Hussein Bashe, zuia mahindi kutoka nje kwanza nchi ijitosheleze

Acha watu wauze nje huko wajikwamue,

Serikali ingekua ya maana ingesaidia uzalishaji uwe kwa wingi na kiwango safi ili apo tuuze nje na hapa
 
Kama utashindwa kununua mahindi nenda kanununue ngano, upuuzi huu yaje mataifa yote dunian kununua mazao uku, wakulima nao tunufaike tena mtuache tuuze popote pale tunapataka
 
Tuna HAKI kudai wizara idhibiti mfumuko wa Bei masokoni,

Tunalipa Kodi, timizeni wajibu wenu.
 
 
Kama yeye msomali na wewe tunakujuwa ni mrundi hapa hatuangalii kabila la mtu tunaangalia utendaji wacha wakulima wauze mazao yao wanapotaka kama serkali inataka iyanunue kwa bei ya soko wakati wa kunyanyasa wakulima umekwisha lazima tumpongeze rais huyu ndiye kabisa rais wa wanyonge tunamuona anafanya kwa vitendo.
 
hii ni hoja ya kijinga zaidi kwa mwaka 2023, nipo mbozi nanua debe kwa 12000, so acha tununue wakulima wanufaike na kazi yao
Anayenunua Kilo ya Unga Leo kwa Tsh 2000 ni huyo peasant ambaye aliuza mahindi yake kwa watumishi na wafanyabiashara kwa Tsh 500 kwa kilo.

Huku ni kuchenji buku kwa njaa ya mtoto. Ameuza 500, Leo serikali yake inamletea anunue kwa 900.

Tena ameuza 500 kupata hela ya kuishi July-Sept, baada ya hapo anahangaikia kilo ya unga 2000 kutoka Sept to June.

Hatari zaidi mvua hazikutosha mwaka huu, msimu huu wa mavuno mkulima hana cha kuuza tena.

Hawa ni wauaji wa kisasa wanaopigiwa makofi na waombolezaji. Tuna serikali mfu.
 
Kwa nini Samia halioni hili angemtoa huyu msomali wizara hiii ingetulia sana maana imekuwa wizara ya hovyo sana maaana ssa kuna mgogoro mkubwa sana na mawakala kuhusu mbolea kutokulipwa hawajui nani aulizewa
 
Wa ndani wangelia mno
 
Naona kwa baadhi ya mikoa bei ya mahindi imeanza kushuka.

Last week nimenunua sehemu debe moja la mahindi shilingi 11,000.

Hope kufikia mwezi Juni, huenda bei ikashuka zaidi
 

Heri ungeishauri serikali inunue hayo mahindi kutoka kwa wakulima na kuyahifadhi kama suala ni usalama wa chakula.

Kuzuia kuuza chakula ni ujinga na uchoyo/ubinafsi dhidi ya binadamu wenzetu. Sisi kuwa na ardhi kubwa na hali ya hewa nzuri isiwe fimbo ya kuwanyima wengine chakula. Juzi tu tumewasaidia Malawi, huoni umuhimu huo?

Kingine labda ni utaratibu mzuri wa kuuza haya mazao ya chakula hata mifugo bado upo hovyo sana. Sioni kama ni tija mgeni kununua mazao yakiwa shambani.

Hapa waziri na wadau wote katika kilimo, tunahitaji kuboresha namna nzuri ya kuuza mazao hayo na sio kama ilivyo sasa.
 
Jamani punguzeni kutukanana basi mujadili hoja kwa faida yetu sote.
 
Hamasisha watu kulima usiwakataze kuuza wapendapo Kama unaona bei ni kubwa nenda shambani ukalime.
Yawezekana hujui kulima au hujalima msimu huu kwa hi yo hujajua watulivyohangaika kupata pembejeo.
 
Hak
Hakuna ujinga huu maana uwekezaji wa kwenye kilimo utatoweka na sera za kijinga jinga kama huyu mdau anavyosema. Tukitaka bei ipungue tuongeze uzalishaji ! Mahindi yakiwa mengi bei itapungua. Sasa kama mtu kalima kwa makubaliano na kampuni au hotel za kenya ukizuia inakuwaje kama kakopa bank?
 

Hizo Tshs wanazipata wapi?
 
 
Wewe mpumbav una uchungu gani na mkulima ? , Eti peasant
Mkulima akinunua chakula kwa bei wewe inakuhusu au kinakuuma ni nini ?
Wewe umekuwa msemaji wa wakulima nyani wewe ?
Ninyi wenye pesa ndio mnaolia kununua kilo ya unga kwa huku tatu ? ,Mna akili ninyi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…