Hi guys. Hope mnado poa.
Kuna page imeandika kuwa bwana Polepole atajitoa chamani wakishirikina na taasisi 2.
Hii ni nyepesi nyepesi.
At Calvary.
====
Taarifa kwa Vyombo vya Habari.
Jumamosi tarehe 11, Disemba 2021 saa 5:00 Asubuhi nitazungumza na Wanahabari pamoja na Mambo mengine nitazungumzia Shule ya Uongozi | The Leadership School. Mahali - Ofisi za Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC).
-Ujamaa ni Imani-
View attachment 2039936View attachment 2039938
=====
UPDATES;
======
"Kama viongozi wasiposali na kumtemea Mungu nchi yetu haiwezi kuendelea, tumtangulize Mungu mbele. Kuanzia diwani, mpaka mawaziri na kule juu tuwe watu wa maombi, kukumbushana ni muhimu, naona kama tunatakiwa tuishi maisha ya Kimungu hivi." - Humphrey Polepole
"Viongozi wanatakiwa wawe waadilifu na wanyenyekevu." - Humphrey Polepole.
"Nilisema kuhusu magonjwa, mfano ebola, kesi moja tu imewahi kupenya na ikafuatiliwa na sasa tuko salama. Yakaja haya magonjwa mengine maarufu hivi karibuni lakini sio kitu. Nikasema muwe makini hawa wahuni wa kimataifa ni wajanja." - Humphrey Polepole.
"Nilizungumza kuhusu songombingo la wamachinga, Mhe. Rais Samia Suluhu alitoa maelekezo mazuri sana lakini wapo waliotekeleza vizuri wengine wamefanya vibaya mno, wameboronga, ukimkosoa DC au RC kuhusu hili wanasema umemkosoa Rais, nani kakwambia?" - Humphrey Polepole.
"Rais Samia Suluhu alitoa maelekezo mazuri sana kuhusu wamachinga, wapangeni vizuri, msiwazonge, msiwapige, msiwanyanyase.... mimi ni mwana-CCM bana, fitina kwangu ni mwiko. Nikasema mlivyotenda kwa machinga baadhi yenu mmekosea na nikatoa mifano." - Humphrey Polepole.
"Kwenye mgongano wa kimasilahi kuna aina tatu, masilahi ya Taifa, kundi au mtu mmoja mmoja, wanaanza na masilani ya mtu mmoja, kisha kundi na baadaye Taifa, nikasema wanaopanga hivi ni wahuni." - Humphrey Polepole.
"Wahuni wanapenda masilahi binafsi kwanza, kazi yetu ni kuwadhibiti bila huruma wala kucheka nao. Yanatokea majitu tena viongozi na kusema mimi ni muhuni nimepenya, unaweza kutafakari namna gani kiongozi huyu yuko serious, huwezi kuwa kiongozi ukachekelea kuwa mhuni." -Polepole.
"Kule bungeni tunakutana mara chache, mfano kuna kipindi cha mwezi Machi hadi Julai, ina maana mimi niongee mara nne tu kwa mwaka kuhusu wahuni, unadhani inatosha, nitatumia fursa zozote za kusema ili kuwasema wahuni," - @hpolepole, Mbunge wa kuteuliwa.
"Kwa sasa nimeshaanza kufuatilia mambo kadhaa, watu wakizingua pahala ninatoka ninasema hapa umezingua nitaruka na wewe, nakulipua, si wanachelewa kuchukua hatua? - Humphrey Polepole.
"Sijasema Serikali haifanyi kazi, Serikali inafanya kazi nzuri sana lakini ni jukumu letu na kukumbushana. Unadhani kwa nini malaria haiishi na tumesoma mpaka madarasa tukayamaliza? Halafu tunasema tu lete net, hivyo viwanda wanatengeneza wapi?, vya msaada. - Humphrey Polepole.
"Nilieleza kuhusu uchambuzi wa matatizo, malaria haiishi Tanzania kwa sababu hatuchambui tatizo, unadhani ufumbuzi ni chandarua kwani ukitoka usiku kwenda haja ndogo mbu si wanaunga na wewe? tunafanya maamuzi ambayo hayajajengwa katika kutatua tatizo, hilo nalo tatizo." -Polepole
"Kuna kiwanda kipo hapa nchini kinatengeneza viuatilifu vya kuua mazalia ya mbu, nyie wanahabari waulizeni wamewahi kunnuua pale? Mtu analala kwenye chandarua mguu upo nje, mbu wanamng'ata, nauliza sisi tumekwenda shule tukasoma, hii ndio suluhisho kweli?" - Humphrey Polepole.