Humphrey Polepole: Sihami CCM labda Wanitupe nje!, Nimeitwa TCRA nijieleze. Hoja haipigwi rungu bali inajibiwa

Humphrey Polepole: Sihami CCM labda Wanitupe nje!, Nimeitwa TCRA nijieleze. Hoja haipigwi rungu bali inajibiwa

Hiki kinyambolero kimechekewa vya kutosha ndio maana kinapata nguvu ya kujitanua na kuropoka kitakavyo ila mimi ndio ningekuwa president 'sidhani' narudia tena 'sidhani' kama hata kingethubutu kufungua kinywa chake kutema shombo
 
Ameyaongea hayo kwenye mkutano wa chama. Ccm kuweni makini makini mmefuga bomu litawalipukia any time
Uongo ndo jadi yenu,
Mi nadhani hamtumii akili zenu wenyewe.
Hicho kipande kiweke hapo tukione maana nimemsikia mwanzo mwisho
 
Dunia inaenda kwa kasi sana...

Kifo cha Magu kinaweza kuzua matatizo ya akili kwa waumini wake wengi sana...

Mungu atupe uhai tuendelee kushudia mengi...
 
Hampley hata Aseme nini ,hawezi eleweka kiulahisi kwani awamu ya 5 alishiliki pakubwa kuvunja Demokrasia na kuvuruga nchi kwa mambo mengi
 
Mkuu hapo ndio umejibu hoja za Polepole au bado una-search majibu kwanza ila umetanguliza tusi kama kawaida ya wabongo?
Atajibiwa na CCM wenzie, Sisi tupo humu kumpaka Kama yeye alivyotusaliti na kuhamia huko kwenye karamu kisha kuanza kuturingishia viete....Kwa ufupi tunafurahia shida zake.
 
Hata ungekuwa wewe ungedata😂 ghafla machawa wote wamekukimbia....we life la mjini unalijua, machawa Wana Raha yake, machawa hawana Tu hela Ila wanajua viwanja vyote vikali, pisikali zote, na hawakataliwagii....! Sasa ghafla wanakukataa wanakuona umekaukiwa damu, zile mkuu, boss, mkubwa huzisikii tena....halafu ghafla tu...lazima udate, huyu tumuhurumie, kuvaa viatu vyake ni ngumu.
Machawa wote wamejikataa hamna convoy tena maana bia zilikuwa zinanyweka kwa bill ya mwenezi😅 papaa Hanfredi Konokono😅😅😅
 
Kama hawakuiangusha dola Maalim Seif, Mrema, Lowasa, Sumaye, Kingunge. Who is Polepole.
Eti kweli mkuu.... hii ni #Agendasetting.

CCM ukipiga saluti kwa mkono wa kushoto umeasi chama/jeshi.

Ila PLPL ameacha legacy ya kuongeza uhai wa chama ambacho kiliporomoshwa na Upinzani. Alikuta wanachama 2ml akaongeza 15ml.

Amejenga vyuo vya chama Kibaha, kiwanda na chuo Iringa vya UVCCM na chuo kingine Zanzibar kuhuisha chama.

Walikuta thamani ya CCM ni 40bl 2015 wakaipandisha hadi 1tr 2020.

Hiyo rekodi haiwezi kufutwa.

Kwenye medani yeye ni askari wa kikosi cha mbele anayeondoa vikwazo. Wakati tuko kwenye vita ya Kagera enzi hizo ningemfananisha na Gen. John Butler Walden na Gen. David Buzigo Musuguri.

Kwenye medani za siasa namfananisha na mzee Nnauye, Cpt. Komba, Thabit Kombo, Tingatinga Malecela, Simba wa vita Kawawa, Mzee Mangula.

Hata Nyerere alifanya kazi nzuri kwenye chama na serikali, ndani na nje ya nchi lakini hajapata tuzo ya Nobel. UD yenyewe imekuja kutambua kazi zake baada ya kustaafu ndipo wakampa shahada ya heshima ya falsafa. Baghosha!

PLPL ni opposition material, akiingia TLP kitakuwa chama cha pili chenye nguvu Tz, ila mimi hata anihonge viete sichukuwi kadi ya chama chake la sivyo nikichukuwa basi naenda kumlipiza alichonifanyia na KM wake 2020.

Ila ni vizuri kuwa na wapinzani ndani ya chama (siyo nje ya chama tu), ni makosa kuwaondoa au kuwaacha wakajiondoa. Identify, control and retain them kwasababu wanakiimarisha chama kwa ukosoaji wao.
 
