Huenda Joanfaith John Kataraia is best DED of the history, anajituma sana huyu binti

Kuvalisha ng'ombe hereni siyo mkakati wa mkurugenzi huo. Hili ni agizo la nchi nzima na linafanyika kote!
 
Nilibahatika Siku moja Kukutana nae Kawe akiwa anatokea NIDA na katika Mazungumzo yetu akajitambulisha kuwa ni mwana CCM na yuko UVCCM.

Kusema ukweli kwa Urembo alionao na unaoendana na Uwezo wake mkubwa wa Akili ( Intelligence ) alionao mwanzoni nilitamani Kumtongoza ila nilipoigundua tu IQ yake ilivyo Kubwa nikaufyata na kuwa Mpole kwani nina 'Allergy' ya Kutongoza Wanawake 'Geniuses' kama Yeye ila nawapenda hawa Niliotukuka nao ambao hawana Akili na unawapeleka utakavyo tu.

Na cha Kufurahisha zaidi huyu Dada hajaingia katika Siasa kwa Njaa au kutafuta Hela kwani pia ni Mtoto wa Kishua ( Kitajiri ) kweli kweli. Kwa hizi Sifa ( Kongole ) zote ulizompa nakubaliana nawe 100% na nitoe RAI kwa CCM wamtunze Kimaadili na Kiutendaji, ila siyo 'Kingono' kwani ni Hazina Kubwa mno kwa Uongozi kwa Siku chache zijazo ukizingatia ameanzia Ngazi za chini kabisa ndani ya Chama.
 
Unasema kamaliza tatizo la migogoro ya wakulima na wafugaji??
Umekaa Malinyi muda gani boss!?

Hayo matatizo walioshughulika ni wengine kabisa! Si ajabu yupo primary huko watu wanatafuta ufumbuzi matatizo hayo, operesheni zimepewa kila aina ya majina.
Teamwork ya wengi tena ngazi ya chini, na haijaanzia kwake tu na hayajaisha!
Huyo Joan yupo hapo muda gani!??

Tuache kuvunja watu mioyo watu wanaojitoa kutatua shida za watanzania huko Ulanga kwa kutoa promo kwa watu wasiostahili tafadhali!

Mkoa mzima haaa haaa MAHABA HAYA, binafsi naweza amini SNOW barafu imedondoka Dar, Ila sitoamini hili la Mkoa mzima yeye ndiye Bora! DED anayeshughulika na hereni ng'ombe.
 
Kama mpaka wewe umemkubali, Mimi ni nani?
 
Nimezungumzia ninachokifahamu,
Bosi hebu tuelimishe huu mfumo wa hereni unavyoongeza thamani, na kama tag zinaongeza thamani kwanini halmashauri hazifanyi hivyo au ugumu uko wapi kuweka hiyo system, na vipi nyie wafanayabishara binafsi kwani hamuwezi implement hiyo system bila kusubiri serikali maana inaonekana faida ni kubwa sana au ugumu uko wapi kwa watu binafsi? tuelimishe
 
Utakuwa humfahamu vizuri wewe. Niishie tu hapo na kingine ninachojua kiumri kalingana na Jokate na yupo single kama Jokate.
 
Mfano ni wapi mkuu?
SOMA HII HABARI HAPA CHINI KWA MUJIBU WA MALUNDE 1 BLOG:
Ng'ombe 6270 wametambuliwa kwa njia ya Kuvishwa Hereni za kielektroniki katika kijiji cha Kitosi Wilayani,Nkasi Mkoa wa Rukwa.
Haya yamebainishwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kwenye, Mkutano na wafugaji katika Kijiji cha Kitosi mara baada ya kushiriki katika zoezi la uwekeji herenikatika kijiji hicho.
Waziri Mashimba amesema kuwa zoezi la utambuaji wa Mifugo linatekelezwa nchini kote na kwa sasa tumeanza na mikoa ya Mfano ambayo ni Rukwa ,Katavi , na Kigoma.
Amesema zoezi hili limeanza Katika kijiji cha Kitosi Wilaya ya Nkasi na tangu zoezi hili limeanza zaidi ya ng'ombe 6270 tayari wameisha tambuliwa kwa kuvishwa hereni katika kiji hicho.
Amesema zoezi hili nimuhimu kwa kuwa linaongeza thamani ya Mifugo ya wafugaji katika Masoko na kusaidia kufuatilia ubora wa mazao yanayo zalishwa na Mifugo iliyotambuliwa kwa njia ya hereni
 
Mashindano
 
Kwa hoja zako ni dhahiri hujawahi kufanya biashara ya kuuza ng'ombe nje ya nchi....sekta ya mifugo nchini inahitaji mageuzi makubwa na sio eartag ili kufikia walipo wenzetu kama Botswana.
 

Hapana, kaelezea anayoyafanya DED ikiwamo kuongeza thamani ya mifugo kupitia hereni. Tabu watu wengi wanauzia soko la ndani hivyo hawakuwa wanajua hili kama lipo considered kimataifa thus why ikageuza mwelekeo wa topic.
 
Kwa hoja zako ni dhahiri hujawahi kufanya biashara ya kuuza ng'ombe nje ya nchi....sekta ya mifugo nchini inahitaji mageuzi makubwa na sio eartag ili kufikia walipo wenzetu kama Botswana.
Ungefafanua ili nasisi tunufaike na uzoefu wako,
 
Hapana, kaelezea anayoyafanya DED ikiwamo kuongeza thamani ya mifugo kupitia hereni. Tabu watu wengi wanauzia soko la ndani hivyo hawakuwa wanajua hili kama lipo considered kimataifa thus why ikageuza mwelekeo wa topic.
Uko sahihi 100%√
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…