Hongera Spika Dkt. Tulia Ackson. Kuna haja MaSpika wetu iwe lazima kuwa Wanasheria?

Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala za Kwa Maslahi ya Taifa, makala ya leo ni kuhusu umuhimu wa viongozi wetu na haswa wakuu wa Mihimili lazima sio tuu wawe wasomi, weledi na wachapakazi, bali lazima wawe Bright, brilliant na wabobezi wa fani husika.

Niko mahali nafuatilia Bunge Live, kiukweli kabisa nimekuwa very impressed na jinsi Madam Spika Dr. Tulia Akson anavyoliongoza Bunge.

Juzi aliifanua vizuri Ripoti ya CAG na kuifafanua ile kauli ya hasira ya Mama ya stupid na "Watupishe", ni walioongeza "cha juu" kwenye ununuzi wa ndege ya mizigo, na sio wote waliotajwa kwenye ripoti ya CAG.

Leo Mbunge wa Liwale kaibua kubwa kuliko Bungeni kuwa Bwawa la Mwalimu Nyerere, JNHPP japo liko Rufiji, bwawa hilo liko wilaya ya Liwale mkoani Lindi, na sio Mikoa ya Pwani na Morogoro, hivyo wilaya ya Liwale inastahili asilimia 60% ya mgao wa fedha za CSR ya JNHPP, lakini Liwale haikupata hata senti 5!.

Spika Tulia akaingilia kati kwa kumuuliza Mhe. Mbunge athibitishe Bwawa la JNHPP liko Liwale, Mbunge akasema lipo Liwale!.

Dr. Tulia akafafanua tofauti ya mahali Bwawa lilipo na the catchment area maji ya kulijaza bwawa yanakotoka!. Mhe. Mbunge akang'ang'ana bwawa liko Liwale!.

Dr. Tulia akamwambia Mhe Mbunge kuwa yeye na wabunge wamekwenda lilipo na hadi kubonyeza kitufe kukajaza maji, bwawa liko Rufiji na sio Liwale, hivyo akamwambia mbunge akae kwanza.

Kisha akauliza wahusika kama wapo waeleze Bunge bwawa la JNHPP liko wapi, ndipo akasimama Naibu Waziri wa Nishati, Byabato, akasema kwa mujibu wa ramani zao, bwawa la JNHPP liko Rufiji na Morogoro, ila kama Mbunge anayo ramani yake inayoonyesha bwawa liko Liwale, ailete na kuwaelimisha wengine tuko tayari kujifunza!.

Mbunge mwingine akasimama kuchangia kuwa bwawa liko Rufiji ila the catchment area ya maji ya bwawa hilo yanatoka Liwale.

Ndipo Spika Tulia akampiga darasa Mbunge huyo kuwa bwawa la JNHPP liko Rufiji ila maji ya kulijaza yanaweza kutiririka kutoka popote na kumruhusu kumalizia kuchangia.

Hii ndio faida ya kuwa na Spika msomi wa sheria, natumaini wengi unakumbuka uendeshaji wa Bunge enzi za Spika Sitta pia alikuwa ni msomi wa sheria.

Kwa vile mimi ni mtu wa mastori mastori
Ngoja niwape mastori ya Mimi na Dr. Tulia Akson, kwa msiopenda mastori jump kule chini

Tanzania tunakwama baadhi ya maeneo kwasababu tuna viongozi vilaza!. We can afford kuwa na wabunge vilaza, ndani ya Bunge la JMT but we can't afford kuwa na wabunge vilaza kwenye Bunge la EALA! Ubunge EALA, Wito Kwa CCM, Msiangalie Ukwasi, Tuteulieni, Wazalendo wa Kweli wa Taifa Hili, Wenye Uwezo na Uzoefu wa Kimataifa Kutuwakilisha Ipasavyo

