Hiyo ni kweli, hata JPM alipojifanya ananunua ndege kwa pesa tasilimu na kujenga barabara na reli ya umeme, mabeberu wakamtangazia kuwa Tanzania imeingia uchumi wa kati. Kuingia uchumi wa kati maana haye huhitaji misaada wala mikopo ya riba nafuu inayotolewa kwa nchi maskini. Hii ilikuwa njia ya kumkomesha na wala sio kweli kwamba uchumi wa Tanzania umekuwa kwa kiasi hicho. Lakini, hii haisababishi nchi kuingia mikataba mibovu ya uwekezaji kwenye madini, gesi, nk, hiyo haisababishi nchi kushindwa kukusanya kodi kikamilifu, kupanga miji na ardhi yake kwa matumizi mbalimbali, kuzoa takataka au ...... Leo hii vinapimwa ardhi ya viwanja tu lakini haipimwi ardhi kwaajili ya kilimo, ufugaji na viwanda. Ardhi ya kilimo inageuzwa kuwa ardhi ya makazi huko vijijini, sijui watalima wapi.