewa..milioni 40 ni kwa lile gari la kwanza ambalo errors zilikuwa nyingi..bei ya hilo gari amesema kwa sasa ni milioni 10
 
Nchi za wenzeti ni zipi..?
Nani kaingiza gari sokoni kienyeji?

Nchi za wenzetu ni watengenezaji wakubwa wa magari duniani. Marekani, Western Europe na Asia[Far East].

Hakuna nimemtaja kwamba kaingiza gari kienyeji ila point yangu ilikuwa hizo nchi mpaka gari inaingia sokoni inapitia test nyingi na siyo mtu kulitengeneza na kulitia sokoni.

Na zipo gari nyingi ambazo zimefeli baadhi ya test.

Nimeeleweka?
 
Sichukulii kama ni ubunifu mkubwa na hatua kubwa tu, bali ni hamasa kwa vijana ambao tulizoea kulalamika "poor gov support".

Hii ni njia, kikubwa serikali muangalieni bw Kp hasa kwenye suala zima la kodi.

Pia atoe matoleo mengine kama SUV na Sedans. Tutanunua vya kwetu huo ndio uzalendo wa kweri (in Magu voice).
 
Nchi za wenzetu ni watengenezaji wakubwa wa magari duniani. Marekani, Western Europe na Asia[Far East].

Hakuna nimemtaja kwamba kaingiza gari kienyeji ila point yangu ilikuwa hizo nchi mpaka gari inaingia sokoni inapitia test nyingi na siyo mtu kulitengeneza na kulitia sokoni.

Na zipo gari nyingi ambazo zimefeli baadhi ya test.

Nimeeleweka?
Sijakuelewa bado unazunguka zunguka
 
Back
Top Bottom