Ili Tanzania tuweze kupata viongozi bora,, the best of the best, hatuwezi kuuendeleza ule ujinga uliochomekewa ndani ya katiba yetu kiubatili, kuwaachia kakikundi ka watu wachache kuamua huyu ni wenzetu mpe uongozi, hata kama ni vilaza!, na huyu sii wenzetu kata jina tupa kule, hatumuhitaji, hata kama ni the best bright and Brilliant

Kwa maoni yangu, nashauri Spika asitokane na ukanda wa chama cha siasa, Spika Dr. Tulia huyu, tunayemsifu leo, kuwa anakwenda kuwa Spika bora ndio Dr. Tulia yule yule aliye naibu Spika chini ya bora Spika, na alinyamaza kimya wakati katiba yetu ikikanyagwa Je, Bunge letu linaendeshwa kikada? Ili tuwe na Bunge la haki, lenye uwezo wa kuisimamia Serikali Kikamilifu, kuna haja Spika asitokane na vyama?

Hitimisho,
Nahitimisha kwa lile swali, la msingi la makala hii, kufuatia Spika Sitta na Spika Dr. Tulia Akson, ambao ni wanasheria, kuwa so good kwenye uendeshaji wa Bunge la JMT, kwasababu, they are smart, bright & brilliant! kuna haja sasa, kuanzia sasa kuhakikisha MaSpika wetu wote lazima wawe wanasheria?.

Wasalaam

Paskali
Kaka paskali ,
Kila mmoja humu ndani anajua uwezo wako na u nguli wako katika tasnia ya habari,
Hongera Sana

Narudi kwenye kumpongeza Dr.Tulia umeandika mengi na Kuna wengi wetu hatukua tunayajua yaan mm binafsi ume add knowledge kuhusu historia ya Dr.Tulia,

Kuhusu makala yako imenifikilisha kidogo kuhusu aina ya wawakilishi wetu Bungeni swali je tuchague watu walio pata first class na wabobevu NDIO watuwakilishe Ili kujikwamua hapa tulipo?

Pia huwezi msifia sana Kwa kuweza kwake ku settle iyo hoja ya Mbunge anae sema bwawa lipo Liwale? Ukiwa na uelewa kidogo tu wa kijamii mtu yeyote anaweza kulijib😊

Wasalaam
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala za Kwa Maslahi ya Taifa, makala ya leo ni kuhusu umuhimu wa viongozi wetu na haswa wakuu wa Mihimili lazima sio tuu wawe wasomi, weledi na wachapakazi, bali lazima wawe Bright, brilliant na wabobezi wa fani husika.

Niko mahali nafuatilia Bunge Live, kiukweli kabisa nimekuwa very impressed na jinsi Madam Spika Dr. Tulia Akson anavyoliongoza Bunge.

Juzi aliifanua vizuri Ripoti ya CAG na kuifafanua ile kauli ya hasira ya Mama ya stupid na "Watupishe", ni walioongeza "cha juu" kwenye ununuzi wa ndege ya mizigo, na sio wote waliotajwa kwenye ripoti ya CAG.

Leo Mbunge wa Liwale kaibua kubwa kuliko Bungeni kuwa Bwawa la Mwalimu Nyerere, JNHPP japo liko Rufiji, bwawa hilo liko wilaya ya Liwale mkoani Lindi, na sio Mikoa ya Pwani na Morogoro, hivyo wilaya ya Liwale inastahili asilimia 60% ya mgao wa fedha za CSR ya JNHPP, lakini Liwale haikupata hata senti 5!.

Spika Tulia akaingilia kati kwa kumuuliza Mhe. Mbunge athibitishe Bwawa la JNHPP liko Liwale, Mbunge akasema lipo Liwale!.

Dr. Tulia akafafanua tofauti ya mahali Bwawa lilipo na the catchment area maji ya kulijaza bwawa yanakotoka!. Mhe. Mbunge akang'ang'ana bwawa liko Liwale!.

Dr. Tulia akamwambia Mhe Mbunge kuwa yeye na wabunge wamekwenda lilipo na hadi kubonyeza kitufe kukajaza maji, bwawa liko Rufiji na sio Liwale, hivyo akamwambia mbunge akae kwanza.

