Mkuu hao jamaa wanafanya kazi tukufu sema tu ndio hivyo hawatangazwi, kazi nyingi na nyeti kwa nchi hii wanafanya lkn sifa zinakwenda kwa wengine maana maadili hayaruhusu kutangazwa, hata huko nyuma walifanya lkn mchukua maamuzi aliwaangusha hivi hamjiulizi ile orodha ya madudu bandari aliyokabidhiwa PM Majaliwa pale bandari ilitoka wapi? ilikuwepo mezani kwa mtu tayar lkn ndio hivyo tena hakuna wakumlazimisha achukue hatua ndio maana nashauri Sheria ya TISS ifanyiwe marekebisho hawa jamaa wapewe meno mtaona mambo yatakavyokuwa good maana sheria ya sasa inawawajibisha chini ya Rais so akitokea Rais asiyechukua hatua vitu vyao vingi vinabumia mezani kwa Rais..