Polepole Humphrey kumbe naye anaamini kuwa rasilimali za nchi lazima zilete Maendeleo ya Watu .
Parallel State iliyoongozwa na watu dizaini ya watu kama kina Gwaji , Ole Sabaya , Mayanga Construction company , wateuliwa wa awamu ya 5 ndiyo ilikuwa wanufaika na nafasi yao ya kimkakati ilipotea na walilia sana kulipotokea msiba wa kiongozi aliyekuwa anaendesha serikali na parallel state ya watu 'wasiojulikana' .
Ujenzi wa reli ya SGR usiokuwa na manufaa, wakati reli ya mkoloni ipo ikikarabatiwa sehemu korofi ingefaa na kufanya kazi ya ileile usafirishaji ni mkakati wa parallel state kujinufaisha kwa kutaka kupeleka madini na makinikia pwani ya bahari , mbali ya kuingiza nchi katika hasara kubwa kupitia mradi huu usio na tija ya reli ya SGR genge hili la watu waliokuwa karibu na uongozi walifaidika na wanaendelea kujinufaisha. Polepole anadai kuna kiongozi hivi karibuni amepambana kama Mwalimu Julius Nyerere alivyopambana wakati wake kwa serikali kuhodhi mashirika ya huduma za jamii n.k
Polepole Humphrey anasema asingependa kusema sana kwa sababu yeye pia Humphrey ni bado sehemu ya uongozi.
Nguvu za 'kibeberu' anazosema Polepole ni kwa kuwepo chama cha CCM , utulivu siyo amani, uongozi wa kimabavu n.k pia unawezesha mazingira ya uporaji wa madini, kuwepo mikataba mibovu ya siri, Bunge la uchama kimoja lisilo na meno ya kuhoji serikali, kuhoji mikataba ya madini / SGR reli/ Ndege za cash n.k
Yanayoendelea huko DR Congo, Humphrey Polepole anasema ni sawa na yanayoendelea Tanzania ila katika hali tofauti yaani Congo wanapambana kugombania ulaji kwa kutumia silaha na vita huku Tanzania wanatumia kuunda Bunge la chama kimoja, vitisho kwa kukamata na kusweka watu dani, kukaba demokrasia na kuzuia Maendeleo ya Watu kwa kakikundi kidogo cha wanaCCM kujinufaisha na kujimilikisha keki ya taifa.