Huenda kuna waislam wengi duniani wameshazikwa wakiwa hai

Na cha kushangaza huyu anayecheleweshwa kuzikwa sio kwamba kawekwa sehemu anapewa huduma ili azinduke bali yupo kwenye friji..sasa sijui atazindukaje wakat yupo kwenye friji
Hakuna kupona hapo.
 
Hao munaowaweka nyinyi wiki,mwezi au miezi wamezirejea duniani? Kwanza kaa ukijua Muislamu akifa anaoshwa sasa katika kuoshwa kuna kusafishwa uchafu tumboni endapo mtu hajafa huo uchafu hautotoka mna misuli itakua haijaregea

Msipende kujadili mambo ambayo hamna elimu nayo mtu ikishathibitika kafa azikwe tuu mana hana lake hapa duniani ata mkikaa nae miezi mtagharamika nyinyi kwa kumtunza kila siku.

Mnawekana miezi ,wiki full gharama za kutunza maiti si bora mungetumia kwenye mambo ya maendeleo gharama zote hizo

Nb.Uislamu ni dini ya haki hata wakichukia wanaochukia lkn ukweli utabaki kua kweli diku zote
 
Umemaliza mjadala.
 
Huo utaratibu wa kuchelewa kuzika si mzuri kabisa
 

Cha ajabu anavunda na kunuka bado kumbe wanasubiri aamke really?

Huwa nauliza wanahangaika nini
Hata mende tunajua kafa na kumfagia
 
Haya mambo hutokea kwa dini zote
Isipokuwa kwenye uislam kuna kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kutokea kwasababu ya muda wa kuzika

Nilikuaga na demu wangu wa kiislam, siku moja ghafla tu mida saa 4 akaanguka wakaitwa wazee wakam check pale wakasema tayari amekufa
Ikatokea sintofahamu pale apelekwe hospital kwa vipimo zaidi lakini kufika saa 7 mchana nadhani, tukawa tumeisha mbebesha tani za kutosha za mchanga kaburini
Hadi leo hii huwa naamini yule bint labda tulimuwahisha aisee

Huko vijijini hospitali zilipo mbali wanazikana sana hai bila kujua
 
Mkuu kumkamua mtu kinyesi na kikatoka sio uthibitisho wa mtu kufa kisayansi
 
Da pole sana,nadhani huo mfano wako umefunga mjadala,bila kujali dini mtu akianguka apelekwe hospitali kwanza daktari athibitishe kifo,kuwaamini sana hawa wazee wetu walah tunazkwa sana tungali hai
 
Mm nipo kiimani zaidi kwaio kma unaamini sayansi mm naamini Imani zaidi
Lakini mkuu ni wewe ndio umesema hivyo kutetea hoja yako
Vitabu havijasema kama akitoka uchafu maana yake ndio uthibitisho wa kifo
Vitabu vinasema mtu akifa kabla hajazikwa asafishwe
 
Lakini mkuu ni wewe ndio umesema hivyo kutetea hoja yako
Vitabu havijasema kama akitoka uchafu maana yake ndio uthibitisho wa kifo
Vitabu vinasema mtu akifa kabla hajazikwa asafishwe
Ww ni mkristo au Muislamu?
 
Kabisa hilo nakubaliana na wewe

Tena kwa africa ndio usiseme tumezika wagonjwa wengi sana waliozimia

Taarifa ya mtu kufa inatangazwa asubuhi kua mgonjwa amekufa alfajiri halafu saa 7 mchana watu wanapanga reli
Hapa cha kujiuliza, kwa wasio kuwa na utaratibu wa kiislamu, yamesha ripotiwa matukio mangapi, ya watu waliotangazwa kufariki na baada ya siku kadhaa, akamka tena.
 
Kuna jamaa kitunda alikuwa fundi umeme kafa saa sita mchana jion saa kumi tukamzika ananiuma nadhan kama alizimia hivi dah
 
Na kuna story Pale Lugalo kuna askari ailuguzwa muda mrefu tena alikua na cheo ,lakini palikuwepo doctor aliyefahamu vizuri tatizo la huyo mgonjwa..ikatokea akazidiwa siku moja madocta wakahangaika lakini wakashindwa hatimaye akaaga dunia ...walivyokua wanapanga mpango wa kumpeleka mochwari yule doctor aliyekua anafahamu vizuri shida ya yule mgonjwa akafika akasikitika sana akawaomba mwili akaenda chumba maalum akajifungia nae akaanza kuhangaika na ma vifaa, oksijeni na kila namna alivyoweza...baada ya masaa kadhaa moyo ukaanza kufanya kazi...baada ya masaa kupita akapiga chafya...nasikia ikaenda hadi akafumbua macho akaanza ongea...yule askari alipona kabisa...jamaa(doctor)alipata sifa nyingi ikiambatana na na cheo...
(Chanzo story ni dada mmoja aliyeishi pale lugalo barracks miaka hiyo)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…