MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Jomba chukua jembe ukalime mahindi ya familia yako. Acha kulilia majasho ya watu wengine.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wizara chini ya Bashe isikwepe wajibu wake kuhakikisha inadhibiti mfumuko wa Bei.Ni kweli kabisa japo mbolea imewekwa ruzuku ambayo hairejeshwi wakati wa kuuza mazao yao hivyo kwa namna moja au nyingine Serikali ina hisa hapo. Nafikiri Muhimu zaidi hapa ni Elimu Elimu Elimu.....
Kwa kukosa Elimu wakulima wanauza mahindi/mazao kwa fujo bila kujiwekea akiba, baada ya miezi sita wanalia kuwa hawana chakula na kuilaumu Serikali kwa kutowapelekea mahindi.....
Watu wanashinda kwenye bajaji huko sijui bodaboda na wengine wezi siku hizi wanajiita wapiga debe.Ungejua tunavyohangaika na kilimo usingesema hivo jombaa. Niuze ndani ya nchi gunia moja elfu 36 anakuja mkenya gunia moja nauza laki 1 na 20 hata kama ni ww unamuzia nani hapo????
Kenya sio mtoto au mjomba wetu; in fact hajawahi kuwa jirani mzuri. Kenya ni jirani "maslahi ".Busara na weledi vitumike kwenye suala la chakula. Hilo ni suala serious.
Kwa nini Serikali isununue na kuwa na akiba ya kutosha ili kuweka security and supply flow of grains?
Serikali yoyote makini huhakikisha usalama na upatikanaji wa chakula kwa wananchi wake. Hicho ni kipaumbele. Ni JUKUMU NA WAJIBU WAKE. Na kama haiwezi au haitekelezi hilo basi haina sababu wala uhalali wa kuwepo.
Hiyo haimaniishi mkulima anyonywe au apunjwe kama Wajamaa na vyama vyao vya ushirika walivyozea kufanya. Hapana!
Mkulima apewe/alipwe kwa competitive market rates/bei shindani za soko. Serikali ihakikishe food security hilo ni kazi yake na hapo hapo maslahi mapana ya mkulima yalindwe.
Kuna wajinga wengi humu wanadhani tunapoinyooshea vidole wizara ya KILIMO chini ya bashe tuna Nia mbaya na wakulima. Si Kweli.Busara na weledi vitumike kwenye suala la chakula. Hilo ni suala serious.
Kwa nini Serikali isununue na kuwa na akiba ya kutosha ili kuweka security and supply flow of grains?
Serikali yoyote makini huhakikisha usalama na upatikanaji wa chakula kwa wananchi wake. Hicho ni kipaumbele. Ni JUKUMU NA WAJIBU WAKE. Na kama haiwezi au haitekelezi hilo basi haina sababu wala uhalali wa kuwepo.
Hiyo haimaniishi mkulima anyonywe au apunjwe kama Wajamaa na vyama vyao vya ushirika walivyozea kufanya. Hapana!
Mkulima apewe/alipwe kwa competitive market rates/bei shindani za soko. Serikali ihakikishe food security hilo ni kazi yake na hapo hapo maslahi mapana ya mkulima yalindwe.
Uko sahihi kwa hili.Kuna wajinga wengi humu wanadhani tunapoinyooshea vidole wizara ya KILIMO chini ya bashe tuna Nia mbaya na wakulima. Si Kweli.
Wizara hiyo inashirikiana na makampuni hayo kuhujumu USALAMA wa chakula nchini.
Hujuma hii ni hatari Kwa Amani na Utulivu wa Nchi.
Kwamba bashew na makampuni yanayoruhusiwa kununua vyakula direct mashambani ni wakulima hao?Bei ni nafuu mno wewe ndio huna hela... Haiwezekani Bia ununue ths 3000/= kwa chupa halafu kilo ya Unga unataka ununue kwa tsh900/=
Sisi wakulima tunataka watu waheshimu kilimo... Tunataka bei kubwa ya mazao bila kujali nani atakufa ndio interest yetu...
Hoja zenu zinafikirisha kana kwamba mnaona kilimo ni sehemu ya watu wanaotakiwa kujitoleaMbona walipopewa ruzuku hukusema kama watoe hela zao chakula ni usalama wa taifa acheni siasa ruzuku ni Kodi za watu wote wanaolima na wasio Lima katika nchi ujue Kuna mgawanyo wa majukumu hawezekani Kila mwana nchi awe analima je huyo mkulima akienda hospital ambiewe hajitibu hutakija kuropoka hapa kuwa sio haki
Huyo msomali ni hatari kwa usalama wa nchi yetu lakini bado anaingia kwenye vikao vya juu kabisa vya nchi.