Ameyaongea hayo kwenye mkutano wa chama. Ccm kuweni makini makini mmefuga bomu litawalipukia any time
Watanzania ni watu wa ajabu sana,Huu uongo mnaowalisha watu ni kwa faida ya nani?

Polepole kasema yeye aliingia CCM voluntarily na hivyo kama kuna wahuni watamfanyia zengwe kumtoa pia hana shida ataondoka voluntarily.

Halafu hajaongea kwenye mkutano wa chama bali kwenye ofisi za LHRC

Sasa wewe tayari kwa chuki za kichagadema Mnakurupuka bila hata kula,mnaanza kumlisha maneno kisa tu aonekane mbaya.

Sote tunajua jinsi chagadema mnavyoumia na kukaa bench kwa miaka mitano mmejaa sumu mnamuona Humphrey Polepole kama mwenezi ndie alichangia kuwapiga benchi.

Lakini uhalisia ni kwamba wapiga kura tuliwapiga chini.

Na bado 2025 mtapigwa tena.

Ona shauri ya kuweka maslahi binafsi siku hizi hamtaki hata salamu za kina Mdee kisa shekeli.

CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO

Hamtakuja kushika uongozi wa nchi hii.
 
si tunamjua Chakubanga.

vipi vietee zimekauka au?
kiujumla kwa sasa jamaa hamtishi hata nzi.
Chama ch
Hi guys. Hope mnado poa.

Kuna page imeandika kuwa bwana Polepole atajitoa chamani wakishirikina na taasisi 2.

Hii ni nyepesi nyepesi.

At Calvary.

====

Taarifa kwa Vyombo vya Habari.
Jumamosi tarehe 11, Disemba 2021 saa 5:00 Asubuhi nitazungumza na Wanahabari pamoja na Mambo mengine nitazungumzia Shule ya Uongozi | The Leadership School. Mahali - Ofisi za Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC).
-Ujamaa ni Imani-
View attachment 2039936View attachment 2039938

=====

UPDATES;

======

"Kama viongozi wasiposali na kumtemea Mungu nchi yetu haiwezi kuendelea, tumtangulize Mungu mbele. Kuanzia diwani, mpaka mawaziri na kule juu tuwe watu wa maombi, kukumbushana ni muhimu, naona kama tunatakiwa tuishi maisha ya Kimungu hivi." - Humphrey Polepole

"Viongozi wanatakiwa wawe waadilifu na wanyenyekevu." - Humphrey Polepole.

"Nilisema kuhusu magonjwa, mfano ebola, kesi moja tu imewahi kupenya na ikafuatiliwa na sasa tuko salama. Yakaja haya magonjwa mengine maarufu hivi karibuni lakini sio kitu. Nikasema muwe makini hawa wahuni wa kimataifa ni wajanja." - Humphrey Polepole.

"Nilizungumza kuhusu songombingo la wamachinga, Mhe. Rais Samia Suluhu alitoa maelekezo mazuri sana lakini wapo waliotekeleza vizuri wengine wamefanya vibaya mno, wameboronga, ukimkosoa DC au RC kuhusu hili wanasema umemkosoa Rais, nani kakwambia?" - Humphrey Polepole.

"Rais Samia Suluhu alitoa maelekezo mazuri sana kuhusu wamachinga, wapangeni vizuri, msiwazonge, msiwapige, msiwanyanyase.... mimi ni mwana-CCM bana, fitina kwangu ni mwiko. Nikasema mlivyotenda kwa machinga baadhi yenu mmekosea na nikatoa mifano." - Humphrey Polepole.

"Kwenye mgongano wa kimasilahi kuna aina tatu, masilahi ya Taifa, kundi au mtu mmoja mmoja, wanaanza na masilani ya mtu mmoja, kisha kundi na baadaye Taifa, nikasema wanaopanga hivi ni wahuni." - Humphrey Polepole.

"Wahuni wanapenda masilahi binafsi kwanza, kazi yetu ni kuwadhibiti bila huruma wala kucheka nao. Yanatokea majitu tena viongozi na kusema mimi ni muhuni nimepenya, unaweza kutafakari namna gani kiongozi huyu yuko serious, huwezi kuwa kiongozi ukachekelea kuwa mhuni." -Polepole.

"Kule bungeni tunakutana mara chache, mfano kuna kipindi cha mwezi Machi hadi Julai, ina maana mimi niongee mara nne tu kwa mwaka kuhusu wahuni, unadhani inatosha, nitatumia fursa zozote za kusema ili kuwasema wahuni," - @hpolepole, Mbunge wa kuteuliwa.

