Kwa hakika Rais Samia Anastahili pongezi sana kutoka kwa jumuiya ya wanamichezo.maana ameleta chachu kubwa sana na hamasa ya kipekee sana katika michezo tangia ameingia madarakani.kwa kuwa kwa sasa wachezaji wanapambana sana wawapo uwanjani ili waweze kupata zawadi ya mama ya pesa taslimu.
Rais Samia Ni Mpango wa Mungu Mwenyewe,maana kila awekapo mkono ni lazima pafanikiwe.mikono ya Rais Samia imebarikiwa na kupewa kibali na Mungu mwenyewe na ndio maana akiweka tu mkono wake mahali popote pale ni lazima ushindi wa kishindo upatikane.ndio maana kama Taifa ni washindi katika kila kitu kinachojitokeza mbele yetu.
Hongera sana Rais Samia umekata kiu ya watanzania ya kutaka kuona tunapata timu mbili hatua ya robo fainali.