Humphrey Polepole: Mambo ya machifu hayana msaada kwa taifa, yanaweza kuleta ukabila na mgawanyiko, yanapaswa kupingwa

Wewe sio Mpuuzi ila hujui ukiacha Jafu niliemsahau ila wengine hao hawakuwa kwny Cabinet ila utabisha kwa kuwa hujui Naibu sio Member wa Cabinet nami niliongelea Cabinet kwa makusudi kwa kuwa nilijua kama Ww mpo wengi mtaokuja na hao Manaibu
Kwa hiyo ndo maana hiyo bibi yenu ndo kaamua kutoa mawaziri wore wakiristo kama Medard Kalemani,faustine Ndugulile,Paragamba Kabudi,William Lukuvi akaweka waislamu vilaza kama Makamba!
 
Tatizo lako ni ufinyu wa ufahamu

Yaani unataka kufananisha Population ya Waislam kwa kulinganisha na Wasukuma bila ya kujua kuwa kuna Wasukuma ambao ni Waislam, hoja ni kuwa wakati wa Magufuli Wateule wengi sana walitokea Usukumani na mtazamo wa kikabila ulikiwepo sana
Huenda kweli nina ufinyu wa ufahamu!

Asante kwa hilo!

Haya nitajie hao wasukuma 10 kwenye cabinet ya magufuli

Usiseme tu wasukuma walikua wengi, wataje!
 
Hua nashangaa sana wao muona kama malaika kwanza sera zake za ujamaa zimeharibu sana hili taifa kutuletea katiba ya hovyo iliyozaa wanafiki na kujipendekeza iliyoleta mzigo katika nchi uliona wapi muungano wa serikali 2 moja ikiwa kupe.

Kimsingi alifanya mazuri ila kuna mengi pia alifeli sana.

Ndio maana aliacha nchi ipo hohehahe.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Kaharibu hii nchi kwa zaidi ya 90%
 
Huenda kweli nina ufinyu wa ufahamu!

Asante kwa hilo!

Haya nitajie hao wasukuma 10 kwenye cabinet ya magufuli

Usiseme tu wasukuma walikua wengi, wataje!
Huyo Pimbi hatakwambia kitu maana anachuki na wasukuma! Hana cha kuwafanya na wanamzidi kila kitu!
 
Humphrey Polepole amesema kuwa

"Mambo ya Machifu yanatusaidia nini kama taifa?nasema jambo hili sio jema,naliona linadhoofisha Utanzania wetu,likiendelea bila kukemewa litaibua tuliyoyazika ya hisia za ukabila, usisi na uwao, Mwalimu Nyerere aliona mbali kukataa haya mambo kwani yataligawa taifa"

"Yapo maeneo uchifu ulishaondoka,haupo. Tulishakubaliana uchifu ni ukoo wenu, mna kiongozi wa ukoo mnazungumza mambo yenu binafsi ya kifamilia leo serikali ikizungumzia uchifu hawa nao wataomba kiongozi wao (wa ukoo) atambulike na apate nafasi huko serikalini"

"Mwalimu Nyerere alikataa jambo hili (uchifu), lina faida gani. Uchifu unataka kutuibulia zile hisia kwamba tuna ukabila kama hakuna wazee wataliona hili jambo, basi mawe yataona"

"Nchi yetu ina wakristo na waislamu, ikitokea mvua imechelewa kiongozi wa serikali huwa anawaomba wakristo kanisani wakaombe na waislamu msikitini wakaombe mvue zinyeshe, lakini huwezi kusikia kiongozi wa serikali akiwaomba washirikina eti wafanye namna mvua inyeshe"

"Kwenye shughuli za serikali ushawahi kuona tunawaita wanaoabudu miti waje kuomba kabla ya shughuli? sasa uchifu wa nini?. Hawa machifu walishafutwa kisheria, tunapowarudisha tunapanda nini?"

"Nenda pale Kilimanjaro, utasema Mareale ndio chifu wao, hapana wako wengi. Kwa hiyo nao wafanye uchaguzi kisha waje kumpata chifu wao wa wote. Kweli tunaenda hivi katika maendeleo"

View attachment 2104792
Alipokuwa anafanya hayati haikua vibaya. Polepole bado hajakubali yaishe.
 
Polepole ana hoja nzuri, ila mnakosea mnapomtetea Magufuli, si ndio alikuwa akipiga kampeni kwa kilugha chao? Si ndio alikuwa akifanya ziara na mawaziri akifika jimboni kwa waziri anamuambia aongee kilugha na wananchi?
Si ndio alikuwa akitaja makabila ya wateuliwa Ikulu alipokuwa akiwaapisha?

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Sijamtetea magufuli, labda kama hujanisoma vizuri!

Hivi mbunge wa kisarawe kuongea kizaramo na wananchi wa kisarawe ni ukabila?
 