"Kwa sasa nimeshaanza kufuatilia mambo kadhaa, watu wakizingua pahala ninatoka ninasema hapa umezingua nitaruka na wewe, nakulipua, si wanachelewa kuchukua hatua? - Humphrey Polepole.

"Sijasema Serikali haifanyi kazi, Serikali inafanya kazi nzuri sana lakini ni jukumu letu na kukumbushana. Unadhani kwa nini malaria haiishi na tumesoma mpaka madarasa tukayamaliza? Halafu tunasema tu lete net, hivyo viwanda wanatengeneza wapi?, vya msaada. - Humphrey Polepole.

"Nilieleza kuhusu uchambuzi wa matatizo, malaria haiishi Tanzania kwa sababu hatuchambui tatizo, unadhani ufumbuzi ni chandarua kwani ukitoka usiku kwenda haja ndogo mbu si wanaunga na wewe? tunafanya maamuzi ambayo hayajajengwa katika kutatua tatizo, hilo nalo tatizo." -Polepole

"Kuna kiwanda kipo hapa nchini kinatengeneza viuatilifu vya kuua mazalia ya mbu, nyie wanahabari waulizeni wamewahi kunnuua pale? Mtu analala kwenye chandarua mguu upo nje, mbu wanamng'ata, nauliza sisi tumekwenda shule tukasoma, hii ndio suluhisho kweli?" - Humphrey Polepole.

"Nilizungumza kuhusu deni la taifa, kuna watu wengine ni wabunge wakaibuka wanasema ooh deni limekuuwa kubwa, zito linamuelea mama. Nikatoka nikasema ukweli wasipotoshe, ni uongo. Si viongozi wote tupo kwa nini mwenzetu anapotosha na hatutoki kusema? kimya. -Humprhey Polepole.

"Sijui kwa nini viongozi wanaogopa kusema, sijui wanaogopa, kwa sababu deni linalosemwa viongozi wote walikuwepo, niweke sawa watu wasielewe tofauti. Kwa nini wenzetu msitoke mkasema, au mpaka watu wachanganyikiwe, penye ukweli lazima tuseme ukweli? - Humphrey Polepole.

"Juzi Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ndiye amekuwa mtu wa kwanza kutoka na kusema deni la Taifa ni himilivu, na yeye amejiongeza tu baada ya kuona kimya." - Humphrey Polepole.

"Sijazungumzia mtu, mbunge, mamlaka ya nchi wala mjomba wake mtu lakini baadhi ya viongozi wamechukia, kwa nini unaongea? Hivi imefika pahala tunaulizana kwa nini umeongea, Mungu amenipa mdomo unataka nifanye nini? Kuna kula na kuongea. - Humphrey Polepole.

ZAIDI SOMA.....


"Nilipofanya Shule ya Uongozi nikapigiwa simu na watu wanaambiwa acha kwanza, nikauliza kwa nini? hakuna majibu. Nimefanya kazi na Mzee Mkapa, Kikwete, Magufuli na Mama Samia, hawa viongozi wangu wote hawajawahi kuniambia 'kaa kimya', nawashangaa wanaotaka ninyamaze." - Polepole.

"Mwalimu Nyerere alisema 'hoja ahipigwi rungu, inajibiwa kwa hoja bora zaidi', mimi ni mwana-CCM ninawaambia hapa kuna tatizo linarekebishika hivi, unasema kaa kimya, hilo ni jibu la hoja nilililoitoa." - Humphrey Polepole.

"Niliitwa kwenye chama kwa tuhuma, nilizijibu zote moja baada ya nyingine, siwezi kusema, chama kitakuja kuzungumza." - Humphrey Polepole.

"Nimeitwa TCRA, wanasema nimetoa maudhui ya kupotosha umma yanayoweza kuchochea Watanzania kugomea na kudhoofisha kampeni ya Kitaifa kujikinga na Corona. Hivi mimi nimeshawahi kuwaambia tudhoofishe kampeni ya kujikinga na corona? hawa wanataka kunichomeka hapa" -Humphrey Polepole

"Sijawahi kusema kwa nini sichanji, sasa tusisukumane nikafafanua kwa nini sikutaka kuchanja. Sasa nitakwenda TCRA kupeleka utetezi wangu nikaseme ukweli maana tunatafutana kwenye korido la corona." - Humphrey Polepole.

"Hii hoja ya wamachinga nasema kweli mmeonea watu, halafu mtu anasema kaa kimya, kumbe jukumu la mbunge ni nini? Sauti ya watu ni ipi? Hii kaa kimya nimehangaika nayo sana, nimefanya tu kiubishi." - Humphrey Polepole.

