Hotuba nyingi za viongozi wa Afrika kwenye mkutano wa UN zimejaa malalamiko

Hotuba nyingi za viongozi wa Afrika kwenye mkutano wa UN zimejaa malalamiko

Lawama zitabaki palepale kwa nchi za kibeberu, hawa jamaa huwa hawataki kiongozi wa Africa anayejielewa, ukiingia madarakani ukawa na msimamo mkali wa kizalendo watakuletea zengwe tu! Hasa wakiona unaleta maproject makubwa ya ukombozi wa Kiuchumi ujue kabisa roho yako umeiweka rehani au nchi yako itadhoofishwa na makundi ya kigaidi, au kuwekewa vikwazo vya kijinga kijinga tu. Kama unataka ku-transform nchi Yako jitoe sadaka kwaajili ya Nchi yako.
Tofautisha hotuba hii ya Israel na za Afrika

View: https://www.youtube.com/watch?v=kNH85jgzJ0Y
 
Ukweli ni Huu kifupi ni Aibu mie mtazamo wangu naona Trump alikuwa sahihi juu yetu watu weusi AFRIKA yote imejaa vituko kutoka kwa hao watawala wetu mie Binafsi naona uko ntakuja kuzikwa tu.View attachment 2761331
Ukweli ni kuwa Afrika karibia yote ipo kwenye utawala wa laana, utawala wa shetani.

Viongozi wa Afrika wanajivunia na kuonea fahari uovu.

Fikiria kiongpzi anasema kuwa Polisi wa CCM hawezi kulenga shabaha; shabaha anayoionea fahari ni ya kuwaua watu wanaopinga uovu wa viongozi. Yaani kiongozi unajisifia kwa ushetani.
 
ni kweli wamelalama sana.

Lakini pia yapo mambo ya msingi sana na ya maana wanayo yalalamikia mathalani kuhusu udhaifu wa taasisi za kidunia kama vile UN na Barazani la usalama katika kuchukua hatua katika majanga na migogoro duniani,

Kadhalika kutokua na usawa wa uwakilishi kwa Taasisi za kidunia kama vile WB, IMF, UN Security Council baina ya Africa, America, Asia, Ulaya n.k
hii imezorotesha utekelezaji wa mambo mengi sana na hata imefikia mahali inaonekana mfano anachafua mazingira mwingine halafu mwingine anapewa fedha za kutunza mazingira.

Rejea 17 Sustainable Development Goals utagundua na kubaini vizuri sana malalamiko yenye mantiki ya viongozi wa Africa huko UN.
Shukran kwa bandiko.
Sasa kama huko nchini kwenu, kuanzia Rais mpaka watendaji, wote ni wevi, nani atakupa nafasi ya uongozi WB au IMF? Hizo taasisi zikipewa Waafrika waziongoze, watauza mpaka ofisi.
 
Misaada ni laana na apokeaye misaada ulaanika zaidi.
Ni kanuni ya asili ombaomba ataendelea kuomba.
Wazungu wanaijua sana siri hii.
Thus wanawasaidia waafrika ili kuchukua baraka zetu kupitia baraka zetu wao ndio wazidi kutajirika zaidi na sisi kuzidi kuwa masikini zaidi.
Si kwamba wao wamemaliza matatizo Yao au wanatupenda sana bali wanaijua Siri hii.
 
Ila bora wanaoingia kwa uchungu,wanaweza kuwa na nafuu kubwa kuliko wanaoingia kwa tamaa😂😂😂
Huwa wanaanza kama malaika lakini mwisho ugeuka shetani,nao hawataki kuachia utamu utaka kuwarithisha watu wao
 
Africa itakuwa na maendeleo siku misaada itakapokoma.
Check mfano wa kanisa katoliki Africa zamani liliendeshwa na sadaka za wazungu baada ya wazungu kukata misaada na sadaka kwa kanisa la Africa,linaendeshwa kwa michango na sadaka za waumini hao hao waafrika bila msaada wa wazungu.
Africa inaweza endelea bila misaada ni ishu tu ya kubadili mifumo ya fikra na uchumi.
Mfano Kodi komozi kuwakomoa walipa kodi au wachache ndio wamiliki magari kwa element za kijima mfano ant dumping na mambo ya traffic control ni upumbavu mtupu hizi sababu.
 
