Hotuba nyingi za viongozi wa Afrika kwenye mkutano wa UN zimejaa malalamiko

Tofautisha hotuba hii ya Israel na za Afrika

View: https://www.youtube.com/watch?v=kNH85jgzJ0Y
 
Ukweli ni Huu kifupi ni Aibu mie mtazamo wangu naona Trump alikuwa sahihi juu yetu watu weusi AFRIKA yote imejaa vituko kutoka kwa hao watawala wetu mie Binafsi naona uko ntakuja kuzikwa tu.View attachment 2761331
Ukweli ni kuwa Afrika karibia yote ipo kwenye utawala wa laana, utawala wa shetani.

Viongozi wa Afrika wanajivunia na kuonea fahari uovu.

Fikiria kiongpzi anasema kuwa Polisi wa CCM hawezi kulenga shabaha; shabaha anayoionea fahari ni ya kuwaua watu wanaopinga uovu wa viongozi. Yaani kiongozi unajisifia kwa ushetani.
 
Sasa kama huko nchini kwenu, kuanzia Rais mpaka watendaji, wote ni wevi, nani atakupa nafasi ya uongozi WB au IMF? Hizo taasisi zikipewa Waafrika waziongoze, watauza mpaka ofisi.
 
Misaada ni laana na apokeaye misaada ulaanika zaidi.
Ni kanuni ya asili ombaomba ataendelea kuomba.
Wazungu wanaijua sana siri hii.
Thus wanawasaidia waafrika ili kuchukua baraka zetu kupitia baraka zetu wao ndio wazidi kutajirika zaidi na sisi kuzidi kuwa masikini zaidi.
Si kwamba wao wamemaliza matatizo Yao au wanatupenda sana bali wanaijua Siri hii.
 
Ila bora wanaoingia kwa uchungu,wanaweza kuwa na nafuu kubwa kuliko wanaoingia kwa tamaa😂😂😂
Huwa wanaanza kama malaika lakini mwisho ugeuka shetani,nao hawataki kuachia utamu utaka kuwarithisha watu wao
 
Africa itakuwa na maendeleo siku misaada itakapokoma.
Check mfano wa kanisa katoliki Africa zamani liliendeshwa na sadaka za wazungu baada ya wazungu kukata misaada na sadaka kwa kanisa la Africa,linaendeshwa kwa michango na sadaka za waumini hao hao waafrika bila msaada wa wazungu.
Africa inaweza endelea bila misaada ni ishu tu ya kubadili mifumo ya fikra na uchumi.
Mfano Kodi komozi kuwakomoa walipa kodi au wachache ndio wamiliki magari kwa element za kijima mfano ant dumping na mambo ya traffic control ni upumbavu mtupu hizi sababu.
 
Sasa kama huko nchini kwenu, kuanzia Rais mpaka watendaji, wote ni wevi, nani atakupa nafasi ya uongozi WB au IMF? Hizo taasisi zikipewa Waafrika waziongoze, watauza mpaka ofisi.
hawakuomba nafasi ya kuongoza mashirika wanahitaji usawa miongoni mwa hayo mashirika
 
Ufanana matendo ya kifisi
Viongozi wetu wana akisi tabia zetu sisi Waafrika hasa katika kupenda dezo kwa mfano leo hii jumatatu 25 Septemba Samia Suluhu akisema nawanyang'anya mali matajiri wote halafu nawapa masikini atashangiliwa kwa vifijo na hoi hoi na watu wazima na mvi zao watagalagala kwa furaha.

Wakati hao hao Wananchi unamkuta anashinda kwenye bao kijiwe cha kahawa amesimika bendera ya Yanga huko kwake ana wake watatu wawili wanauza mihogo mibichi kwenye karai wanazunguka mitaani.
 
Sio kweli mbona Kagame ni mwembamba mrefu na ana pua iliyochongoka? atafananaje na Mfalme wa Eswatini mfupi mnene mwenye pua pana.

Hebu fafanua zaidi
Kagame ana akili nyingi sana kulko viongozi wengi wa Afrika, Rwanda iko kama Ulaya. Ona inavyofanya branding ya nchi yake duniani. Anadhamini hadi timu za ligi kuu ya Ulaya.
 
ni heri ya yule anaetoa kuliko anaepokea. Wazungu hawatoi misaada bali wanatoa chambo. Kuna wazungu wengi huko kwao ambao ni maskini sana na wenye uhitaji wa kusaidiwa lakini hawapewi misaada hiyo, iweje wakupe msaada wewe mwafrika mvivu mwenye ardhi kubwa ya kulima, kufuga na kuvua? think critically blaza.
 
Kagame ana akili nyingi sana kulko viongozi wengi wa Afrika, Rwanda iko kama Ulaya. Ona inavyofanya branding ya nchi yake duniani. Anadhamini hadi timu za ligi kuu ya Ulaya.
Ni mazingira ndio yamemfanya awe hivyo amepitia ukimbizini amepitia umasikini kapitia jeshi ana exposure ya kutosha amepitia Rebelion with a cause kakomesha genocide nk.

Ana madhaifu yake sikatai ila wasiwasi wangu ikitokea akaondoka hienda Rwanda inaweza kurudi kwenye machafuko ya kikabila.
 
Malalamiko huwa ni mazuri hata Mungu huwa anayapenda. Kibaya ni lawama
 
wasiwasi wako sio wa kubezwa kabisa, uongozi wa one mana show badala ya system ndiyo chanzo cha mara ujamaa, mara ruksa, mara kilimo kwanza, mara viwanda kwanza, mara siasa ni kilimo, BRN, mara kasi mpya na mara kazi iendelee. vurugumechi ya vipaumbele vya taifa.
 
Watawala kutoka Afrika hasa kusini mwa Sahara desert,ni wajinga wa kutupwa,hizo hutuba uko UN ni ishara ya ujinga wao,ambao wamejikita katika kutoa lawama badala ya kutafuta suluhu ya matatizo,wao wanawaza chaguzi tu kuliko kutatua matatizo ya wananchi.
 
actually,
kwa tones za viongozi wengi wa Africa, hawako tena na interests za misaada ya ng'ambo wanahitaji tu usawa katika kupanga, kuamua na kutekeleza agenda za pamoja kwa maslahi ya wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…