FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Binafsi ni mkulima na mfugaji, tena wa siku nyingi sana, sijaanza leo wala jana.Zamani tulisikia kauli kama "kama umeshindwa maisha ya mjini nenda kalime" tukaenda kulima. Sasa hivi hao hao waliotufukuza mjini wanaona wivu tusiishi maisha mazuri kwa pesa nzuri ya mazao yetu.
Nyie watu wa mjini mmezidi kudeka. Mkija Krismass mnatulingishia vigari vyenu ila mpaka Samia na Bashe wanaondoka madarakani tutakuwa tumewatia adabu.
Nyie watu wa mjini badala ya kununua stock ya chakula mkaweka ndani nyie mmejaza majumba na maTV, ma-home theater, makochi ya kichina, n.k. mnatumia fedha kwa mashindano kununua mahari na kuyajaza mafuta kila siku hata kama uwezo hamna, mnashindana kumiliki mademu, kununua nguo kila mwezi, kula bata bar n.k lakini kutenga laki 2 ununua gunia mbili za mahindi unaona mkulima anapewa hela nyingi.
Nikushukuru FaizaFoxy kwa kuunga mkono wakulima.
Nawashangaa wasioelewa faida za mashamba.
Kama ni ushamba basi mimi ni mshamba namba 1.