Ana wahujumu watanzania.
Hana uzalendo wowote.
Rais Samia nae Wala hajali.
Wala hajui afanye nini.
Hayo mahindi yaliyokutesa kukausha, ulilimia wilaya ya Rungwe? Maana huko ndio wanakaushia mahindi darini!!!Acha kukimbia hoja???? Je huyo mkulima unaweza fidia gharama aliuzotumia shambani au unapuyanga jombaaa. Kuna mwaka nimelima mahindi napata gunia 60 nikasema nimeuaga umasikini bei ya soko la ndani tukauza elfu 24 gunia kisa kufunga mipaka. Mahindi hayo yalinitesa kukausha mvua zinapiga kila siku.
Kwani mkulima anapomwuzia Mkenya ni kwa sababu anataka kumsaidia Mkenya?. Mkulima anatafuta mahali panapoweza kumpa bei nzuri. Iwe ni Kenya, Zambia, Ulaya, na iwe hivyo.Kenya sio mtoto au mjomba wetu; in fact hajawahi kuwa jirani mzuri. Kenya ni jirani "maslahi ".
Akikuchekea tizama jino pembe
Pia Bashe akizuia mahindi au mchele usitoke kwenda nje ahakikishe wakulima wanalipwa bei ya masoko yao ya nje !! Sio muwapangie bei mnazotaka ninyi ! Kwani mliwasaidia kulima ??!! Kila mtu ashinde mechi zake !!Nimeona baadhi ya maeneo mahindi yameanza kuvunwa hasa mkoa wa Rukwa na nimeona malori kutoka Kenya na wanunuzi karibia wote wanapeleka shehena ya mahindi Zambia na Congo...
Hatukatai watu kuuza nje lakini kwa kuwa maeneo mengi ya nchi hawakulima mahindi ya kutosha na mikoa mingine kama Morogoro mahindi yameharibika mashambani kwa kukosa mvua za kutosha ...
Nakushauri Tena kwamba zuia kwanza mahindi yasiende nje ili tujitosheleze ... au serikali kupitia nrfa iingie kununua kabla hatujabaki na mabua !!
Nakufahamu hupendi kushauliwa na mtu lakini asiesikia la mkuu huvunjika
Kwakweli !Miye niko kijijini ndiyo maana nawashangaa nyie wa mjini kutaka bei ishuke uliona wapi mtu wa kijijini akalala njaa wanaolala njaa ni nyie wa mjini msio lima
Umemaliza kila kitu !!Kwani mkulima anapomwuzia Mkenya ni kwa sababu anataka kumsaidia Mkenya?. Mkulima anatafuta mahali panapoweza kumpa bei nzuri. Iwe ni Kenya, Zambia, Ulaya, na iwe hivyo.
Mkulima anatafuta mahali palipo na maslahi mazuri.
Na hizi story za kusema Kenya.siyo jirani mzuri, acheni hadithi za kipuuzi. Kenya amefanya nini kwa Tanzania mpaka aonekane ni jirani mbaya? Matatizo yenu msibebeshe watu wengine.
Mimi ni kati ya wwtu wanaoathitiwa sana na bei za vyakula, kwa sababu nina wafanyakazi ambao ni lazima niwape chakula wawapo kazini. Wapo wanaokula saa 4 asubuhi na saa 7 mchana, wapo wanaokula milo yote mitatu (walinzi). Zamani nilikuwa natumia milioni 5 kwa mwezi lakini sasa hivi ni milioni 15. Hata hivyo siwezi kuthubutu kushauri mkulima afungiwe masoko, auze tu ndani ya nchi. Safari hii tayari nimeingia makubaliano na wakulima fulani, kuanzia mwezi ujao naanza kukusanya mahindi magunia 800 na mpunga magunia 500 na magunia 200 ya maharage kwaajili ya chakula cha wafanyakazi.
Kila mtu ni lazima aangalie maslahi yake. Wewe kama mwajiriwa, siku zote unafurahia kupata mahali penye mshahara mzuri zaidi, mkulima anamtafuta mnunuzi mwenye bei nzuri zaudi,mnunuzu anatafuta mahali penye beu ndogo, n.k. Ndivyo maisha yalivyo.
Na huo ndio ukweli mchungu !!Kama serikali inaweza kununua mahindi kwa bei ya juu ili kunusuru walaji, kwa nini isitumie pesa hizo hizo kuwapa ruzuku wakulima ili walime kwa bei nafuu na kuuza kwa bei nafuu?
Wakulima wanalima kwa ukiwa na shida tele , wanakuja kuonekana na serikali wanapouza mazao yao tu.
