Huko Vijijini unakosema,kuna watu wataalamu,na hawakusomea mambo ya afya,lakini wamerithi kutoka mababu na mababu,kuanzia kutibu,dawa,uuguzaji,ukunga wa jadi,hao watu wakiwa ni dini tofauti.Tanzania bara hakuna familia ya kiislamu,isiyohusiana na ukristo,Mpaka waarabu wapo wenye ndugu ni wakristo,wenyeji.
Ukiangalia kwenye ukunga,wapo wakunga wa jadi,ambao wanazalisha wanawake Vijijini Bila kujali ni wa dini gani,na wakunga walikuwako toka enzi za mabibi na mababu.Na ndio hivyo hivyo wataalamu,wanaojuwa kama mtu amefariki au bado,bila kujali,anayepima ni wa dini gani na anayepimwa ni wa dini gani.