Huenda kuna waislam wengi duniani wameshazikwa wakiwa hai

Huenda kuna waislam wengi duniani wameshazikwa wakiwa hai

Ni utaratibu mzuri sana wa kuwahi kuzikana, ukikata moto asubuhi mchana tunazika

Ila nina hakika kuna watu wengi wameshazikwa Ili hali wakiwa wamezimia au wakiwa kwenye coma, hasa vijijini pasipo na hospitali na daktari wa kuthibitisha kifo.

Kuchelewa kuzika ni mbaya ila ina faida zake, maiti inaeza kupiga chafya. Mwaka 2012 mchezaji Fabrice muamba wa bolton wakicheza dhidi ya spurs alianguka uanjani na moyo wake ulisimama kwa dakika 78.

Referee howard webb aliahirisha mechi huku machozi yakimtoka, uwanja mzima ni huzuni madaktari wa kizungu na kudra za Mungu jamaa akaamka bwana na kustaafu mpira rasmi.

Angekuwa Afrika tungeshamsahau na mke wake angekuwa single mother tayari, ila jamaa anakula bata tu.
[emoji28]
 
Kabisa hilo nakubaliana na wewe

Tena kwa africa ndio usiseme tumezika wagonjwa wengi sana waliozimia

Taarifa ya mtu kufa inatangazwa asubuhi kua mgonjwa amekufa alfajiri halafu saa 7 mchana watu wanapanga reli
We toka asubuhi mpaka saa saba kama hajapiga chafya tuanze kuchezea madhambi ya makusudi?
 
Kuna jamaa alikata moto wakapeleka mochwari wakati wanadubiri doctor aje athibitishe kifo ili wamuweke kwrnye friji ile baridi ya kule jamaa akafumbua macho
Hii imetokea sana...
sometimes huwa nawaza mama yangu mzazi nae lengine pale kairuki walimuwahisha kwenye jokofu...
 
Hii imetokea sana...
sometimes huwa nawaza mama yangu mzazi nae lengine pale kairuki walimuwahisha kwenye jokofu...
Pole sana mkuu kama alifia hospitali walimpima kwanza kabla ya kumuweka kwenye jokofu so relax
 
Waislam ni dini ya wajanja wajanja ndo maana dua ya chakula wameaeka fupi utisikia BISMILAH
ha ha ha ha ha sala ya kuufinyia ubeche alafu wanapenda wali mweupe kuliko pilau ili wale mwingi kila tonge wanafinya na nyama
 
Sisi tunawaamini Madokta wetu wakisema kafariki hatucheleweshi, ila sasa ni kushauri watu wawe wanazikwa na simu zao akishtuta anatwanga tunamfukua.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kumbe mlimzungusha yule mzee Tanzania nzima mkitegemea atanyanyuka?
Sasa nimeelewa sababu za kuweka maiti zaidi ya wiki
Huwa mnasubiri wapendwa waamke

Ila hakuna takwimu zenu pia ambazo mlitangaza kifo cha fulani halafu baada ya siku kadhaa akaamka

Walahi kama kuna ushuhuda huo mlimvundika mtu wiki mbili na akaamka basi nitaamini nyie ni wajanja sana
 
hili linaniwazisha sana.......kunamchungaji mmoja alisema ukifariki ndio muda uliopangwa na muumba...wa kurudi kwake...
sasa kama kuna watu wanawaishwa inaonesha mungu hana uhusiano wowote na kufariki kwetu
labda tupambane na sayansi yetu itufanye immortal
 
Muhimu watu wazikwe na simu zao zikiwa full charge na kifurushi kama alizimia akazinduka anapiga simu, afukuliwe
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ona sasa baba ya GSM kafa asubuhi saa kumi yupo mavumbini.hivi mzee wa vile si alikuwa labda ka moyo kanadunda kwa ndani?

Kingine ni hizi mochwari, mtu eti kafia wodi nusu saa nyingi washamuingiza kwenye ile barafu unategemea nini?

Watu wengi hawajui hata ile ya kumpampu mgonjwa kwenye moyo kwa kutumia mikono, hiyo nao inasaidia kumstua mtu kama hajafa sana.
 
Back
Top Bottom