Hussein Bashe, zuia mahindi kutoka nje kwanza nchi ijitosheleze

Kwa nini sasa iwe lazima mkulima apangiwe wa kumuuzia mazao yake?
Mimi naona Serikali ingeruhusu soko huria kwa pande zote mbili! Yaani kwa wakulima wa ndani kuuza mazao yao nje ya nchi kwa bei nzuri!

Lakini pia wafanyabiashara wetu nao wangeruhusiwa kuingiza chakula chenye ubora ndani ya nchi, na kukiuza kwa bei nafuu.
 
Ukweli mtupu.. Hawa wajinga ndio wanafanya kilimo kionekane cha watu masikini... Tunataka mahindi yote yatoke nje tupate hela turudi shamba... Sisi wakulima tunataka hilo
 
Ukweli mtupu.. Hawa wajinga ndio wanafanya kilimo kionekane cha watu masikini... Tunataka mahindi yote yatoke nje tupate hela turudi shamba... Sisi wakulima tunataka hilo
Hakuna shida hizo faida na makusanyo yanayopatikana kwenye kilimo zitumike kugharamia hizo sector pia na madeni yake serikali inayokopa.

Hela za watu wa mjini zitumike kutengeneza utajiri wa mijini pia kuna vijana wengi hayo mabillioni yanayoenda vijijini wangefaidika kama zingewekezwa kwenye viwanda wapate ajira; hiko chakula wakimudu.

Yaani wakulima wao wanajua kupokea tu, ubaya tunawalaumu watu wasiofaidika isipokuwa madalali wa chakula.
 
Unajua mahusiano yaliyopo kati ya hazina ya CHAKULA nchini na USALAMA wa Nchi?

Kama Kweli wakulima wanatosheleza soko la ndani, mbona hatuoni competition itayoleta unafuu wa Bei masokoni na ubora wa bidhaa Kutoka masokoni?
Bei ni nafuu mno wewe ndio huna hela... Haiwezekani Bia ununue ths 3000/= kwa chupa halafu kilo ya Unga unataka ununue kwa tsh900/=
Sisi wakulima tunataka watu waheshimu kilimo... Tunataka bei kubwa ya mazao bila kujali nani atakufa ndio interest yetu...
 
So uache uongeleee mambo mengine,au unaonea wivu wakulima,Kama unaumua mwambie mwenyekiti wako akupe muongozo Basi, jamaniiii,tuacheni tuu, wakulima
 

Hutaki kulazimishwa kulima sasa kwa nini unataka kulazimisha mkulima apangiwe pa kuuza?
 
Acha wivu, watu wafanye kazi sio kutegemea ruzuku


N:B nimeandika kwa swahil ili unielewe
 

Sawa muhimu hapo mkulima hajapangiwa pa kuuza
 
Hutaki kulazimishwa kulima sasa kwa nini unataka kulazimisha mkulima apangiwe pa kuuza?
Mimi sijalazimisha mkulima kupangiwa pa kuuza. Mimi natamani kuona bei ya chakula ikiwa rafiki kwa mlaji. Hivyo naunga mkono wakulima kuuza mazao yao nje ya nchi kwa bei nzuri.

Ila wakati huo huo Serikali iruhusu chakula kutoka nje, kuingizwa nchini na kuuzwa kwa bei nafuu na hivyo kupunguza mfumuko wa bei ya chakula nchini.
 
Muwe waelewa pia pale Serikali itakapofungua mipaka yake kuruhusu chakula kutoka nje, kuuzwa nchini. Maana na sisi ambao siyo wakulima, tunachoka kununua chakula kwa bei isiyo na uhalisia.
Wewe husiye lima unadhani bei yenye uhalisia ni kama bei gani
 
Bro nenda kalime acha ujinga aisee...
 
Huu ujinga ulimezeshwa na nani ndugu..
 

Wa kuangalia maslahi ya wazo lako ni serikali na sio mkulima/wakulima mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…