Huduma benki ya CRDB ni mbovu sana
Sijajua kama wao wanajua mteja ni mfalme. Ni sawa CRDB wanataka kwenda kidijitali lakini hawaendani na service ku satisfy customer. Haiwezekani mteja anataka kufanya transaction kwa Simbaking lakini anachukua zaidi ya saa 3 kukamilisha huduma.

Hivi hii huduma inarahisha au inachelewesha huduma? Ni Bora tuelekee kwenye benki za kigeni sasa maana watanzania wenzetu mmetuangusha. Mpo faster sana kukata bills kwaajili ya account services lakini kwenye kumuhudumia huyo mteja mmeshindwa.

Naondoka hii benki haifai na sishauri mtu awe mteja benki hii. Ukiendelea just do it at your own risk.
Ondoka tu hatukutaki go f.. yourself Cc ephen_
 
Benki za wazawa Tanzania zinaishi kwa pumzi ya serikali na regulations za BoT.
Sekta ikiamuliwa iwe huria na mazuio yapunguzwe ni benki chache zitasimama. Wana mazoea na kutojituma kwingi.

Kwanza ni benki zote matawi yote yana upungufu wa wafanyakazi, madirisha manne hayawezi kuwa na wahudumu wote hata mara moja, benki zote wafanyakazi wake wanapata overtime. Benki zote ikifika saa kumi jioni wanafunga na kuingiza watu ndani na kuzuia wengine kuhudumiwa eti "muda umeisha".
CRDB Mbezi Luis, Makumbusho, Tabata Bima wote kuna madirisha unakuta yako wazi mpaka unajiuliza labda wameenda lunch
 
N

Nilishaacha manyoya kitambo sana kwenye hiyo bank, waliniibia pesa yangu fln hv, ikabidi niwapigie huduma kwa wateja sababu nilikuwa mbali na bank ilipo

Nilichojibiwa mungu ndiye anajua

Ikanibid niachane nao mazima
Wana huduma mbovu sana kwa wateja
 
Ni heri kwa sasa tutumie benki za nje hawa ABSA nimeambiwa wako vizuri kiasi nitaenda huko. Au niende mkombozi au amana kidogo benki za dini hawana umangi mezani.
Hata Equity wako vizuri... kufungua ACC na kupata kadi same day, tena masaa machache tuu...simbanking pia iko very fast
 
Ukiacha customer service mbovu pia suala la benki kudhamini vitu vingi nalo ni tatizo, wamejitahidi kukusanya volume ya wateja ila suala la kuwahudumia ndio tatizo lilipo. Pia hata ukitaka kupata mkopo inachukua muda mrefu ukilinganisha na benki zingine.
 
Benki hizi zinalindwa sana ,bank za nje zingepewa full support kama bank za ndani mbona wangejirekebisha tu
 
Back
Top Bottom