Hotuba nyingi za viongozi wa Afrika kwenye mkutano wa UN zimejaa malalamiko


Watakwambia eti afrika ina demokrasia yake sio lazima ifanane na ya magharibi,upuuzi mtupu majizi yanataka kuendelea kunyonya wananchi wao huku yakijineemesha yenyewe viongozi wa afrika ni laana.
 
Inafikirisha sana kwa wenye Akili na wanaojali !! πŸ™πŸ™
 
Na yote hayo uliyoyaeleza Wazungu wanayajua yanafanyika sana Afrika !!
Tukiwalalamikia wanatuzoom tu kisha wanacheeeeka !!
 
Hata wakilalama vipi Wazungu wanawatazama tu maana Wazungu wanayajua yote yanayofanywa na hao wanaolalamika !!
 

Wala wazungu si chanzo cha matatizo 100%.
Utumwa ilipata nguvu maana sisi waafrika tuliuzana wenyewe kwa wenyewe.
watawala wengi wa kiafrika walipewa zawadi na vitu. Mbali mbali na mtu mweupe ili kuwauza wenzao, tena wengine walisaidia kuwakamata waafrika wenzao.

Hili mpaka leo linaendelea, viongozi wa kiafrika wanaongeka, kupenda pesa za mtu mweupe na kutoa sadaka rasilimali za nchi

Mpaka hapo mtu mweusi atakapo gundua chanzo cha matatixo yake ni yeye mwenyewe, hakuna litalobadilika
 
Kagame ana akili nyingi sana kulko viongozi wengi wa Afrika, Rwanda iko kama Ulaya. Ona inavyofanya branding ya nchi yake duniani. Anadhamini hadi timu za ligi kuu ya Ulaya.
Jamaa kweli anajitahidi sana tena sana !!
 

Ni sisi waafrika tumekosa msimamo tokea zamani. Viongozi wa hovyo tunao wapata ninsababu sisi wenyewe tunawaruhusu kwa jina la siasa.

Mtu mweupe anapata nguvu pale kiongozi wa nchi husika anapokuwa mtu wa tamaa ya mali na pesa. Wazungu kuonga kwao ni ishu ndogo

Walitokea akina sankara, lumumba wana harakati wa kweli. Nani aliwaua kama sio watu wao wa karibu ambao ni waafrika wenzetu?
 
Nashangaa ninapomsikia mtu anasingizia umasikini wa Africa eti ni sababu ya utumwa ! Kwani huo utumwa ndio umewafunza watu ukwapuaji na ubadhirifu kwenye mali za Afrika. ??!!
Maisha ya fahari tunayoishi ni kwa sababu ya Utumwa ?!
 
Kabisa !!
 
Tutawasingizia sana wazungu mkuu wakati shida ni sisi wenyewe.
 
Ndugu, hili neno ni la kweli kwa 100%, Democrats ni utamaduni wa kwao, ndiyo maana walipoiingiza kwenye nchi za kiarabu ambazo wao utamaduni wao wanaoongoza nchi zao kiimla na hawakua na shida yoyote, walipomezeshwa neno democrats wakapigana vibaya

Rejea pale Libya, walisukwa watu wachache na kulipwa pesa,kuhusu kumkataa Gaddafi kwamba ameongoza miaka mingi,kwamba wanatakiwa kudai demokrasia, walipojichanganya tu, mpaka leo wanajuta

Mtu awaye yote akitaka kujua demokrasia ni ngumu aende akai- apply nyumbani kwake akae ki-demokrasia na mke wake na watoto wake aone kitakacho tokea

Afrika ilitakiwa kua na taratibu zake zisizo ingiliwa maana haya mambo ya kuiga yamefeli pakubwa, we unafanya siasa watu wanagawana mapesa mengi kuendesha siasa ktk nchi ambazo hazina maji, madawa, umeme, barabara.. hamuoni kama huu ni ujinga mkubwa? Pesa za kuchimba maji watu wanaenda kununua magari wafanyie siasa, na lengo kubwa la kufanya hivi ni mzungu anajaribu kama Kuna watu wa chama fulani wako madarakani na wamewanyima dhahabu zao, Almasi zao, na baadhi ya wanacho taka kupora, basi wanaingia ku- support chama kingine ili kikifanikiwa wapitie hicho kukidhi matakwa yao, Democrats ni mtego mbaya na WA kishenzi sana hapa Africa.
 
Una hoja nzuri sana mkuu, ukweli ni kuwa hili bara linapuuzwa sana kwenye kila kitu, limegeuzwa eneo la majaribio ya chanjo na kuvunia rasilimali tu tena kwa bei sawa na bure.
Hakuna kitu kibaya kama kuwa tegemezi kwa mtu. Kama Afrika hatutaacha mentality ya kuwa bila kupewa msaada hatuwezi hatutoboi. Ni bora ya mkopo kuliko msaada.
 
Mitaala yetu ya elimu Ina kasoro nyingi sana. Wakoloni waliondoa SoMo la critical thinking kwenye mitaala waliyotuandikia. Elimu hii na jinsi ya kufikiria kwa kina ni muhimu sana. Mtoto wa kizungu wa darasa la 1 kama ukimpa pipi atakuuliza Kwanini unanipa "mimi", unataka nini kwangu. Ukimpa lift kwenye gari ataikataa mazima kama hakujui, akisikia sauti asiyoielewa anakimbia mbali na tukio. Hii ni kinyume na watoto wetu, watu wetu na hata viongozi wetu.
 
Afrika hatuna utamaduni wa demokrasia, hata malezi yetu hayana demokrasia, mtoto utalazimishwa kula, kunyamaza, kulala, kuswali, kwenda kanisani, kucheza mbali na wakubwa, kuvaa nguo inayokubalika kwenye familia, nk. Mama anachapwa na mtoto anachapwa. Demokrasia haiko majumbani haiwezi kuweko mitaani na kwenye taasisi.

Hebu ona kule mashuleni na vyuoni wasomi wetu wanakotoka je, Kuna demokrasia? Demokrasia haiwezi kuzuka TU ghafla kwenye Katiba ya nchi kwakuwa malezi ya viongozi wetu hayakuwa ya kidemokrasia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…