Humphrey Polepole: Mambo ya machifu hayana msaada kwa taifa, yanaweza kuleta ukabila na mgawanyiko, yanapaswa kupingwa

Ukabila pia ujue hautambuliki kiserkali ila upo! Endelea kuunga mkono wewe unadhani kama vikabila vidogo hapa Tanzania si vitabaguliwa sana maana makabila makubwa yatahodhi ajira na nafasi nyeti kwa kubebana!
Makabila yanatambulika ila ukabila ndio unapigwa vita..

Machifu wanatambulika kwenye jamii kama nilivyoyaja hapo juu ila hauko kwenye mfumo rasmi wa uongozi.

Sasa kuna shida gani hapo? Aukwa vile msiyempenda Kaja 😃😃😃

 
machifu si ndo hao hao walioshirikiana na wakoloni kuzinyonya nchi za kiafrika kwa leo bado tunataka kurudi kwenye uchifu ili utusaidie nn.wenzetu wanakimbizana na mifumo ya kisasa ambayo pia ni ya kinyonyani ss tunawaza machifu.tujikite kwenye sayansi na teknolojia yake ili taifa liondokane na unyonyaji wa mifumo kutoka nje.machifu hawana tija,tuna mambo mengi ya kitaifa tunatakiwa kuyajadili ili tutoke hapa tulipo na tusonge mbele.tuachane na hizi minor issues.tuna mambo lukuki ya kujadiliwa kwa sasa lkn machifu si kipaumbele cha taifa letu.
 
Hata mimi naamini Magufuli alikuwa anatania tu! Kuhusu miradi wakati wa Magufuli kila kona ya nchi kama ni hospital zilijengwa kama madaraja walijengwa na mpaka jana Tanzanit imefunguliwa! Pia upande wa kaskazini mwa nchi yetu wanajengewa daraja pale mto wami!
 
Hii myth ndio inajengwa sasa hivi kuhusu uislamu na Zanzibar usipofuatilia vizuri unaweza kuamini.
 
Tatizo nadhani tunaongelea Polepole Kasema na sio Kilichosemwa...., nadhani tukijikita kwenye nini kimesemwa na sio nani kasema tunaweza kuwa na mijadala yenye afya zaidi...

Nacho ni Pro and Cons za kuuutambua Uchifu kwenye Uongozi wa nchi..., sasa tunautambua vipi kama symbolically kila mtu akienda kwao na atambikie anavyotaka, au tunauweka rasmi kwamba wanapewa ruzuku ili kuendesha mambo yao; Au tunaanza kuwapa madaraka kwa kofia za uchifu wao..., au kila nikienda sehemu kufanya shughuli zangu lazima nione uongozi wa machifu wanipe baraka ?

Kwa haraka haraka karne hii sioni tija ya kuutukuza ingawa kila mtu kwa wakati wake anaweza aka-perform their cultural rituals (no need kama taifa / au wasiohusika kuhusishwa)
 
Hatuhitaji kuwatambua machifu kwa sababu hakuna sababu hawana msaada wala mchango wowote katika maendeleo yetu. Kabila ni sehemu ya utambulisho wa mtu
 
Hivi Tanzania mtu pekee aliyekuwa na akili timamu ni mwalimu pekee?
Waliobaki wenye akili Humprey Polepole na Spika mstaafu Job Yustino Ndugai.

Mwalimu alishasahaulika tangu zama hizo. Mambo ya mwalimu siyo relevant kwa kizazi cha leo.
 
Shaka Hamdu(kutwa kusifia) naye atakua kama huyu(kutwa kukandia) siku akinyofolewa siyo
 
Hatuhitaji kuwatambua machifu kwa sababu hakuna sababu hawana msaada wala mchango wowote katika maendeleo yetu. Kabila ni sehemu ya utambulisho wa mtu
Wanatambulika kwenye jamii na sio kwenye mfumo rasmi wa kiungozo.

Sasa sijui nani kakwambia anataka kuwaingiza kwenye mfumo wa serikali naona unabwata.
 
Wanatambulika kwenye jamii na sio kwenye mfumo rasmi wa kiungozo.

Sasa sijui nani kakwambia anataka kuwaingiza kwenye mfumo wa serikali naona unabwata.
Wana mchango gani wa maana katika hizo jamii wanazotambulia?
 
Hilo ndilo tatizo kubwa, badala ya kujadili hoja watu wanaanza kumjadili mleta hoja. Kuna baadhi ya watu wala hata hawaeleweki wanataka nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…