Mkwere
Huyo Pimbi hatakwambia kitu maana anachuki na wasukuma! Hana cha kuwafanya na wanamzidi kila kitu!
Mie Mke wangu mdogo Msukuma na ninampenda sana

Mie jitu likiwa Jinga jinga nalichukia hata kama litakuwa Mkwere
 
Humphrey Polepole amesema kuwa

"Mambo ya Machifu yanatusaidia nini kama taifa?nasema jambo hili sio jema,naliona linadhoofisha Utanzania wetu,likiendelea bila kukemewa litaibua tuliyoyazika ya hisia za ukabila, usisi na uwao, Mwalimu Nyerere aliona mbali kukataa haya mambo kwani yataligawa taifa"

"Yapo maeneo uchifu ulishaondoka,haupo. Tulishakubaliana uchifu ni ukoo wenu, mna kiongozi wa ukoo mnazungumza mambo yenu binafsi ya kifamilia leo serikali ikizungumzia uchifu hawa nao wataomba kiongozi wao (wa ukoo) atambulike na apate nafasi huko serikalini"

"Mwalimu Nyerere alikataa jambo hili (uchifu), lina faida gani. Uchifu unataka kutuibulia zile hisia kwamba tuna ukabila kama hakuna wazee wataliona hili jambo, basi mawe yataona"

"Nchi yetu ina wakristo na waislamu, ikitokea mvua imechelewa kiongozi wa serikali huwa anawaomba wakristo kanisani wakaombe na waislamu msikitini wakaombe mvue zinyeshe, lakini huwezi kusikia kiongozi wa serikali akiwaomba washirikina eti wafanye namna mvua inyeshe"

"Kwenye shughuli za serikali ushawahi kuona tunawaita wanaoabudu miti waje kuomba kabla ya shughuli? sasa uchifu wa nini?. Hawa machifu walishafutwa kisheria, tunapowarudisha tunapanda nini?"

"Nenda pale Kilimanjaro, utasema Mareale ndio chifu wao, hapana wako wengi. Kwa hiyo nao wafanye uchaguzi kisha waje kumpata chifu wao wa wote. Kweli tunaenda hivi katika maendeleo"

View attachment 2104792
Polepole Wa sasa Ni yule Wa katiba ambaye Ni tofauti Na Wa katiba mpya, simkubali jamaa Ila alichoongea kinaukweli, naona members wengi mnamjadili mtu badala ya hoja yake.
 
Hivi Tanzania mtu pekee aliyekuwa na akili timamu ni mwalimu pekee?
Kwa kweli, Ibaki hivyo tu ,, hawa MaCCM yaliobaki yote akili zao hazina akili, wanapuyanga tu kama kuku aliekatwa kichwa.
 
Polepole wewe humjui! Ni mtu anayeongea ukweli! Issue ya mapungufu yake muachane nazo! Kaongea kweli uchifu ni ujinga wa hali ya juu sana
Hakuna lolote ni hasira tu za kukosa madaraka makubwa ndani ya chama na serikalini,inamaana wakati wa Magufuli kulikuwa hakuna kasoro yoyote? Mbona hatujasikia kelele kelele zake.
Sasa wewe ndio inaonekana humjui yule ni njaa ya madaraka ndicho kinachomsumbua.
 
Yaani huwa sielewi wanaomsifu kumbe kaacha nyumba za tembe tupu
Nyerere Katukosea sana pale alipoitengeza katiba mwaka 77 ili iwe ya Chama dolla.. alikengeuka kwa kweli, na maujinga mengi aliotuletea,
Lakini bado haya MaCCM chumia tumbo anayacha mbali sana.
 
Ulitaka awe nani? Maana kama ubunge aliteuliwa na Magufuli! Na kwenye baraza hakumteua!
Hakuna lolote ni hasira tu za kukosa madaraka makubwa ndani ya chama na serikalini,inamaana wakati wa Magufuli kulikuwa hakuna kasoro yoyote? Mbona hatujasikia kelele kelele zake.
Sasa wewe ndio inaonekana humjui yule ni njaa ya madaraka ndicho kinachomsumbua.
 
Sijamtetea magufuli, labda kama hujanisoma vizuri!

Hivi mbunge wa kisarawe kuongea kizaramo na wananchi wa kisarawe ni ukabila?
Huo ni ukabila, tena kipindi cha Nyerere ambaye Polepole anam refer hiyo ingeweza kukuondoa.
Na Magufuli alikuwa kiongozi wa kitaifa sio mbunge
Otherwise hoja ya Polepole ina mashiko na muhimu sana

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna lolote ni hasira tu za kukosa madaraka makubwa ndani ya chama na serikalini,inamaana wakati wa Magufuli kulikuwa hakuna kasoro yoyote? Mbona hatujasikia kelele kelele zake.
Sasa wewe ndio inaonekana humjui yule ni njaa ya madaraka ndicho kinachomsumbua.
CCM wote mnaokosa fursa ndio mlivyo, hata nape na January walitoswa na jiwe walianza nongwa.
Mjifunze nyie watu wa ccm
 
Ulitaka awe nani? Maana kama ubunge aliteuliwa na Magufuli! Na kwenye baraza hakumteua!
Si bado alibakia na uenezi CCM sasa mama angemuachia uenezi au kumpandisha kuwa naibu katibu mkuu unafikiri ungesikia kelele, ingekuwa ni kusifu na kuabudu tu.
 
Back
Top Bottom