"TCRA wanasema wamenipa leseni kwa ajili ya maudhui ya kipindi cha Papo kwa Hapo, wanahoji kwa nini ninafanya Shule ya Uongozi... hivi mimi nimekulipa milioni ile halafu unanipangia cha kuzungumza? naweza kuposti familia yangu au mbwa wangu, utaniuliza?" - Humphrey Polepole.

"Kuhusu corona kuna ubishi wa kidunia, kila mtu ana upande wake, na mimi niweke wazi nipo kwenye ubishi huo. Mpaka Yesu atarudi tunaendelea na ubishi," Humphrey Polepole.

"Suala la machinga wanasema nimesema uongo, tena kwenye hilo nitasema na mengine ambayo sikutaka kusema, nina ushahidi, nimepeleka watafiti wilaya zote za Dar es Salaam, mtu amehamishwa na kupelekwa kwenye karo la choo, hivi Mhe. Rais aliwatuma hivyo?" - Humphrey Polepole.

"Kuna watu wanasema Polpole anajitoa CCM anakwenda kuanzisha chama chake, nataka niwaambie niliingia CCm kwa hiari mwaka 2000 nikapiga kura kwa mara ya kwanza, sitatoka CCM kwa hiari. Kama ninatoka CCM washike wanitupe nje, bado tupo sana hapa." - Polepole.


Mbunge wa Kuteuliwa (CCM),Humphrey Polepole amesema amepokea Mashtaka ya TCRA yanayosema kupitia Kipindi chake cha Shule ya Uongozi, amerusha Maudhui yanayopotosha Umma na yanayoweza kuchochea Watanzania kuweza kugomea Kampeni ya Kitaifa ya #COVID19

Akizungumza leo amesema, "Hivi mimi nimewahi kuwaambia ninyi tudhoofishe Kampeni ya Corona? Wapi niliwaambia kwa maana hiyo?"

Amesema kwasababu amepewa nafasi ya kujibu, atapelekea Utetezi wake aliodai unajitosheleza

#JamiiForums #UVIKO3

Sii wewe uliyeusaliti mchakato wakupatikana katiba mpya, au no mwingine baada ya kuwa na yhakika wakushibisha tumbo lako punde baada ya teuzi za chamani, je nini kimeenda kombo unajaribu kujitenga na Cha kwa gharama ya kiwango hiki, au anafadhili nani gharama?
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana,Huu uongo mnaowalisha watu ni kwa faida ya nani?

Polepole kasema yeye aliingia CCM voluntarily na hivyo kama kuna wahuni watamfanyia zengwe kumtoa pia hana shida ataondoka voluntarily.

Sasa wewe tayari kwa chuki za kichagadema mnaanza kumlisha maneno kisa tu aonekane mbaya.

Sote tunajua jinsi chagadema mnavyoumia na kukaa bench kwa miaka mitano mmejaa sumu mnamuona Humphrey Polepole kama mwenezi ndie alichangia kuwapiga benchi.

Lakini uhalisia ni kwamba wapiga kura tuliwapiga chini.

Na bado 2025 mtapigwa tena.

Ona shauri ya kuweka maslahi binafsi siku hizi hamtaki hata salamu za kina Mdee kisa shekeli.

CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO

Hamtakuja kushika uongozi wa nchi hii.
Umesahau wagombea wa chadema walivyokuwa wanatekwa na polisi ili wasirudishe form? Umesahau mlivyokuwa mnajitangaza kuwa mmpita bila kupingwa? Sasa hapo mwanachi anaaply wapi kura yake!!
 
Napenda wajuvi wa Mambo Kama wewe,japo Sina uhakika na kile umekilenga kutokana na story ya mzee wa vitendawili.

Ila namuhurumia maana Rutto ni kitu kingine.
Ruto hawezi tena kushinda urais kwa njia ya masanduku ya kura, amebakisha option moja tu ya assassination ya Uhuru ili kwa huruma ya katiba achukuwe nchi pale rais akifa madarakani, ili kwamba a-postpone uchaguzi apate muda wa kujipanga na kushughulikia wapinzani wake wote. Ziara ya Uhuru Kisumu kikosi cha Ruto kilitegesha bomu kwenye ndege iliyomfuata Uhuru toka Kisumu, Raila aligundua njama akamkataza Uhuru asipande ndege hiyo, ndege ilipofika Kisumu ikakaguliwa na kukuta bomu, Uhuru akarudi Nairobi kwa ndege ya jeshi na wote waliohusika na maandalizi ya ndege hiyo ya kumfuata rais wakaingizwa kwenye mateso makali hadi wakatajana na kumtaja Ruto.
 
Back
Top Bottom