Hussein Bashe, zuia mahindi kutoka nje kwanza nchi ijitosheleze

Wizara chini ya Bashe isikwepe wajibu wake kuhakikisha inadhibiti mfumuko wa Bei.

Zipo njia mbalimbali za kuhakikisha Bei zinahimilika.

MKULIMA auze atakapo, lakini kuruhusu Wageni kuingia Hadi shambani ni kuminya ajira ya Watanzania ktk masoko ambao ndo Huwa wanawauzia wageni.

Mfano Wafanyibiashara Kutoka Sea Shells wakiruhusiwa kwenda mashambani kununua Kwa MKULIMA, Soko la KARIAKOO litakuwepo?

IPO haja ya aliyetoa kauli ya KULA KWA UREFU wa KAMBA atoke hadharani na kuifuta.

Kuna namna Bashevu ananufaika na makampuni haya.
 
Ungejua tunavyohangaika na kilimo usingesema hivo jombaa. Niuze ndani ya nchi gunia moja elfu 36 anakuja mkenya gunia moja nauza laki 1 na 20 hata kama ni ww unamuzia nani hapo????
Watu wanashinda kwenye bajaji huko sijui bodaboda na wengine wezi siku hizi wanajiita wapiga debe.
Ndo wauziwe chakula bei rahisi!
Uza nje chakula chote kikiisha watarudi vijijini kwao walikokimbia kilimo na kuja kutujazia tu miji
 
Busara na weledi vitumike kwenye suala la chakula. Hilo ni suala serious.

Kwa nini Serikali isununue na kuwa na akiba ya kutosha ili kuweka security and supply flow of grains?

Serikali yoyote makini huhakikisha usalama na upatikanaji wa chakula kwa wananchi wake. Hicho ni kipaumbele. Ni JUKUMU NA WAJIBU WAKE. Na kama haiwezi au haitekelezi hilo basi haina sababu wala uhalali wa kuwepo.

Hiyo haimaniishi mkulima anyonywe au apunjwe kama Wajamaa na vyama vyao vya ushirika walivyozea kufanya. Hapana!

Mkulima apewe/alipwe kwa competitive market rates/bei shindani za soko. Serikali ihakikishe food security hiyo ni kazi yake na hapo hapo maslahi mapana ya mkulima yalindwe.
 
Kenya sio mtoto au mjomba wetu; in fact hajawahi kuwa jirani mzuri. Kenya ni jirani "maslahi ".

Akikuchekea tizama jino pembe
 
Kuna wajinga wengi humu wanadhani tunapoinyooshea vidole wizara ya KILIMO chini ya bashe tuna Nia mbaya na wakulima. Si Kweli.

Wizara hiyo inashirikiana na makampuni hayo kuhujumu USALAMA wa chakula nchini.

Hujuma hii ni hatari Kwa Amani na Utulivu wa Nchi.
 
Uko sahihi kwa hili.
 
Kwamba bashew na makampuni yanayoruhusiwa kununua vyakula direct mashambani ni wakulima hao?

Kwahiyo pale KARIAKOO, wafanyibiashara Kutoka visiwa vya shelisheli waruhusiwe kwenda kununua viungo mashambani, soko la KARIAKOO litabaki na KAZI Gani?
 
Hoja zenu zinafikirisha kana kwamba mnaona kilimo ni sehemu ya watu wanaotakiwa kujitolea
Huyo msomali ni hatari kwa usalama wa nchi yetu lakini bado anaingia kwenye vikao vya juu kabisa vya nchi.

Ana wahujumu watanzania.

Hana uzalendo wowote.

Rais Samia nae Wala hajali.

Wala hajui afanye nini.
 
Zamani tulisikia kauli kama "kama umeshindwa maisha ya mjini nenda kalime" tukaenda kulima. Sasa hivi hao hao waliotufukuza mjini wanaona wivu tusiishi maisha mazuri kwa pesa nzuri ya mazao yetu.

Nyie watu wa mjini mmezidi kudeka. Mkija Krismass mnatulingishia vigari vyenu ila mpaka Samia na Bashe wanaondoka madarakani tutakuwa tumewatia adabu.

Nyie watu wa mjini badala ya kununua stock ya chakula mkaweka ndani nyie mmejaza majumba na maTV, ma-home theater, makochi ya kichina, n.k. mnatumia fedha kwa mashindano kununua mahari na kuyajaza mafuta kila siku hata kama uwezo hamna, mnashindana kumiliki mademu, kununua nguo kila mwezi, kula bata bar n.k lakini kutenga laki 2 ununua gunia mbili za mahindi unaona mkulima anapewa hela nyingi.