Kisha akauliza wahusika kama wapo waeleze Bunge bwawa la JNHPP liko wapi, ndipo akasimama Naibu Waziri wa Nishati, Byabato, akasema kwa mujibu wa ramani zao, bwawa la JNHPP liko Rufiji na Morogoro, ila kama Mbunge anayo ramani yake inayoonyesha bwawa liko Liwale, ailete na kuwaelimisha wengine tuko tayari kujifunza!.

Mbunge mwingine akasimama kuchangia kuwa bwawa liko Rufiji ila the catchment area ya maji ya bwawa hilo yanatoka Liwale.

Ndipo Spika Tulia akampiga darasa Mbunge huyo kuwa bwawa la JNHPP liko Rufiji ila maji ya kulijaza yanaweza kutiririka kutoka popote na kumruhusu kumalizia kuchangia.

Hii ndio faida ya kuwa na Spika msomi wa sheria, natumaini wengi unakumbuka uendeshaji wa Bunge enzi za Spika Sitta pia alikuwa ni msomi wa sheria.

Kwa vile mimi ni mtu wa mastori mastori
Ngoja niwape mastori ya Mimi na Dr. Tulia Akson, kwa msiopenda mastori jump kule chini

Tanzania tunakwama baadhi ya maeneo kwasababu tuna viongozi vilaza!. We can afford kuwa na wabunge vilaza, ndani ya Bunge la JMT but we can't afford kuwa na wabunge vilaza kwenye Bunge la EALA! Ubunge EALA, Wito Kwa CCM, Msiangalie Ukwasi, Tuteulieni, Wazalendo wa Kweli wa Taifa Hili, Wenye Uwezo na Uzoefu wa Kimataifa Kutuwakilisha Ipasavyo

Ili Tanzania tuweze kupata viongozi bora,, the best of the best, hatuwezi kuuendeleza ule ujinga uliochomekewa ndani ya katiba yetu kiubatili, kuwaachia kakikundi ka watu wachache kuamua huyu ni wenzetu mpe uongozi, hata kama ni vilaza!, na huyu sii wenzetu kata jina tupa kule, hatumuhitaji, hata kama ni the best bright and Brilliant

Kwa maoni yangu, nashauri Spika asitokane na ukanda wa chama cha siasa, Spika Dr. Tulia huyu, tunayemsifu leo, kuwa anakwenda kuwa Spika bora ndio Dr. Tulia yule yule aliye naibu Spika chini ya bora Spika, na alinyamaza kimya wakati katiba yetu ikikanyagwa Je, Bunge letu linaendeshwa kikada? Ili tuwe na Bunge la haki, lenye uwezo wa kuisimamia Serikali Kikamilifu, kuna haja Spika asitokane na vyama?

Hitimisho,
Nahitimisha kwa lile swali, la msingi la makala hii, kufuatia Spika Sitta na Spika Dr. Tulia Akson, ambao ni wanasheria, kuwa so good kwenye uendeshaji wa Bunge la JMT, kwasababu, they are smart, bright & brilliant! kuna haja sasa, kuanzia sasa kuhakikisha MaSpika wetu wote lazima wawe wanasheria?.

Wasalaam

Paskali
Hivi catchment area y Rufiji inatokaje Liwale na kuwa significant wakato maji mengi ya mto Rufiji inatoka katika mito ya Ruaha na Kilombero? Na catchment area ya Ruaha inaanzia as far as upande wa kaskazini mwa mlima Rungwe, Mitelemko ya Mbarali na Makete, Iringa, Mtera hadi milima ya Udzungwa.
 
Seriously Dr. Tulia Mimi binafsi naona ni speaker Bora kwanza anaongoza Bunge Kwa kutulia na umakini mkubwa Mbeya sisi tumepata Mbunge

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
Hata na mimi naunga mkono, nimekuwa nikisikiliza kwa makini majibu yake, kwa kweli huwa yametulia.