Tatizo miaka yote wakulima wanachukuliwa kama vile wao ni manamba wa watu wa mijini ! Serikali ni lazima iwalinde wakulima na iwape ruzuku kama inavyowapa ruzuku watu wa vyama vya siasa !! Ikifanya hivyo ndipo itakapokuwa na uhalali wa kuwapangia wauze wapi mazao yao 🙏🙏🙏Siyo lazima kila mtu alime! Mfanyakazi analipwa mshahara, ambao atatumia sehemu ya huo mshahara kununulia chakula kutoka kwa mkulima.
Na mkulima akipata hiyo pesa, atanunulia mahitaji yake ya msingi. Maisha siku zote hutegemeana. Hatuwezi wote kuwa wakulima.
Na mfahamu fika hii biashara ya mazao mnayofanya na Wakenya hao na Wasomali, siyo endelevu! Siku wakiamua kununua hayo mazao yenu sehemu nyingine; mtalia na kusaga meno.
Lakini pia tusiwaone mkilalamika pale serikali itakapo ruhusu chakula kutoka nje, kuingizwa nchini ma kuuzwa kwa bei nafuu. Nyinyi wauzieni Wakenya na Wasomali hico chakula chenu kwa bei nafuu!! Na wakati huo huo Serikali iruhusu wafanyabiashara kuingiza chakula kutoka nje ili kupunguza mfumuko wa bei ya chakula.
Nadhani hamtalalamika. Maana kila mtu atakuwa ameshinda mechi zake.
Kwanini utafute unafuu wa Bei Kwa MKULIMA kama una Nia ya kumsaidia MKULIMA?Kwani mkulima anapomwuzia Mkenya ni kwa sababu anataka kumsaidia Mkenya?. Mkulima anatafuta mahali panapoweza kumpa bei nzuri. Iwe ni Kenya, Zambia, Ulaya, na iwe hivyo.
Mkulima anatafuta mahali palipo na maslahi mazuri.
Na hizi story za kusema Kenya.siyo jirani mzuri, acheni hadithi za kipuuzi. Kenya amefanya nini kwa Tanzania mpaka aonekane ni jirani mbaya? Matatizo yenu msibebeshe watu wengine.
Mimi ni kati ya wwtu wanaoathitiwa sana na bei za vyakula, kwa sababu nina wafanyakazi ambao ni lazima niwape chakula wawapo kazini. Wapo wanaokula saa 4 asubuhi na saa 7 mchana, wapo wanaokula milo yote mitatu (walinzi). Zamani nilikuwa natumia milioni 5 kwa mwezi lakini sasa hivi ni milioni 15. Hata hivyo siwezi kuthubutu kushauri mkulima afungiwe masoko, auze tu ndani ya nchi. Safari hii tayari nimeingia makubaliano na wakulima fulani, kuanzia mwezi ujao naanza kukusanya mahindi magunia 800 na mpunga magunia 500 na magunia 200 ya maharage kwaajili ya chakula cha wafanyakazi.
Kila mtu ni lazima aangalie maslahi yake. Wewe kama mwajiriwa, siku zote unafurahia kupata mahali penye mshahara mzuri zaidi, mkulima anamtafuta mnunuzi mwenye bei nzuri zaudi,mnunuzu anatafuta mahali penye beu ndogo, n.k. Ndivyo maisha yalivyo.
Tatizo ni Haki bin Haki! Wakulima huwa hawapangi bei za PEMBEJEO!Tatizo nadhani ni Samia mwenyewe wala sio huyo Bashe
Hii comment imefunga mjadala huu !! Umemaliza Mkuu !Kwanini utafute unafuu wa Bei Kwa MKULIMA kama una Nia ya kumsaidia MKULIMA?
Hatuna ugomvi na MKULIMA.
Tunataka Serikali inunue vyakula hivyo Kwa Bei ya sasa MKULIMA apate pesa yake ajiandae na msimu ujao.
Serikali Itunze chakula hicho kwenye maghala katika mikoa mbalimbali nchini.
Itakapofika miezi ya Sept Hadi January, Serikali ifungue maghala Ili wakulima na wafanyabiashara masokoni wakinunue tena Kwa Bei nafuu wakati wakisubiri mavuno.
Jambo hili la Serikali kutunza vyakula ktk maghala kutamsaidia MKULIMA akipate chakula hicho hicho alichokiuza wakati ambao Yuko katika kusubiri mavuno.
Sirikali isifuche udhaifu wake Kwa HOJA mufilisi kwamba MKULIMA asipangiwe wapi auze wakati yenyewe hainunui na kutunza ghalani kudhibiti mfumuko wa Bei.
Sirikali imsaidie MKULIMA kutunza chakula ghalani Kwa kukinunua na kumuuzia tena Kwa Bei nafuu.