Huenda kuna waislam wengi duniani wameshazikwa wakiwa hai

Huenda kuna waislam wengi duniani wameshazikwa wakiwa hai

Ona sasa baba ya GSM kafa asubuhi saa kumi yupo mavumbini.hivi mzee wa vile si alikuwa labda ka moyo kanadunda kwa ndani?

Kingine ni hizi mochwari, mtu eti kafia wodi nusu saa nyingi washamuingiza kwenye ile barafu unategemea nini?

Watu wengi hawajui hata ile ya kumpampu mgonjwa kwenye moyo kwa kutumia mikono, hiyo nao inasaidia kumstua mtu kama hajafa sana.
CPR
 
Ni utaratibu mzuri sana wa kuwahi kuzikana, ukikata moto asubuhi mchana tunazika

Ila nina hakika kuna watu wengi wameshazikwa Ili hali wakiwa wamezimia au wakiwa kwenye coma, hasa vijijini pasipo na hospitali na daktari wa kuthibitisha kifo.

Kuchelewa kuzika ni mbaya ila ina faida zake, maiti inaeza kupiga chafya. Mwaka 2012 mchezaji Fabrice muamba wa bolton wakicheza dhidi ya spurs alianguka uanjani na moyo wake ulisimama kwa dakika 78.

Referee howard webb aliahirisha mechi huku machozi yakimtoka, uwanja mzima ni huzuni madaktari wa kizungu na kudra za Mungu jamaa akaamka bwana na kustaafu mpira rasmi.

Angekuwa Afrika tungeshamsahau na mke wake angekuwa single mother tayari, ila jamaa anakula bata tu.

Hii ni kweli kabisa mtaani kwetu Bibi mmoja wa kisomali alipata ajali saa 10 jioni saa 1 usiku kazikwa na tochi.
 
Dah inaonekana kifo kinavyoogopewa
 
Mleta Uzi anaogopa kufa
Kufa ni kufa mungu ndio mjuaji zaidi we fuata maelekezo yake yeye ndio mjuaji zaidi.

Pale ulipokuwa mdogo unaambiwa na mzazi wako nenda shule ulikuwa unaona mateso sasa ona shule ilivyokusaidia na wewe unaandika vizuri tu
 
Ni utaratibu mzuri sana wa kuwahi kuzikana, ukikata moto asubuhi mchana tunazika

Ila nina hakika kuna watu wengi wameshazikwa Ili hali wakiwa wamezimia au wakiwa kwenye coma, hasa vijijini pasipo na hospitali na daktari wa kuthibitisha kifo.

Kuchelewa kuzika ni mbaya ila ina faida zake, maiti inaeza kupiga chafya. Mwaka 2012 mchezaji Fabrice muamba wa bolton wakicheza dhidi ya spurs alianguka uanjani na moyo wake ulisimama kwa dakika 78.

Referee howard webb aliahirisha mechi huku machozi yakimtoka, uwanja mzima ni huzuni madaktari wa kizungu na kudra za Mungu jamaa akaamka bwana na kustaafu mpira rasmi.

Angekuwa Afrika tungeshamsahau na mke wake angekuwa single mother tayari, ila jamaa anakula bata tu.
Mkuu kuna vitu vingi sana hujui kwenye mazishi ya waislamu, achana navyo, wenyewe watakupiga mawe.
 
Nadhani waislam wana vitu vya kuangalia (according to mafundisho) ili kuthibitisha kua mtu kafariki. Moja wapo ya hivyo vitu ni kwamba ukifungua jicho la mtu ambaye unadhani kafariki then ukajiona kwenye kiini cha jicho jua hajafa, ukiona kiini cha jicho hakioneshi image yako jua kasha rest in peace na anatakiwa akapumzike kwenye nyumba yake mapema sana.
Mmh kumbe, ukiona kwenye jicho la mtu lazima ujiangalie ? Ni kama kioo? Embu nifatilie hii
 
Mzee abdallah alizimia siku 3 ...ustadh mmoja akaamuru mzee atolewe kitandani aoshwe na aswaliwe sala ya mayyit....wakati tunampeleka mzee abdallah kumzika akiwa ndani ya jeneza si akakohoa na kupiga chafya..aisee watu tulipoteana kwa kukimbia tukamuacha mzee abdallah ndani ya janayza....
Ikawaje sasa baadae?
 
Hivi madaktari huwa wanafanya juhudi za kumuookoa yule ambaye wanaona ameshakufa? Au mimi ndio sijakuelewa?

Kwani kifo huthibitishwa vipi?

Na kwa pointi yako inamaana juhudi zifanyike hata kwa yule ambaye tunaona ameshakufa, hiyo maana yake hatuwezi kuthibitisha kifo.
Kama hujaelewa,subiri uzimie saa 2,unathibishwa umekufa. Saa 7 unapelekwa kuzikwa unazindukia njiani. Utaleta mrejesho
 
Mbaya zaidi wakati wanajadiliana 'huyu tayari, saa tisa alasiri tumpige chepe' wewe unawasikia ila huna cha kufanya 😎😎😎
natikisa hata mguu 😂😂😂😂.lakini pia unakuta labda mgonjwa hajiwezi hata kugeuza jicho anawasikia kwa mbaliii mipango ya mazishi akiwaza na shida zote alizowahi zipitia anajisemea moyoni wacha wanizike tu.
 
Ni utaratibu mzuri sana wa kuwahi kuzikana, ukikata moto asubuhi mchana tunazika

Ila nina hakika kuna watu wengi wameshazikwa Ili hali wakiwa wamezimia au wakiwa kwenye coma, hasa vijijini pasipo na hospitali na daktari wa kuthibitisha kifo.

