Hotuba imemuumbua sana...! Bado Lissu anafikira za kiharakati. Uharakati haulipi katika masuala mazito yanayohusu nchi.
Masuala mazito yanayohusu nchi yanahitaji, Mipango, Mbinu bora kabisa ya kutekeleza mipango hiyo kwa weledi wa hali ya juu, bila kuwasahau mikakati mizito ya kulinda matokeo chanya yaliyotokana na utekelezaji wa mipango husika.
Kuonyesha, Lissu kaabika yeye na wale wanaomshabikia katika harakati zake za kutimiza ndoto zake binafsi, ni namna alivyoelezea suala la uchumi. Kwa yeyote anayejielewa, anaweza kukubaliana na mimi kuwa Lissu kushindwa kujadili suala la Uchumi kwa kutumia takwimu. Lissu (ambaye amepona sasa, na Mshukuru Mungu kwa hili ambalo nililiombea ili aje aone jinsi Tanzania inavyipiga hatua kiuchumi na kijamii), ameshindwa kuonyesha udhaifu wa kiuchumi wa nchi yetu anaoufikiria yeye na pia kashindwa kuonyesha kwa namna gani ataboresha uchumi huo wake wa kufikirika kwa kutumia takwimu.
Kwa kipengere hicho tu nasema Lissu amewaabisha mashabiki wake, yeye na chama anachowaza kukitumia kutimiza matakwa yake binafsi.
Yangu ni hayo.