Sasa kama huko nchini kwenu, kuanzia Rais mpaka watendaji, wote ni wevi, nani atakupa nafasi ya uongozi WB au IMF? Hizo taasisi zikipewa Waafrika waziongoze, watauza mpaka ofisi.
hawakuomba nafasi ya kuongoza mashirika wanahitaji usawa miongoni mwa hayo mashirika
 
Ufanana matendo ya kifisi
Viongozi wetu wana akisi tabia zetu sisi Waafrika hasa katika kupenda dezo kwa mfano leo hii jumatatu 25 Septemba Samia Suluhu akisema nawanyang'anya mali matajiri wote halafu nawapa masikini atashangiliwa kwa vifijo na hoi hoi na watu wazima na mvi zao watagalagala kwa furaha.

Wakati hao hao Wananchi unamkuta anashinda kwenye bao kijiwe cha kahawa amesimika bendera ya Yanga huko kwake ana wake watatu wawili wanauza mihogo mibichi kwenye karai wanazunguka mitaani.
 
Sio kweli mbona Kagame ni mwembamba mrefu na ana pua iliyochongoka? atafananaje na Mfalme wa Eswatini mfupi mnene mwenye pua pana.

Hebu fafanua zaidi
Kagame ana akili nyingi sana kulko viongozi wengi wa Afrika, Rwanda iko kama Ulaya. Ona inavyofanya branding ya nchi yake duniani. Anadhamini hadi timu za ligi kuu ya Ulaya.
 
Misaada ni laana na apokeaye misaada ulaanika zaidi.
Ni kanuni ya asili ombaomba ataendelea kuomba.
Wazungu wanaijua sana siri hii.
Thus wanawasaidia waafrika ili kuchukua baraka zetu kupitia baraka zetu wao ndio wazidi kutajirika zaidi na sisi kuzidi kuwa masikini zaidi.
Si kwamba wao wamemaliza matatizo Yao au wanatupenda sana bali wanaijua Siri hii.
ni heri ya yule anaetoa kuliko anaepokea. Wazungu hawatoi misaada bali wanatoa chambo. Kuna wazungu wengi huko kwao ambao ni maskini sana na wenye uhitaji wa kusaidiwa lakini hawapewi misaada hiyo, iweje wakupe msaada wewe mwafrika mvivu mwenye ardhi kubwa ya kulima, kufuga na kuvua? think critically blaza.
 
Kagame ana akili nyingi sana kulko viongozi wengi wa Afrika, Rwanda iko kama Ulaya. Ona inavyofanya branding ya nchi yake duniani. Anadhamini hadi timu za ligi kuu ya Ulaya.
Ni mazingira ndio yamemfanya awe hivyo amepitia ukimbizini amepitia umasikini kapitia jeshi ana exposure ya kutosha amepitia Rebelion with a cause kakomesha genocide nk.

Ana madhaifu yake sikatai ila wasiwasi wangu ikitokea akaondoka hienda Rwanda inaweza kurudi kwenye machafuko ya kikabila.
 
Viongozi wa nchi zote za dunia wanakutana Marekani kwenye mkutano mkuu wa Baraza la usalama la umoja wa mataifa (General Assembly of United Nations). Hotuba nyingi za viongozi kutoka Afrika ni za malalamiko kuhusu nchi za Magharibi na Marekani kama chanzo Chao kikuu Cha matatizo kwenye nchi zao. Hotuba nyingi za viongozi wetu ni kuhusu wazungu kutotimiza ahadi zao za kutoa mapesa kwa nchi za Afrika kugharimia miradi Yao, madeni makubwa wanayodaiwa na ukosefu wa masoko na technology.