Kuchelewa kuzika ni mbaya ila ina faida zake, maiti inaeza kupiga chafya. Mwaka 2012 mchezaji Fabrice muamba wa bolton wakicheza dhidi ya spurs alianguka uanjani na moyo wake ulisimama kwa dakika 78.

Referee howard webb aliahirisha mechi huku machozi yakimtoka, uwanja mzima ni huzuni madaktari wa kizungu na kudra za Mungu jamaa akaamka bwana na kustaafu mpira rasmi.

Angekuwa Afrika tungeshamsahau na mke wake angekuwa single mother tayari, ila jamaa anakula bata tu.
Sio kweli,umedanganywa na aliyeakuambia.Hakuna Muislamu anayefariki bila kuitwa daktari,kuthibitisha kifo,hata akifia nyumbani,lazima ataitwa Daktari athibitishe,kama kaanguka ghafla lazima atapelekwa hospital,kule ndio wanaambiwa na Doctor huyu ameshafariki.Kunapatikana ushahidi wa kupata karatasi,itakayopelekwa kwenye usajili wa vifo na vizazi,ili kupata cheti cha kifo.
Mara nyingi kwenye vijiwe vya Pombe za kienyeji huwa mnadanganywa,mambo mengi kuhusu uislamu.Ni dini pekee duniani,kiongozi wake ,amehimiza kujitibu,kwenda hospital,kutafuta matibabu,kwa kuandikwa katika vitabu vya dini ya kiislamu kwa ushahidi wa Maandishi.Pia ni dini pekee,duniani inayohimiza kutafuta elimu,popote na ya aina yoyote.
 
ACHA KUIZUNGUMZIA DINI YA HAKI WEWEEEE

Maamuma watakushambulia hadi ukome
Mkikaa kwenye vijiwe vya Pombe za kienyeji,huwa mnadanganywa mengi kuhusu uislamu.Hakuna Muislamu,anayefariki,asiitwe Doctor,kuthibitisha kifo chake.Na nchi zote za kiislamu,hairuhusiwi kuzika,bila karatasi ya uthibitisho wa Daktari.Ndio ukaona pia waislamu wana TBS,zao,Inaitwa HALAL.
 
Kama hujaelewa,subiri uzimie saa 2,unathibishwa umekufa. Saa 7 unapelekwa kuzikwa unazindukia njiani. Utaleta mrejesho
Kwani unawezaje kumtofautisha aliyekufa na aliyezimia?
 
Hii ni kweli kabisa mtaani kwetu Bibi mmoja wa kisomali alipata ajali saa 10 jioni saa 1 usiku kazikwa na tochi.
Ujuwe hapo Doctor,ameshathibitisha kama ameshafariki.Hakuna kifo cha ajali,ila Daktari atathibitisha,kifo au vifo.
 
Hapa cha muhim sio kuwai kuzika wala kuchelewa kuzika, issue ni kuboresha huduma za afya mda mwingne moyo kusimama sio kufa. Maana mnaweza zika mtu mzima kwa haraka ama mkamuua mtu pamoja na kuchelewa kuzika pia.
Kuna shoga yangu nahisi walimuwahisha mochwari, alikuwa anaumwa kidogo tu anatapika, usiku akazidiwa akiwa kwa mama yake, akawa anashindwa kulala kitandani wakamshushia godoro chini, mama yupo anasali huku anampigia mme wake ambae yupo ubungo na wengine.

Mama huku anampigia dereva aje wamuwahishe hospital, dereva yuko club hapokea hata simu, mama anampigia jirani ambae hupo hapa hapo masaki awahishe gari, mama hawezi endesha ni mzee, wakati mama anafanya mawasiliano dada wa kazi kamshikilia shoga yangu, na alivyokuwa kibonge, pande la mdada mmmh ,mara akamuomba dada wakazi maji, dada wa kazi kumpa maji meno yameishashikana, mara dada wa kazi akasikia shoga yangu kapumua kwa nguvu saana hakupumua tena akaona mikono imelegea na kijitupa pembeni.

Upimaji wa kibongo ni kubinus jicho na kushika mspigo ya mikono na kugusa kifuani kamaliza.

Fasta wote walopigiwa simu walifika kwa pamoja wanakuta mtu hajitikisi tena, beba hivyo hivyo hospital, wakasema ashakufa na muda huo huo kawekwa mochwari.

Wasiwasi wangu ni alivyokuwa kibonge na pressure alokuwa nayo wenda alikuwa hajafa sana, barafu ikammalizia.
 
Upo sahihi kabisa,nimekua nikiwaza hivyo.

Mfano nilishuhudia Muscat mshkaji wetu alipata ajali asubuhi saa 3...kufikia saa 11 jioni watu walikua wanafungua turubai pale kwao,yaani ni kwamba shughuli ilishaisha..watu washazika na wameshatawanyika..!

Saa 12 jioni siku hiyo unapita pale kwao nje maisha yanaendelea utadhania hakuna kilichotokea!
Hakuna Muislamu anayefariki bila uthibitisho wa daktari.Huko Oman ndio kabisa,katika mambo ya mazishi na makaburi yana wizara ya serekali,inayoshughulikia,huwezi kumzika mtu,bila cheti cha uthibitisho wa daktari,kwa maelezo ya kina,kafa na nini,kifo chake kumesababishwa na nini,ameumwa,ajali,ameuliwa,ameanguka kwa presha,moyo,sukari nk.
 
Back
Top Bottom