Hussein Bashe anastahili pongezi kwa namna anavyochapa kazi katika Wizara ya Kilimo na kutekeleza maelekezo ya Rais Samia

Hussein Bashe anastahili pongezi kwa namna anavyochapa kazi katika Wizara ya Kilimo na kutekeleza maelekezo ya Rais Samia

Clearly either kuna kitu unajua kuhusu Bashe sisi wengine hatujui au labda ni chuki tu zisizo na msingi.

Kwa mim raia wa kawaida kabisa na akili yangu ndogo wizara ya kilimo nikiipima kwa data kabla na baada ya Bashe naona kuna mambo mengi ameyapa momentum/msukumo. Wakati mwingine hata kuwapa wadau wa sekta confidence na political will ni mchango tosha.
Hata nami naona Hilo mkuu kuwa huyu ndugu yetu ana chuki binafsi na mh Waziri Hussein Bashe, maana naona hajengi hoja za kueleza kwa takwimu au ushahidi za kupinga tusemayo Bali amejikita katika matusi na kauli zenye ukakasi kwa mh Waziri

Ukiona mtu badala ya kujenga hoja anajikita katika matusi Basi ujuwe Kuna tatizo mahali linalomsibu, maana mtu mstaarabu na muungwana lazima ajikite katika hoja bila matusi Wala ukakasi wa lugha hata Kama hamtakubaliana katika hoja,
 
Hussein Bashe hata kabla ya kuingia na kuteuliwa katika wizara hii alikuwa akisimama bungeni kuchangia katika wizara hii. Kila mtanzania alitamani na kuomba apewe uwaziri wa kilimo ili atekeleze kwa matendo yale azungumzayo. Hatimaye akaaminiwa na kupewa wizara. Kiukweli tangu amepewa tumeona namna wizara ilivyobadilika kiutendaji.

Ni mfuatiliaji mzuri juu ya kinachoendelea wizarani kwake na hata akisimama kuzungumza unajua na kuona kuwa anazo taarifa zote za wizara na anafuatilia utendaji kazi wizarani. Naona namna yeye na mama yetu Mh. Rais wanavyopambana kuhakikisha mwaka huu mbolea inapatikana kwa bei rafiki kwa kutoa ruzuku huku mkulima akiuza mazao yake kwa bei nzuri.

Hongera Sana Mh. Hussein Bashe, vijana tunakutegemea uendeleee kuchapa kazi ili kilimo kitunufaishe. Maana kilimo ni ajira na pumzi yetu, kilimo ndio usalama wa nchi, hivyo simamia vyema kulinda usalama wetu wa chakula na uchumi wetu. Maana kilimo ndio uti wa mgongo wa nchi yetu.

Asante, kazi iendeleeee! Baba yangu anasema wewe ni kama mzee Paul Kimiti alivyoitendea haki wizara hiyo.
Kazi gani anachapa?
 
Back
Top Bottom