Bahati mbaya sijamsikia kiongozi wetu hata mmoja akizungumzia shida wanazozisababisha wao wenyewe kama vile:
1. Kuiba kura kwenye chaguzi
2. Kung'ang'ania madarakani
3. Wizi wa mali za wananchi wao na ubadhilifu.
4. Matumizi mabaya ya mikopo wanayopewa.
5. Kushindwa kukusanya kodi
6. Rushwa kwenye nchi zao.
7. Viongozi kujiwekea kinga za kutokushitakiwa.

Bahati mbaya nchi za Magharibi wanayajua madhaifu yote ya viongozi wa Afrika, ndio maana wakati wa hotuba za viongozi kutoka Afrika Wazungu wengi wanapuuza na wanatoka nje.

Afrika hawana mshipa hata mmoja wa aibu, kazi Yao ni kuwanyooshea vidole nchi za Western na kusahau udhaifu wao kwanza.

Mfano, nani anawazuia nchi za Afrika kuuziana bidhaa wao kwa wao kwa kutumia fedha zao. Nani kawazuia waafrika kuondoa VISA kati ya nchi na nchi ili watu Waafrika wawe huru kwenda na kutoka nchi nyingine ya ya Africa kufanya kazi au biashara? Nani kawazuia waafrika wasilime chakula Chao? Nani kawazuia kukusanya kodi?
Malalamiko huwa ni mazuri hata Mungu huwa anayapenda. Kibaya ni lawama
 
Ni mazingira ndio yamemfanya awe hivyo amepitia ukimbizini amepitia umasikini kapitia jeshi ana exposure ya kutosha amepitia Rebelion with a cause kakomesha genocide nk.

Ana madhaifu yake sikatai ila wasiwasi wangu ikitokea akaondoka hienda Rwanda inaweza kurudi kwenye machafuko ya kikabila.
wasiwasi wako sio wa kubezwa kabisa, uongozi wa one mana show badala ya system ndiyo chanzo cha mara ujamaa, mara ruksa, mara kilimo kwanza, mara viwanda kwanza, mara siasa ni kilimo, BRN, mara kasi mpya na mara kazi iendelee. vurugumechi ya vipaumbele vya taifa.
 
Watawala kutoka Afrika hasa kusini mwa Sahara desert,ni wajinga wa kutupwa,hizo hutuba uko UN ni ishara ya ujinga wao,ambao wamejikita katika kutoa lawama badala ya kutafuta suluhu ya matatizo,wao wanawaza chaguzi tu kuliko kutatua matatizo ya wananchi.
 
Kama nchi za Afrika zikitaka misaada mingi kutoka nchi za Magharibi ni sawa na kutaka nchi za Magharibi zituibie sana rasilimali zetu. Sio kweli kabisa kwamba pesa wanazotumia kuyafadhili mashirika ya umoja wa mataifa na misaada/mikopo wanayotupatia inatokana na kodi ya walipakodi wao, lahsha!!! Pesa hizi zinatokana na dhuluma na faida kubwa kwenye biashara za dunia zisizo na uwiano wa haki, kutaifisha mali za watu na nchi nyingine, riba kubwa za mikopo wanayotukopesha, kupora mali za nchi wakati na baada ya vita, kuwapunja malipo wahamiaji wanaofanyakazi kwao, na mikataba ya kinyonyaji. Waafrika wasifikiri kuwa pesa wanazopewa ni kodi za wazungu, noooo! Wazungu hawana cha bure.
actually,
kwa tones za viongozi wengi wa Africa, hawako tena na interests za misaada ya ng'ambo wanahitaji tu usawa katika kupanga, kuamua na kutekeleza agenda za pamoja kwa maslahi ya wote.
 
Back
Top Bottom