Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Hussein Bashe hata kabla ya kuingia na kuteuliwa katika wizara hii alikuwa akisimama bungeni kuchangia katika wizara hii. Kila mtanzania alitamani na kuomba apewe uwaziri wa kilimo ili atekeleze kwa matendo yale azungumzayo. Hatimaye akaaminiwa na kupewa wizara. Kiukweli tangu amepewa tumeona namna wizara ilivyobadilika kiutendaji.
Ni mfuatiliaji mzuri juu ya kinachoendelea wizarani kwake na hata akisimama kuzungumza unajua na kuona kuwa anazo taarifa zote za wizara na anafuatilia utendaji kazi wizarani. Naona namna yeye na mama yetu Mh. Rais wanavyopambana kuhakikisha mwaka huu mbolea inapatikana kwa bei rafiki kwa kutoa ruzuku huku mkulima akiuza mazao yake kwa bei nzuri.
Hongera Sana Mh. Hussein Bashe, vijana tunakutegemea uendeleee kuchapa kazi ili kilimo kitunufaishe. Maana kilimo ni ajira na pumzi yetu, kilimo ndio usalama wa nchi, hivyo simamia vyema kulinda usalama wetu wa chakula na uchumi wetu. Maana kilimo ndio uti wa mgongo wa nchi yetu.
Asante, kazi iendeleeee! Baba yangu anasema wewe ni kama mzee Paul Kimiti alivyoitendea haki wizara hiyo.