Hospitali ya Mloganzila yaanzisha huduma ya kurekebisha 'shape' ya mwili
Taarifa mpya iliyotolewa leo na Hospitali ya Muhimbili ( Mlonganzila ) , inaeleza kwamba Hospitali hiyo itaanza kufanya upasuaji ili kurekebisha Makalio na Matiti .

Screenshot_2023-10-10-18-28-51-1.png
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa mara ya kwanza nchini itafanya huduma za kibingwa bobezi za upasuaji wa kupunguza uzito na upasuaji rekebishi (Bariatric and Reconstructive surgery) ambao utahusisha kupunguza mafuta na kurekebisha sehemu ya mwili mfano kupunguza au kuongeza ukubwa wa matiti na makalio, kupunguza tumbo au nyama kwenye mikono na sehemu nyingine za mwili.

Mkuu wa Idara ya Upasuaji Dkt. Eric Muhumba amesema upasuaji huo utaanza kufanyika kuanzia October 27,2023 na utafanywa na Wataalamu wa MNH-Mloganzila kwa kushirikiana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa kupunguza uzito na Upasuaji Rekebishi kutoka India, Dkt. Mohit Bhandari pamoja na MedINCREDI.

“Upasuaji huu utafanyika kwa bei nafuu sana ukilinganisha na endapo Mtu angeenda kutafuta huduma hizi nje ya Nchi, hivyo tumeamua kuwasogezea Wananchi huduma hizi na kuwapunguzia usumbufu wa kusafiri nje ya Nchi kutafuta huduma hizi”
Naona ya taanza kukosa soko,wadangaji wataanza kushusha bei.
 
Sasa Hospital ya Mloganzila kuanza kutoa Huduma ya kuongeza Shepu na Matiti kwa wenye Uhitaji

Source Ayo tv

Sasa unaweza kutengeneza " Kalio la Mloganzila" au " Titi la Mloganzila"

Tanzania bhana!

Mlale Unono huku mkiwaombea Wana wa Israel na Palestine [emoji3][emoji3]
Hii Hospitali recently imekuwa ikitrend kwa taarifa hovyo hovyo tu
Hivi wamekosa mambo mengine ya kushughulikia hadi waanze kutrend kwa habari za beauty industry ?
 
Back
Top Bottom