Kimsingi huyu jamaa hana ajenda yeyote.
Lakini ni kuwa ni haki yake kugombea,napenda kumshauri jambo moja kubwa.
Mosi, apunguze ujuaji mwingi usiomsaidia. Mfano,kumkashifu Nyerere bungeni haikuwa good move kwake na wenda ndio ilimgharimu. Ajikite kwenye hoja mbadala na kama hilo kwake litakuwa gumu basi chama chake kihusike kum-brand ajiite sana kujenga hoja mbadala watanzania wamwelewe. Zile tambo za kukashifu watu hasa opponents wake hazitampa credit.
Pili, asiwe too emotional kuelekea azma yake ya kupata kura za watanzania, hana haja sana yeye kama mgombea kuchafua watu na kuponda hasa anapouza ajenda au sera zake. Wawepo wetu wengine kufanya hivyo yeye ajikite katika ajenda na sera,kwa kufanya hivyo atapata uungwaji mkono wa makundi yote na public sympathy na atapata kura.
Tatu, chadema kama wataweza waifanyie review ya ilani yao ya mwaka 2010 ambayo aliitumia Dr. Slaa watoe au waboreshe baadhi ya sera waitumie mwaka huu.
Kila la heri CHADEMA.