Hapa cha muhim sio kuwai kuzika wala kuchelewa kuzika, issue ni kuboresha huduma za afya mda mwingne moyo kusimama sio kufa. Maana mnaweza zika mtu mzima kwa haraka ama mkamuua mtu pamoja na kuchelewa kuzika pia.
Kuna shoga yangu nahisi walimuwahisha mochwari, alikuwa anaumwa kidogo tu anatapika, usiku akazidiwa akiwa kwa mama yake, akawa anashindwa kulala kitandani wakamshushia godoro chini, mama yupo anasali huku anampigia mme wake ambae yupo ubungo na wengine.
Mama huku anampigia dereva aje wamuwahishe hospital, dereva yuko club hapokea hata simu, mama anampigia jirani ambae hupo hapa hapo masaki awahishe gari, mama hawezi endesha ni mzee, wakati mama anafanya mawasiliano dada wa kazi kamshikilia shoga yangu, na alivyokuwa kibonge, pande la mdada mmmh ,mara akamuomba dada wakazi maji, dada wa kazi kumpa maji meno yameishashikana, mara dada wa kazi akasikia shoga yangu kapumua kwa nguvu saana hakupumua tena akaona mikono imelegea na kijitupa pembeni.
Upimaji wa kibongo ni kubinus jicho na kushika mspigo ya mikono na kugusa kifuani kamaliza.
Fasta wote walopigiwa simu walifika kwa pamoja wanakuta mtu hajitikisi tena, beba hivyo hivyo hospital, wakasema ashakufa na muda huo huo kawekwa mochwari.
Wasiwasi wangu ni alivyokuwa kibonge na pressure alokuwa nayo wenda alikuwa hajafa sana, barafu ikammalizia.