Nikushukuru FaizaFoxy kwa kuunga mkono wakulima.
 
Hayo mahindi yaliyokutesa kukausha, ulilimia wilaya ya Rungwe? Maana huko ndio wanakaushia mahindi darini!!!
 
Kenya sio mtoto au mjomba wetu; in fact hajawahi kuwa jirani mzuri. Kenya ni jirani "maslahi ".

Akikuchekea tizama jino pembe
Kwani mkulima anapomwuzia Mkenya ni kwa sababu anataka kumsaidia Mkenya?. Mkulima anatafuta mahali panapoweza kumpa bei nzuri. Iwe ni Kenya, Zambia, Ulaya, na iwe hivyo.

Mkulima anatafuta mahali palipo na maslahi mazuri.

Na hizi story za kusema Kenya.siyo jirani mzuri, acheni hadithi za kipuuzi. Kenya amefanya nini kwa Tanzania mpaka aonekane ni jirani mbaya? Matatizo yenu msibebeshe watu wengine.

Mimi ni kati ya wwtu wanaoathitiwa sana na bei za vyakula, kwa sababu nina wafanyakazi ambao ni lazima niwape chakula wawapo kazini. Wapo wanaokula saa 4 asubuhi na saa 7 mchana, wapo wanaokula milo yote mitatu (walinzi). Zamani nilikuwa natumia milioni 5 kwa mwezi lakini sasa hivi ni milioni 15. Hata hivyo siwezi kuthubutu kushauri mkulima afungiwe masoko, auze tu ndani ya nchi. Safari hii tayari nimeingia makubaliano na wakulima fulani, kuanzia mwezi ujao naanza kukusanya mahindi magunia 800 na mpunga magunia 500 na magunia 200 ya maharage kwaajili ya chakula cha wafanyakazi.

Kila mtu ni lazima aangalie maslahi yake. Wewe kama mwajiriwa, siku zote unafurahia kupata mahali penye mshahara mzuri zaidi, mkulima anamtafuta mnunuzi mwenye bei nzuri zaodi,mnunuzu anatafuta mahali penye bei ndogo, n.k. Ndivyo maisha yalivyo.
 
Pia Bashe akizuia mahindi au mchele usitoke kwenda nje ahakikishe wakulima wanalipwa bei ya masoko yao ya nje !! Sio muwapangie bei mnazotaka ninyi ! Kwani mliwasaidia kulima ??!! Kila mtu ashinde mechi zake !!
 
Umemaliza kila kitu !!
 
Na huo ndio ukweli mchungu !!
 
Tatizo miaka yote wakulima wanachukuliwa kama vile wao ni manamba wa watu wa mijini ! Serikali ni lazima iwalinde wakulima na iwape ruzuku kama inavyowapa ruzuku watu wa vyama vya siasa !! Ikifanya hivyo ndipo itakapokuwa na uhalali wa kuwapangia wauze wapi mazao yao πŸ™πŸ™πŸ™
 
Kwanini utafute unafuu wa Bei Kwa MKULIMA kama una Nia ya kumsaidia MKULIMA?

Hatuna ugomvi na MKULIMA.

Tunataka Serikali inunue vyakula hivyo Kwa Bei ya sasa MKULIMA apate pesa yake ajiandae na msimu ujao.

Serikali Itunze chakula hicho kwenye maghala katika mikoa mbalimbali nchini.

Itakapofika miezi ya Sept Hadi January, Serikali ifungue maghala Ili wakulima na wafanyabiashara masokoni wakinunue tena Kwa Bei nafuu wakati wakisubiri mavuno.

Jambo hili la Serikali kutunza vyakula ktk maghala kutamsaidia MKULIMA akipate chakula hicho hicho alichokiuza wakati ambao Yuko katika kusubiri mavuno.

Sirikali isifuche udhaifu wake Kwa HOJA mufilisi kwamba MKULIMA asipangiwe wapi auze wakati yenyewe hainunui na kutunza ghalani kudhibiti mfumuko wa Bei.

Sirikali imsaidie MKULIMA kutunza chakula ghalani Kwa kukinunua na kumuuzia tena Kwa Bei nafuu.

Mara nyingi UONGO Huwa unaaminika na kupokea kirahisi na haraka na WAJINGA.

Lowassa: ELIMU, ELIMU, ELIMU, ELIMU.
 
Hii comment imefunga mjadala huu !! Umemaliza Mkuu !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…