Way to go Dr. Tulia, hongera sana.
 
wapo nchi hii kwa unavyoona?
Paskal hebu musome huyu bwana
"Without the study of sociology, the training and knowledge of the candidates aspiring to hold high posts in the administrative set-up of their country will be incomplete and imperfect." (Puja Mondal)
 
Pasco, huwa una mawazo mazuri most of the times, lakini taaluma yako inakufanya uwe na winding stories.
Nakuunga mkono hata hivyo.
Jana suala la Mwigulu kumuingiza Rais kama mlipaji mkuu katika malipo ya serikali, Dr Tulia amelicrush kisomi sana, hadi "Dr" Mwigulu akabaki mdomo wazi.
Aliyehoji na kuzua mjadala huo ni mbunge wa simanjiro Ole Sendeka .

Tulia alijazia nyama tu wacheni kumpasifa asizokuwa nazo huyo Tulia.
 
Sifa ya kujadili bwawa lilipo kweli si unamkosea heshima mwalimu wako, hizi billioni zinazoliwa ndio sheria yake ilitakiwa kutumika, wabunge wanawake wa UVICO hapa ndio heshima ya huyu mama iliingia shaka, kwamba wanasheria wa nchi hii hawatendi haki pale maslahi yao na chama chao yanapoguswa. Mwanasheria anyestahili sifa ni yule anayetenda haki sawa kwa watu wote sio kuwa mwalimu wako tu.
Bila kubebwa na Jiwe Tulia tusingemjua kabisa.

Sasa hayo masifa wanayo mptwisha naona kama maigizo
 
Pascal yani maigizo ya bwawa lipo Liwale mara Rufiji na Morogoro ndio yamukukosha sana kuhusu Spika?
Bunge lake halina mvuto, Bunge halina meno wala halina msaada kwa Wananchi.
 
Aliyehoji na kuzua mjadala huo ni mbunge wa simanjiro Ole Sendeka .

Tulia alijazia nyama tu wacheni kumpasifa asizokuwa nazo huyo Tulia.
Dr Tulia kiukweli yupo vizuri upstairs ila tu kutokana na mifumo ilivyo sometimes ni lazima aonyeshe ukada !!
 
She is just so good!.
P
Ngoja tuupambe Uzi na picha yake nzuri
IMG-20230405-WA0009.jpg

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Ili Tanzania tuweze kupata viongozi bora,, the best of the best, hatuwezi kuuendeleza ule ujinga uliochomekewa ndani ya katiba yetu kiubatili, kuwaachia kakikundi ka watu wachache kuamua huyu ni wenzetu mpe uongozi, hata kama ni vilaza!, na huyu sii wenzetu kata jina tupa kule, hatumuhitaji, hata kama ni the best bright and Brilliant
Mzee Mayalla unajaribu kusukuma gari huku ukiwa ndani yake....

Wewe ulishakiri kuwa Ccm ndio dola yenyewe, hivyo endeleeni kuishi kwa fadhila na huruma zake maana ndio maisha mliyochagua.
 
Pascal, brilliance hapo iko wapi? Mtoto wa darasa la Saba au sekondari aliyefundishwa vema regional geography mbona atajibu tu vizuri?
Hapo excellence ya Sheria Iko wapi? Watu ilipotumika Sheria?

Bado una fight for uteuzi. Kazana more and more
Hata mimi nimemsoma mleta mada lakini sijaona chochote kilichomfanya amsifie hivyo. Bila shaka mleta mada anafukuzia teuzi.
 
H
Kwa kweli Tulia ni msomi wa hali ya juu mno. Siasa zake ni za kimkakati sana za kumkimbiza mwizi kimyakimya. Angesema aende na siasa za kuropoka majukwaani kama Sugu basi 2025 angegaragazwa vibaya. Ila hadi muda huu tayari kashashinda 2025 Mbeya mjini kwa jinsi anavyowagusa wapiga kura moja kwa moja.
Hebu tueleze jinsi alivyowagusa.
 
Back
Top Bottom